Nchimbi aunda Tume ya mauaji ya kijana wa Morogoro

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Wanajamvi,

Katika Gazeti la mwananchi leo, kuna taarifa kuwa Waziri wa mambo ya ndani Nchimbi ameamua kuunda tume kufanya uchunguzi wa kijana aliyepigwa risasi na polisi na kufariki dunia mkoani Morogoro, wakati Polisi ilipozuia maandamano ya mapokezi ya viongozi wa Chadema.

Nchimbi anasema kijana huyo alikuwa umbali wa mita 300 toka eneo la vurugu na polisi wala hawaakujua mwanzo kama kuna kijana kajeruhiwa na risasi bali raia waliokuwa naye jirani kijana huyo.

MY Take:
Tume hii itakuwa na jipya?? Sidhani
 
...msanii tu huyu...Ripoti ya mauaji dhidi ya wafuasi wa CHADEMA yaliyofanywa na polisi magamba kule Arusha, Tarime, Igunga, Mbeya iko wapi? Au mauaji yale hayakustahili kufanyiwa uchunguzi?
 
Asipoteze pesa ya walipa kodi za watanzania kwa kuendelea kuzitumia baada ya kumwaga damu zao....Naamini hii sio tume ila ni kikao cha kupongezana cha ile timu aliyoituma iwaue wananchi wasio na hatia
 
Ila yanamwisho, atakapokufa mtoto ama ndugu wa familia zao ndipo watakapojua uchungu wa kuua ndugu zetu
 
[FONT=century
gothic]...msanii tu huyu...Ripoti ya mauaji dhidi ya wafuasi wa
CHADEMA yaliyofanywa na polisi magamba kule Arusha, Tarime, Igunga,
Mbeya iko wapi? Au mauaji yale hayakustahili kufanyiwa
uchunguzi?
[/FONT]

kwani nchimbi alikuwa waziri wa mambo ya ndani wakati huo?
 
Tume ya mauaji ya Arusha vp bado inaendelea na upembuzi yakinifu?
 
kwani nchimbi alikuwa waziri wa mambo ya ndani wakati huo?

Uwaziri sio mtu uwaziri ni ofisi au taasisi kwani wakati huo wizara ya mambo ya ndani haikuwepo? hakukuwa na waziri? tume zilizoundwa mbona hadi leo hazikutoa majibu??
 
Zile zilizopelekea wagonjwa kufa kwa kushinikiza migomo ya madaktari?

Tupatie idadi ya wagonjwa waliofariki kutokana na kadhia ile, sambamba na wanaoendelea kufariki kutokana na ukosefu wa vifaa tiba , madawa na madaktari.
 
Tushachoka na hizi tume za kila siku zisizokuwa na utatuzi wa matatizo ya msingi zaidi ya kutumia kodi zetu wananchi halafu report zinaishia makabatini mm nadhani wangeacha tu likapita sababu hakuna kitakacho fanywa zaidi ya kukaa kimya ukizingatia wabongo tulivyo wasahaulifu wapi dr.uli ashatiwa kapuni nn wadau chezea serikali
 
Wanajamvi,

Katika Gazeti la mwananchi leo, kuna taarifa kuwa Waziri wa mambo ya ndani Nchimbi ameamua kuunda tume kufanya uchunguzi wa kijana aliyepigwa risasi na polisi na kufariki dunia mkani Morogoro, wakati Polisi ilipozuia maandamano ya mapokezi ya viongozi wa Chadema.

Nchimbi anasema kijana huyo alikuwa umbali wa mita 300 toka eneo la vurugu na polisi wala hawaakujua mwanzo kama kuna kijana kajeruhiwa na risasi bali raia waliokuwa naye jirani kijana huyo.

MY Take:
Tume hii itakuwa na jipya?? Sidhani

Tume hii inataka kuchua nani kaua? Hivi video shooting na picha hazionyeshi game lilikuwaje? Sasa nafikiri tumechoshwa na tume na tuungie hatua ya pili ya viongozi wa ngazi za juu kabisa kuwajibika wenyewe bila kuambiwa - Nchimbi ajiuzulu na Bwana Said Mwema pia.

Na hili la kujiuzulu liingie kwenye katiba mpya kwamba any serious problem ikitokea kwenye eneo la kazi basi msimamizi wa juu kabisa wa kitengo hicho aondoke na asipate mafao yake na kufikishwa mahakamani kwa uzembe.
 
He is joking, Kazi ya polisi baada ya kununuliwa silaha za moto ni kuzitumia na pia Ijulikane madhara yake ni pamoja na Vifo!! Kama angekuwa na busara alitakiwa kumzuia Shilogile asizitumie hizo silaha!! Wamemwacha amezitumia madhara yamepatikana sasa ndio wanakuja na single zao ambazo hazina mashiko!!
 
Back
Top Bottom