Nchi za magharibi zimefurahi Dr Slaa kushindwa

Nafikiri hata majirani zetu pia wamefurai. Nchi nyingi zinapenda kushirikiana na sisi kwa sababu viongozi wetu hawajali rasirimali zetu. Dr. Slaa ,kampeni zake lazima ziliwatingisha wanyonyaji, alisema anagombea urais wa Tz sio Africa mashariki, Tanzania kwanza mengine baadaye na rasirimali zetu zinufaishe Tz kwanza. Msimamo kama huu lazima utaogopwa na wanyonyaji. Na nchi nyingi za magharibi ni wanyonyaji na 1.

Umenena, na ungetaja kabisa KENYA. Kichuguu bwana, amezaliwa mwezini huyo. NI TANZANIA PEKEE DUNIANI ambapo utaifa na uzalendo ulikufa siku nyingi. Wenzsetu hata kama ni wafanyabiashara binafsi wanachuma nchi zingine na kupeleka kwao. Na serikali zao zinawahakikishia ulinzi wa mali walizochuma na usalama wao. Wachina wanafanya kwa uwazi kuliko nchi nyingine duniani, maana wao wanakuja kama idara za serikali zao. Usidanganyike Kichuguu, hakuna msaada wa bure! Mzee Matsushita wa Japan ni mfanyabiashara binafsi lakini anatumia pesa nyingi kushawishi Bunge na Serikali yake itoe misaada Tz, halafu anakuja huku anawahi na makampuni yake kibao ya ujenzi nk kuchukua hizo kazi. Hivyo hivyo waswede. Ukiona msaada umekuja ni mtu binafsi ana-loby serkali yake isaidie Tz na kwa ajili hii anakuja huku kufanya hio kazi. Kuna kitabu kizuri unapaswa kusoma wewe 'Rich Dad' - nitakupa full citation baadae Nd Kichuguu- maana wewe ni lazima upigwe darasa la nguvu kweli kweli
 
Kuna watu hapa jamvini wanadhani baadhi ya nchi za magharibi hazijafurahishwa na uchakachuaji wa kura. Naomba tufunguke macho,

Nchi za magharibi hazinufaiki chochote na uamuzi wa wananchi wa nchi hii kama uamuzi huo unawanyang'anya fursa za kuendelea kupora nchi hii. Angalia sera za chadema kuhusu maslahi ya nchi hizi.

Chadema walikusudia kurejea mikataba ya madini, kutonunua mashangingi, kutoa elimu bora bure, kutoa afya bora bure, kutumia gesi asilia kunyanyua uchumi kupitia wazawa, kuwapa wananchi wadaraka zaidi kuliko serikali kuu inayoongozwa na internatinal consultants, etc, etc

jiulize kwa nini JK alialikwa white house baada tu ya Obama kuapishwa. Kwa nini G Bush alitembelea tz kabla ya muda wake kwisha. Kwa nini Iraq ilivamiwa? Kwa nini marekani inawachukia Mugabe na rais wa Venezuela?

Kwa nini Rwanda inaanza kupiga hatua kukuza uchumi wa wananchi wake na nchi za magharibi zinaibua hoja ya demokrasia? Je, maana ya demokrasia kwai ni sawa na ile ya kwetu?

Niliwahi kusema Hapa janvini kwamba nchi hizi haziwezi kufurahia sera na umaarufu wa Slaa. Kwa nini uamuzi wa kuchapa karatasi za kura nje ya nchi ulifanyika gafula baada ya kugundua Slaa ni tishio?

Heading ya hii thread ilitakiwa kusomeka: Nchi za Magharibi zimefurahi JK kumwibia kura Dr. Slaa.
 
Heading ya hii thread ilitakiwa kusomeka: Nchi za Magharibi zimefurahi JK kumwibia kura Dr. Slaa.

mkuu, nakubaliana na wewe nadhani hiyo heading yako imetulia zaidi. hivi kuna uwezekano wa ku edit heading?
 
Kikwete hajawahi kualikwa White House baada ya Obama kushinda. Kikwete alilobby, kupitia Goodworks International kupata nafasi ya photo op na Obama Ikulu. Ilitugharimu $500k
 
Kikwete hajawahi kualikwa White House baada ya Obama kushinda. Kikwete alilobby, kupitia Goodworks International kupata nafasi ya photo op na Obama Ikulu. Ilitugharimu $500k

ni kama shilingi ngapi hizo?
 
Kuna watu hapa jamvini wanadhani baadhi ya nchi za magharibi hazijafurahishwa na uchakachuaji wa kura. Naomba tufunguke macho,

Nchi za magharibi hazinufaiki chochote na uamuzi wa wananchi wa nchi hii kama uamuzi huo unawanyang'anya fursa za kuendelea kupora nchi hii. Angalia sera za chadema kuhusu maslahi ya nchi hizi.

Chadema walikusudia kurejea mikataba ya madini, kutonunua mashangingi, kutoa elimu bora bure, kutoa afya bora bure, kutumia gesi asilia kunyanyua uchumi kupitia wazawa, kuwapa wananchi wadaraka zaidi kuliko serikali kuu inayoongozwa na internatinal consultants, etc, etc

jiulize kwa nini JK alialikwa white house baada tu ya Obama kuapishwa. Kwa nini G Bush alitembelea tz kabla ya muda wake kwisha. Kwa nini Iraq ilivamiwa? Kwa nini marekani inawachukia Mugabe na rais wa Venezuela?

Kwa nini Rwanda inaanza kupiga hatua kukuza uchumi wa wananchi wake na nchi za magharibi zinaibua hoja ya demokrasia? Je, maana ya demokrasia kwai ni sawa na ile ya kwetu?

Niliwahi kusema Hapa janvini kwamba nchi hizi haziwezi kufurahia sera na umaarufu wa Slaa. Kwa nini uamuzi wa kuchapa karatasi za kura nje ya nchi ulifanyika gafula baada ya kugundua Slaa ni tishio?

... in short BARRICK na lobbysts wake wasingependa wanyanganywe ulaji, BASTA. Na wale wanaohemea kwao pia wasingependa. At the end of the day, kwani nchi za magaharibi ni MUNGU??
kwa staili yangu, ningeseam so what??? Ikumbukwe leo hii Mchina ni namba mbili, na soon second to none. Mwalimu (RIP) aliona mabali sana kwa kushupalia ile kitu cha SOUTH commission... yaani, the demise of North Atlantic powerhouse was imminent.
Kwa hiyo tunaweza sana kusema, who gives a damn (kind word) what they think?
 
kuna watu hapa jamvini wanadhani baadhi ya nchi za magharibi hazijafurahishwa na uchakachuaji wa kura. Naomba tufunguke macho,

nchi za magharibi hazinufaiki chochote na uamuzi wa wananchi wa nchi hii kama uamuzi huo unawanyang'anya fursa za kuendelea kupora nchi hii. Angalia sera za chadema kuhusu maslahi ya nchi hizi.

Chadema walikusudia kurejea mikataba ya madini, kutonunua mashangingi, kutoa elimu bora bure, kutoa afya bora bure, kutumia gesi asilia kunyanyua uchumi kupitia wazawa, kuwapa wananchi wadaraka zaidi kuliko serikali kuu inayoongozwa na internatinal consultants, etc, etc

jiulize kwa nini jk alialikwa white house baada tu ya obama kuapishwa. Kwa nini g bush alitembelea tz kabla ya muda wake kwisha. Kwa nini iraq ilivamiwa? Kwa nini marekani inawachukia mugabe na rais wa venezuela?

Kwa nini rwanda inaanza kupiga hatua kukuza uchumi wa wananchi wake na nchi za magharibi zinaibua hoja ya demokrasia? Je, maana ya demokrasia kwai ni sawa na ile ya kwetu?

Niliwahi kusema hapa janvini kwamba nchi hizi haziwezi kufurahia sera na umaarufu wa slaa. Kwa nini uamuzi wa kuchapa karatasi za kura nje ya nchi ulifanyika gafula baada ya kugundua slaa ni tishio?

nadhani kikwete anatafuta kazi ya house boy ikulu ya marekani ndo maana wanamwandaa.
 
kuna watu hapa jamvini wanadhani baadhi ya nchi za magharibi hazijafurahishwa na uchakachuaji wa kura. Naomba tufunguke macho,

nchi za magharibi hazinufaiki chochote na uamuzi wa wananchi wa nchi hii kama uamuzi huo unawanyang'anya fursa za kuendelea kupora nchi hii. Angalia sera za chadema kuhusu maslahi ya nchi hizi.

Chadema walikusudia kurejea mikataba ya madini, kutonunua mashangingi, kutoa elimu bora bure, kutoa afya bora bure, kutumia gesi asilia kunyanyua uchumi kupitia wazawa, kuwapa wananchi wadaraka zaidi kuliko serikali kuu inayoongozwa na internatinal consultants, etc, etc

jiulize kwa nini jk alialikwa white house baada tu ya obama kuapishwa. kwa nini g bush alitembelea tz kabla ya muda wake kwisha. Kwa nini iraq ilivamiwa? Kwa nini marekani inawachukia mugabe na rais wa venezuela?

Kwa nini rwanda inaanza kupiga hatua kukuza uchumi wa wananchi wake na nchi za magharibi zinaibua hoja ya demokrasia? Je, maana ya demokrasia kwai ni sawa na ile ya kwetu?

Niliwahi kusema hapa janvini kwamba nchi hizi haziwezi kufurahia sera na umaarufu wa slaa. Kwa nini uamuzi wa kuchapa karatasi za kura nje ya nchi ulifanyika gafula baada ya kugundua slaa ni tishio?

kikwete anatafuatilia kazi yake ya u-house boy kwa obama. Lakini blog moja jana ilisema ukimwona anasafiri sana anakwenda kuchukua vidonge.
 
Chadema ni Central Right Party -- Masuala yake ya kiuchumi ni ya kibepari(Capitalistic) Nchi za kibepari kinakipenda chama hicho zaidi

Lakini Ukisema Nchi zinazopenda kuibia nchi za africa rasilimali yeah watipenda CCM kwa udi na uvumbi angalia GOLD inapanda bei kila siku lakini hakuna maisha bora GEITA au Kule Musoma

Sasa Weigh CCM (WIZI) au CHADEMA (UBEPARI WA HAKI) kila mtu atapenda wizi wa kiusalama --- watanzania tuko wapole chini ya CCM na vyombo vyake
 
Lazima wafurahie si wanajua moto ungewawakia!
unajua wanafaidi sana kwa uzezeta wetu wa kuomba misaada na wao wanapenyeza mambo yao. na wanajua Dr. Slaa hangekuwa na utaahira huo. Sisi sio wakuomba misaada bali wa kuombwa misaada na nchi masikini kama malawi, burundi rwanda n.k kwasababu vingi tulivyonavyo hawana na hivyo kuttufanya matajiri lakini kwa akili ya mkerw du!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kuna watu hapa jamvini wanadhani baadhi ya nchi za magharibi hazijafurahishwa na uchakachuaji wa kura. Naomba tufunguke macho,

Nchi za magharibi hazinufaiki chochote na uamuzi wa wananchi wa nchi hii kama uamuzi huo unawanyang'anya fursa za kuendelea kupora nchi hii. Angalia sera za chadema kuhusu maslahi ya nchi hizi.

Chadema walikusudia kurejea mikataba ya madini, kutonunua mashangingi, kutoa elimu bora bure, kutoa afya bora bure, kutumia gesi asilia kunyanyua uchumi kupitia wazawa, kuwapa wananchi wadaraka zaidi kuliko serikali kuu inayoongozwa na internatinal consultants, etc, etc

jiulize kwa nini JK alialikwa white house baada tu ya Obama kuapishwa. Kwa nini G Bush alitembelea tz kabla ya muda wake kwisha. Kwa nini Iraq ilivamiwa? Kwa nini marekani inawachukia Mugabe na rais wa Venezuela?

Kwa nini Rwanda inaanza kupiga hatua kukuza uchumi wa wananchi wake na nchi za magharibi zinaibua hoja ya demokrasia? Je, maana ya demokrasia kwai ni sawa na ile ya kwetu?

Niliwahi kusema Hapa janvini kwamba nchi hizi haziwezi kufurahia sera na umaarufu wa Slaa. Kwa nini uamuzi wa kuchapa karatasi za kura nje ya nchi ulifanyika gafula baada ya kugundua Slaa ni tishio?

Umezungumza point ambazo ni tofauti kabisa. Kwanza umesema sera za Chadema ni kwamba, elimu bure, afya bure, halafu wananchi watakuwa na madaraka zaidi, huh?

Unaposema kwamba Serikali itatoa huduma bure kwa wananchi, ujue kwamba hapo tayari umeshawaondoa Wananchi ktk private sectors. Kwa hiyo kila kitu kinahudumiwa na Serikali,= Ujamaa.
Sasa, swali, wakati wa Nyerere, je Wananchi walikuwa na madaraka? Kama sectors zote zinamilikiwa na serikali, ina maana kwamba central governmant itakuwa na nguvu sana. Hapo ndipo ujue kwamba sera za Chadema zinajicontradict itself.
 
Magharibi wameendelea kwa kufuata mifumo ya kwao, singapore,china,urusi n.k.Hivyo basi africa kuendelea ni mpaka pale tutakapoachana na mifumo ya magharibi,mpaka hapo akili zetu zitakapofanya kazi vizuri.tumekuwa mazuzu wa kuambiwa fanya hivi,fanya vile kwa ujinga wetu tusijue kwamba tunafanya kwa maslahi yao na si ya kwetu.Africa na hii Tz kutakucha lini?
 
GURUDUMU: Tueleze na utusema haswa kwa sababu wanadhani nchi za magharibi zinania ya dhati ya kuona mambo yanakuwa mazuri katika nchi kama ya Tanzania. Leo hii kwa wale wachache mliotembelea hizo nchi wanazosema zimeendelea ni kweli zimeendelea kwa migongo yetu na mali zetu na wakipata mazuzu kama haya yaliochukua uongozi wa nchi yetu wanashangilia badala ya kulaani. Ukweli ni rasilimali za dunia ni adimu (Natural Resources are limited).

  1. Asilimia 80 ya rasilimali asili za dunia hii na vitu vitokanavyo navyo vinatumiwa na asilimia 20 tu ya watu wanaokaa katika nchi ZILIZOENDELEA: hapa nina maana ya madini (mfano uranium kutengeneza umeme), maji, matunda, mbogamboga, fukwe, mbao.
  2. Chini ya asilimia 20 ya rasilimali za dunia na vitu vitokanavyo na rasilimali hizo ndizo zinazotumika katika nchi ZINAZOENDELEA na watu asilimia 80 ya dunia nzima WANAOISHI KATIKA NCHI HIZO.
  3. Sasa basi unapotengeneza mazingira ya kupunguza kiwango cha rasilimali zinazotakiwa ku sustain maisha ya wazungu lazima uwe mbaya-Msimamo wa Slaa unawaumiza wazungu SI RAHISI WAMKUBALI HATA WAKISEMA JAMBO NI UNAFIKI WA KIZUNGU AMBAO TUMEZOEA.
  4. Unapokuwa mjanja kwa maana ya kupata elimu ambayo itakwenda kinyume na matakwa ya wazungu ni lazima ukosane nao na ndio sababu wao wanatoa elimu bure lakini hawataki sisi tutoe elimu hiyo bure. Lakini jingine ambalo hatujagundua ni utarabu wa makampuni kama BARICK wa kupita katika mashule yetu ya msingi na kuchagua WATOTO WETU ambao ni BRIGHT na kuwapeleka katika nchi zao kuwasomesha kwa lengo la kuwabraini wash ili wakirudi nyumbani wawe maCEO wenye sura Za kitanzani na fikra ZA kizungu huku wakitetea maslai ya wazungu.
  5. Wanaharibu elimu yetu mfano maprofessor KAPUYA mmoja wapo anatumiwa kuharibu mitaala yetu kwa kuanzisha masomo ya ajabu physichemistry.
  6. TUSIWATEGEME WAZUNGU TUFANYE MAAMUZI YETU TUENENDE KWA MTINDO WA SERA ZA NYERERE TUFANYE TU KILE AMBACHO KINA MASLAHI KWETU. LEO HII TUNA URANIUM JE MKATABA TULIOINGIA NA AUSTRALIA UTATUWEZESHA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITANO KUWA NA KINU CHA KUFUA UMEME ILI TUONDOKANE NA TATIZO LA UMEME TZ. HIZO FIKRA HAZITEKELEZEKI KWA VIONGOZI WETU MABUNJU WANABAKI TU KUWAKUMBATIA KWA KUSEMA IF OBAMA SAYS YOU ARE A GOOD MAN HE MEANS IT-RABISH- SLAA WAKUPENDE WASIKUPENDE CHA MUHIMU NI KILE AMBACHO WATANZANIA WANANUFAIKA NACHO NA SI WAZUNGU SONGA MBELE BABA
 
$ 500k * Shs 1500 = Shs 750 million

Halafu nakumbuka jk alionekana kwene tv amekaa kashika bunda kubwa la karatasi za hadidu alizokuwa ameaandaliwa na wasaidizi wake. Lakini Obama alionekana mikono mitupu lakini anayafahamu matatizo ya tz fika
 
Soko huria si kitu kibaya lakini ni kwa kiasi gani tuachie soko huria kufanya kazi. Huduma muhimu za kijamii kama elimu, afya ni muhimu pakawepo mkono wa serikali. Marekani ni moja ya nchi ambazo zinaongozwa na market mechamisms lakini wameona haifai wamekuja na issue ya afya bure,wana public universities ambazo watu wao wanasoma bure lakini bado ni nchi inayoendeshwa na soko. Dr slaa hajasema serikali ianzishe viwanda vya kuteneza juice au magari, bali anazungumzia sekta ambazo zinamjenga mtanzania kuweza kupata fursa za kujitegemea kama elimu, afya ambazo ni muhimu serikali ikaingilia kwa vile soka huria halimtendea haki yule asiye na uwezo. Kama wakati wa nyerere elimu isingekuwa bure leo hii mkwere wetu angekuwa wapi-labda angekuwa mganga wa kienyeji.
 
Back
Top Bottom