Nchi yetu masikini?-tembelea India.

Majoja

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
612
186
Katika jiji la Chennai, nilikuta hii katikati ya jiji.Mgambo hawathubutu kuwaondoa hawa jamaa. DSC00624.JPG
 
Sawa lakini hatuwezi kujifariji kwa hilo kwani miaka 50 ya uhuru tulitakiwa tuwe mbali kama si hawa magamba kutufanya hivi.
 
Katika jiji la Chennai, nilikuta hii katikati ya jiji.Mgambo hawathubutu kuwaondoa hawa jamaa.View attachment 36073
Hii picha hai'justify umasikini hata kidogo!
Hicho kibanda ni cha aina ya kupumzikia, na ni cha kiasili fulani!
Huoni context ya eneo lenyewe?...kUNA MAGOROFA hapo, na inaonyesha ni downtown fulani!
Useme shida ya hapo ni makaratasi na uchafu mwingine kuzagaa!
 
Bwana mukubwa sijustify umasikini wetu, lskini masikini kama sisi wanaendelea tena vibaya sana.
Hapo chini ni maendeleo ya Mumbai, but elements za umasikini zipo-cheki smog
India  and Bombay 088.JPG
 
Sawa lakini hatuwezi kujifariji kwa hilo kwani miaka 50 ya uhuru tulitakiwa tuwe mbali kama si hawa magamba kutufanya hivi.

India  and Bombay 089.JPG
Masikini wenzetu wanafanya serious construction, tena kwa kutumia vifaa vyao wenyewe(Indian lorry in the picture).
Hiyo barabara ni elevated.
 
nchi yetu sio maskini bali utawala wetu ndio mbovu wa kimasikini hivyo kutujengea fikra za kimaskini
 
nchi yetu sio maskini bali utawala wetu ndio mbovu wa kimasikini hivyo kutujengea fikra za kimaskini

Kama masikini wako uwasingizie wengine ndio wamekujengea, pole sana! aliyewatia umaskini wa fikra Watanzania alisha kufa zamani sana. Kama mpaka leo bado fikra zako ni za kimaskini basi hautoamka tena. Hivi unangoja Serikali ije kukupa fedha utajirike? Unanchekesha!

Fanya kazi kwa bidii, hutofanikiwa kwa kupiga firimbi JF. Utawaona tu wenzako wakipaa wewe baki kulalama hapa!
 
Tanzania ni maskini hakuna mfano. Ukizingatia hatujawahi kuwa na vita au janga kama tetemeko au mafuriko maharibifu nk.

Hii yote ni kwa sababu sisi watz plus serikali ni wavivu sana, tunapenda porojo bt no actions.

Serikali yenyewe kutwa mguu na njia kuomba omba nchi za watu. soo sad.
 
Ni kweli kuwa India wana viwanda vingi na kiteknolojia wanatuzidi.

Ni kweli pia kuwa kuna matajiri wengi wakubwa nchini India.

Ni kweli pia kuna middle class kubwa India.

Lakini ikumbukwe kuwa India ni nchi yenye watu wengi sana, zaidi ya Bilioni moja. (about 1.2 billion)

Asilimia ya watu wanaoishi katika umaskini wa kupindukia nchini India ni kubwa zaidi ya Tanzania. (42% kwa India na 35% kwa Tanzania)

India watu 20% walio matajiri wa juu wanamiliki 45% ya utajiri wa nchi yao, na 40% wa chini kwa utajiri/umaskini wanamiliki 19% ya utajiri wa nchi yao. Source: UNICEF - India - Statistics kwa India na http://www.imf.org/external/np/prsp/2000/tza/02/100100.pdf kwa Tanzania

Kitu ambacho ni positive sana kwa India ni kwamba wanapunguza umaskini kwa kasi. Mwaka 1985 waliokuwa kwenye umaskini wa kupindukia walikuwa 60% ya Wahindi, na sasa ni karibu 40%, wakati sisi ni kama tunarudi nyuma.

Maskini wa Tanzania ambao wako vijijini bado wanaweza kuwa na ardhi ya kulima na kujenga, India ardhi ni ndoto kwa maskini yeyote. Hapo ndio tofauti kubwa.

Mimi mwenyewe nimeishi India na hivyo binafsi nina ulinganisho wa kushuhudia
 
Kama masikini wako uwasingizie wengine ndio wamekujengea, pole sana! aliyewatia umaskini wa fikra Watanzania alisha kufa zamani sana. Kama mpaka leo bado fikra zako ni za kimaskini basi hautoamka tena. Hivi unangoja Serikali ije kukupa fedha utajirike? Unanchekesha!

Fanya kazi kwa bidii, hutofanikiwa kwa kupiga firimbi JF. Utawaona tu wenzako wakipaa wewe baki kulalama hapa!

Faiza naona umerudi kiaina. Habari za kule Jamii nyingine?
 
Nimewahi kutembelea Jiji la Bombay kuna eneo linaitwa Churchgate, hapo ni balaa tupu umasikini usio na mfano. Afadhali ya kwetu TZ. Umewahi kuona film ya Slum dog millionear? That is a real life ya India.
 
sina hakika kama ni india kweli! nahisi ni mtaa mmoja wa wahindi dar
Cheki vizuri hizo picha au enlarge. Mabango yote ni ya kihindi.Sina sababu ya kuleta kitu feki,na picha zote nimepiga mwenyewe.
 
Back
Top Bottom