Nchi yetu kuvamiwa

idumu

Member
Jun 5, 2009
44
1
Habari wana JF, Hivi sisi kama watz tunatafakari vipi kuhusu kujaa kwa wachina nchini, wakenya. Hivi wewe MTZ waweza kwenda china kirahi tu na ukaishi. Hili suala hata kama ni uwekezaji, MCHINA ANAUZA MTUMBA. Hawa jamaa wakizaana hapa bongo tutakoma. Kuwaondoa itakuwa taabu, Pembe za ndovu zinapotea, Kama Jana uliona ITV pembe za ndovu zinaibiwa hiv hiv?/ Hongera kwa POLISI kuwakamata. Je wewe kama Kiongozi wa UHAMIAJI na USALAMA WA TAIFA MNAFANYA NINI ILI TUIKOE HII NCHI YETU JAMANI.

Bless, Maoni yangu
 
Jana nilikuwa nasoma gazeti la Raia Mwema makala ya Johnson Mbwambo.Nilivutiwa na hoja yake kwamba serekali ya China ina sera ya kuwasambaza raia wake sehemu mbali mbali duniani hasa Afrika kwasababu hawana mahali pa kuwaifadhi.

China inakadiriwa kuwa na idadi ya watu 1.3 bilioni kwa sasa. China ina sera ya kununua ardhi hasa katika nchi za Afrika zinazopokea msaada kutoka China,tayari imeshanyakua mamilioni eka nchini Kongo Brazaville.Sitashangaa kama wachina watakujapewa mamilioni ya eka hapa Tanzania au tumesahau mkuu wa kaya tayari kesha wamegea waarabu wakati ndugu zetu Wameru mkoani Arusha hawana ardhi ya kutosha hadi wakaamua kumtolea uvivu Mheshimiwa Kimaro.

Mwaka jana mwishoni nilipita mitaa ya Kariako nilidhani niko Shanghai jinsi wachina walivyojazana. Aina ya biashara wanayofanya wachina ni pamoja na kuuza maua,vitambaa,vyombo vya udongo na biashara zote ndogo ndogo wanazoweza kufanya wazawa.

Raia wa Kenya wamejaa kupita kiasi hasa katika sekta ya utalii, madereva, mahotelia katika mji wa Arusha hakuna mahali utakapowakosa. Nawashangaa idara ya uhamiaji sijui wanafanya kazi gani.Nilipata bahati ya kutembelea mbuga za wanyama mwezi uliopita yaani kila hotel utakayotia mguu imejaa wafanyakazi kutoka Kenya. Sio siri hawa jamaa wamechukuwa ajira za watanzania yaani mpaka mbeba mizigo ya wageni ni wao! Tusisahau Tanzania haijaridhia kile kipengele cha free movement of labour [EAC], hali iko hivi je siku ikafika Tanzania ikaridhia hicho kipengele hali itakuwaje?.

Wizara ya kazi ajira na Wizara ya mambo ya ndani zinahitajika kuchukuwa hatua haraka kukabiliana na ongezeko la wageni wanaovamia ajira na fursa za watanzania.
 
Katika hili, mambo mengi twajitakia kutokana na njaa zetu. Uhamiaji, polisi. n.k. ukiwa na mgeni aka mwekezaji, ambaye kupitia kwake unapata mlo wako wa kila siku, bila kujali madhara au kwamba akishapata documents zinazomwezesha kuishi na kufanya kazi Bongo, atakunyanyasa na kukusimanga na hata kukutimua kama tayari alishakuajiri kwenye kampuni (duka la kuuza maua, vitambaa, vyombo vya udongo (ceramics), n.k.). Cha muhimu ni UZALENDO NA KUIPENDA nchi yetu, hao ni wageni tu hawatufikishi popote! Hata travel agency nyingi utakuta ni wahindi, unaweza kusema WATANZANIA WENYE ASILI YA KIASIA, likini je ni mtanzania gani asiyependa kuongea kiswahili?? Mmenielewa waungwana! CHUNGUZENI WAJOMBA, MTABHAINI!!!
 
vIONGOZI ETI WANAJIVUNIA waTz tunapenda sana wageni lakini athari zake baadae ni kubwa kama hatua hazitachuliwa mapema,Mh Lukuvu Mkuu wa Mkoa Dsm alitoa tamko wachunguzwe hawa wawekezaji wa Kariakoo(CHINESE) kama wanasifa thabiti za uwekezaji sijui kama hilo limetekelezwa na wahusika! na wale madada poa wa kichina na kihindi mikocheni ni uozo mtupu wa wawekezaji hao.
Mi nahisi tusipowadhibiti ipo siku watatuchezea mpaka masharubu yetu.
 
Mara zote watanzania tumekuwa tukisubiri athari za globalisation!

Hamjazuiwa kwena china, nendeni muone kama mnaweza, nchi kama ya canada ili kuwa accomodate hawa jamaa, hata ATM machine zinaandikwa kichina, wako wengi hamna mfano!

tubadilishe mifumo yetu ya elimu, viongozi wawe serious ili tuwe competent dunia ya sasa hatutaweza kuwa kisiwa.

Japo ukweli unabaki palepale kosa lilishafanyika, hatukuwa tayari kuingia dunia hii ya globalisation, mpaka sasa inaonekana hatuko tayari, hii ni kuwa na viongozi vipofu, wenye kufuata matakwa ya watu wa dunia ya kwanza, hatujawahi kujisimamia na kamwe haitakuja kuwa hivyo

ukiwafukuza hawa wachina au kuwawekea ngumu athari yake kwa sasa itaonekana!

umeshawahi kujiuliza kwa nini kwenda nchi za ulaya na amerika ni kazi sana lakni wao kuja kwetu ni rahisi ka kwenda sokoni??

hii athari haitakiwi inatakiwa kujadiliwa kitaifa, lakinitu iwapo na sisi tupo tayari kubadilika kuchagua viongozi wenye vision

CCM walishauza nchi hii siku nyingi sana tangu enzi za mwinyi , nyio wachekeeni!
 
Dawa ni kuwa na vitambulisho vya uraia kukomesha wakenya na wageni wote kuvamia nchi.

Uhamiaji wae makini sana katika kutoa permit kwa wageni wanaokuja kufanya kazi.
 
We have to have an East African spirit, mimi naamini hilo. Tanzania geographically ilitengenezwa na wakoloni for their convinience it was not our will ndio maana makabila kama wamaasai, wakuria, wadigo, wajaluo wamegawanywa. Kabila la wadigo limeanzia toka Momabasa pale Likoni Ferry mpaka Tanga wajomba shangazi wamezagaa nchi zote mbili. Na believe you me, Mji wa Mombasa una Watanzania wengi sana. From my perspective zaidi ya nusu ya wakaazi wa Mombasa (Kenya) ni watanzania au wana asili ya Tanzania au wana undugu na Tanzania.

Miaka ya sabini wahaya wengi wakina mama walimiminika Mombasa na mpaka leo hawajarudi. Wengi wao walienda kufanya biashara ya kuuza miili yao maeneo ya Bondeni kwa kitsao, Msufi mkavu, Mwembe Kuku etc. Wazee wengine walienda Mombasa kwa sababu ya hali ya kiuchumi Bongo ilikuwa mbaya enzi hizo za kupanga foleni kununua maziwa. Hawa walioenda Mombasa walipofanikiwa walibeba ndugu zao kwa fujo tena sana. Watangazaji redio wengi pia walikimbilia Kenya, vijana wa Tanga na Dar es salaam walienda Mombasa kuzamia Meli enzi hizo miaka ile bahari ya Mombasa ilikuwa imesheheni meli (Ubaharia ulikuwa dili).


Wachagga nao walienda Mombasa wakijifanya wao ni wataveta maana wanafanana kiaina. Askari polisi wa Kenya kutoka maeneo bara hawezi kutambua tofauti ya Mchaga na Mtaveta. Wapare nao walipofika Kenya wanajifanya wao ni Wataita. Mdigo wa Kenya na Mdigo wa Tanzania hata mimi nashindwa kumtofautisha.

Kwa kifupi Watanzania walipokuwa Kenya (Mombasa) walipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wenyeji kiasi kwamba waliweza kujumuika nao na kujifanya wakenya. Believe you me, most of the Natives of Mombasa wako Nairobi sasa hivi maana wengi wao ni wasomi. Kwa hiyo wengi waliobaki Mombasa ni watu wenye asili ya Tanzania maana nyakati zile hawakutilia maanani mambo ya shule walienda Mombasa kuepuka utaka uliokuwa unawasonga. Mombasa kiuchumi sio kama ile ya zamani imeshuka kweli. Most of the people are migrating to Nairobi. Kuna viwanda kadhaa vimefungwa ikiwemo cha bia (EABL).

Wamaasai huwa wanapita border bila passport nimeshaona kwa macho yangu. Do you think you can know the difference between a Kenyan Maasai and a Tanzanian Maasai? Nafahamu sana muingiliano wa makabila ya sehemu za Mwambao.


Kwa uhakika movement ya watu kati ya Kenya na Tanzania haiwezi kudhibitiwa hata kidogo, kuna uhusiano mkubwa wa hali ya juu. Mpende msipende udugu ni mkubwa. Kuna makabila mengi yamehusishwa hapa. Wadigo, Maasai, Wakurya, Wajaluo, (Wataveta-Chagga), (Wapare-Wataita), Waarabu nao wamechanganya nchi zote mbili, usiwahau Wahindi.

In my perspective we should think as East Africans, najua wengi wanawaogopa wakenya, then this shows explicitly that we are not competent in what we are doing. The proctectionism until when?
 
Last edited:

Similar Discussions

Back
Top Bottom