Nchi Yetu Haipo Salama

Gamba la Chuma

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
1,243
340
Nafanya tafakuri ya masahibu yaliyomkuta mpambanaji Mh. Mwakyembe (Mb) NW.

Nashindwa kabisa kupata picha, Waziri ambaye yupo madarakani, zaidi ya mwaka uliopita alitoa taarifa na ushahidi kuhusu tishio dhidi ya uhai wake. Taarifa hiyo ilipuuziwa na vyombo husika, na leo kwa mujibu wake amewekewa sumu, bado vyombo husika vinapuuzia. Na zaidi Waziri mwingine anajaribu kuwasisitizia ukweli wa Mwakyembe kuwekewa sumu, wanadai alete ushahidi. Je, sio kazi ya Polisi kutafuta ushahidi baada ya kupelekewa taarifa au tetesi.

Nasema nchi haipo salama kwa kuwa kama kwa Viongozi wakuu hawa inakuwa hivi, je kwa mwananchi wa kawaida inakuwaje?

Angelalamika mwekezaji ingekuwa hivyo?

Hakuna haki, watu wengi wanauawa bila kosa, na jela wamejaa watu wengi wasio na hatia kutokana na serikali iliyojaa ubinafsi na kuangalia maslahi yake na vibaraka wachache.

Serikali sasa sio ya Watanzania bali ni ya kundi fulani la watu.

Inasikitisha kuona nchi imekuwa kama haina uongozi, leo si ajabu Rais na PM kupishana kauli, Spika kuwa na misimamo ya kibinafsi, na hata wazee wetu ni kama hawapo.

Nchi haipo salama kabisa!
 
Avatar yako imenifanya niamini tanzania haiko salama.
Inflation rate imepanda zaidi ya 20%, zimbabwe mtoto
 
nchi haiko salama kama mawaziri nao wanalalamika na kuambiwa wapeleke ushahidi...............
kazi ipo ..........
Tanzania aliyeturoga atakuwa amekufa...........
 
nchi haiko salama kama mawaziri nao wanalalamika na kuambiwa wapeleke ushahidi...............
kazi ipo ..........
Tanzania aliyeturoga atakuwa amekufa...........

Alituroga Sheikh Yahya Hussein na sasa amekufa!!! Ulikuwa hujui?
 
Back
Top Bottom