Gembe
JF-Expert Member
- Sep 25, 2007
- 2,483
- 159
Heshima Mbele,
Jana nilikuwa naongea na mpwa wangu kuhusuiana na mipango yake ya shule hasa ya chuo kikuu anakosoma,katika maelezo yake alilaumu jinsi ya ufundishaji katika vyuo,mpwa wangu aliniambai kuwa hawapi elimu kwa vitendo na ndiyo inachangia wao kutokuwa na uwezo wa kujieleza na kujiamini.
Maelezo haya yalivuta hisia zangu sana,nikakumbuka mambo mengi sana ya zamani na pia tabia ya sasa ya watanzania ya kulalamika tu bila kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na matataizo yaliyopo hapa nchini
Mtakumbuka toka miaka ya tisini mpaka elfu mbili,wanachi wengi wa nchi hii imekuwa na watu wa kulalmika elimu yetu haiwezi kuendelea kwa kuwa elimu yetu haijali elimu kwa vitendo.tumeendelea kulia kulia sana na hili jambo bila ya sisi wenyewe kujaribu kutatua tatizo lenyewe kwa kuanzakubadilika.Tunajua tatizo ni nini ila tumebaki kulalamika tu!
Tabia hii imeka vichwani mwetu na imejengeka mpaka sasa,tumekuwa watu wa kuilaumu serikali tu,tumekuwa tukiwalaumuwatu flani kwa kutufikisha hapa.
Je tumefanya nini kuondokana na tatizo hili?uwezo tunao na sijui tunangoja nini?tumekuwa wa tu wa kulalamiak tu na baadaey tunarudisha watu wale wale na kibaya zaidi wasiojua kwa nini wao ni viongozi(Rejea chenge aliyesema kamuulizeni Rais kwa nini alinichagua)
Ndiyo tupo kwenye nchi ambayo viongozi wakishachukua madaraka wanatoa ahadi nyingi ila badaye wanatupuuza na kutudharau kwa kuwa watanzania ni mandondocha sasa hivi wamerudi mikoani huko kuwaomba kura,wameamua kuwa karibu na nyie kwa kuwa kampeni ni 2010.
Naomba sa kutoa wito kwa wanachi wote
1.Kwanza Tuanze upya mwaka 2010,tiusahau yote na tukubali sawa walituibia,kama anavyosema mwanakijiji siku zote tuanze uoya na tukubali kuna sehemu tulikosea,imetosha sasa na nina amani kabisa akili mnazo na uwezo mnao,kama mnahitaji maisha bora ni wakati huu sasa kuweka wabunge ambao wataleta maendeleo.
2.Kataa kabisa kupigia kampeni watu ambo pesa yao ni ile imetokana na kodi yako,usipokee Rushwa kwa kuuza haki yako,hata kama ni chaguo la Rais kataa kabisa mawazo yake na huu uwe mwanzo wa Tanzania ile uipendayo!
Enyi wanachi mlio wakimya,wapole,mlio na uwezo wakushika yale mnayoona ni madogo na kusahu makubwa nawaapieni Kama ukishindwa kuamua
1.Mtaendelea kupuuzwa na kuhudumia wagonjwa!
2.Mtaendela kuishi maisha ya kifukara na kimasikini milele
3.Mtandelea kupuuzwa!
4.Dhahabu na utajiri wote uliopo nchini utachukuliwa na wageni
Tuacheni kuilalamika,tuchukue hatua na kuhakikisha tunaanza upya 2010.
Nawatakieni maandalizi mema na naomba CCM ijetenge ili kufanikisha hili!

- Tumelalamika kuhusiana na IPTL wakasikiliza na baadaye wakatupuuza
- Tumelalamika kuhusiana RDC wakatusikiliza na baadaye wakatupuuza
- Tumelalamika ujenzi wa BOT-Twin Towers ,wakatuikiliza ila wakatupuuza
- Tumelalamika kuhusu EPA,wakatusikiliza,wakaweka usanii alafu wakaamua kutupuuza
- Tumelaamaika kuhusu na Dowans,wakatusikiliza ila badaye watatupuuza
- Tumelalamika kuhusu Import Suuport,wakaamua kukaa kimya na kutupuuza
- Tumelalamika maisha magumu na wao wanaendelea kufuja pesa zetu kwa safari ila wanapuuza

Last edited: