Nchi ya Norway Sio Salama Tena...!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Norway ilihusika sana na kuleta maridhiano Mashariki ya Kati kati ya Waisraeli na Wapalestina mpaka yakapatikana maridhiano (Oslo Agreement) mwaka 1993, na ilionekana kwamba nchi hiyo ya Skandinavia ni nchi isiyoegemea upande wowote (neutral). Lakini sasa hivi mambo yamegeuka. Osama bin Laden ameanza kuleta makeke huko, nchi hiyo, kama zilivyo nchi nyingi za Ulaya kwa sasa, sio salama tena kwa upande wa ugaidi wa kiislamu!

Source: BBC na Al Jazeera.
 
Osama na Mtandao wake Hawana urafiki na Mtu; Nafiki hata wao kwa wao ni maadui na wanaweza kulipuana muda wowote.
 
Osama na Mtandao wake Hawana urafiki na Mtu; Nafiki hata wao kwa wao ni maadui na wanaweza kulipuana muda wowote.
Kweli, Iraq karibu wanamalizana wao kwa wao!
 
Norway ilihusika sana na kuleta maridhiano Mashariki ya Kati kati ya Waisraeli na Wapalestina mpaka yakapatikana maridhiano (Oslo Agreement) mwaka 1993, na ilionekana kwamba nchi hiyo ya Skandinavia ni nchi isiyoegemea upande wowote (neutral). Lakini sasa hivi mambo yamegeuka. Osama bin Laden ameanza kuleta makeke huko, nchi hiyo, kama zilivyo nchi nyingi za Ulaya kwa sasa, sio salama tena kwa upande wa ugaidi wa kiislamu!

Source: BBC na Al Jazeera.

Hilo ni fundisho kwa Tanzania ambayo imekuwa inanyemelewa na mataifa ya magharibi kwa udi na uvumba na sasa wamepata makuwadi (Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi) wao wa kuwatumia.
 
waislamu wenye msimamo mkali hawahifadhiki, ni hatari sana
kuwakumbatia, ni heri wajue tu kuwa wewe hupendi shughuri zao,
ni janga kubwa kujihusisha nao kwa namna yoyote ile, ni kweli hata
wao kwa wao ni maadui
 
Mimi nazani Muislam mcha Mungu atawakataa hawa jamaa kwa kila hali....Sasa ni wajibu wa Waislam kujiuliza je, wanaunga mkono magaidi hawa au lah! Mimi ninavyojua Muislam mcha Mungu ni mtu mwema na mwenye kupenda watu kwa hiyo kwangu nawaona hawa jamaa kama MAMLUKI WA DINI!!!!!!!!!
 
Kuchinjana ndio itikadi yao.Leo Pakistan karibu watu 40 wamechinjwa na suicide bomber!
Hawa suicide bombers wanaamini kuwa watapata malaika na virgin huko mbinguni
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom