Nchi inavyoongozwa kimjini mjini.

Mwangaza

Senior Member
Feb 26, 2008
198
64
Wadau,

Wahenga hawakukosea waliposema utatambua matendo na moyo wa mtu kwa kauli zake, na mtoto wa nyoka ni nyoka. Kwa nasaha hizo za wahenga tunangalie kauli mbili tu za Ridhiwani Kikwete.
Kauli ya kwanza; “..Ndivyo nilivyolelewa na wazazi kuhusu namna ya kuishi".
Kauli ya pili ; "..mjini tunaishi kimjini si kila kitu unachomuona nacho mtu ni chake.."

Nijuavyo mimi;

Kuishi kimjini mjini ni kuishi kwa ujanja ujanja (yawezekana kwa shughuli halali au halamu), kuishi kwa kupeana kazi/dili/michongo kwa kujuana bila kujali ufanisi (hii ni mbaya inapoingizwa kwenye sekta za serikali/chama), na mambo yanayoenda na hayo.

Tafsiri ya nukuu;

Kama Baba kamlea mwana kuishi kimjini mjini hivi, Bila shaka Baba naye anaishi kimjini mjini vivyo hivyo.(maana kama mtoto wa nyoka ni nyoka,hata mzazi wa nyoka ni nyoka)

Rais anapoisha kimjini mjini;

1. Nchi inaongozwa kimjini mjini,
2. Uteuzi wa mawaziri,wakurugenzi,maRC,majaji,MaDC,wabunge na viongozi engine nao hufanywa kimjini mjini bila kuangalia sifa.
3. Mikataba ya kinyonyaji isiyojali maslahi ya Taifa inafanywa kimjini mjini
4. Mambo muhimu kwa Taifa mfano ishu ya katiba mpya yanafanywa kimjini mjini bila kujali mahitaji ya wananchi. Ushahidi ni Huu muswada wa katiba ulivyoandaliwa kimjini mjini ukizuisha masuala muhimi yasijadiliwe.

5. n.k n.k..(wadau mnaweza kuongezea 5,6,7...).

BINAFSI NAWEZA KUSEMA AHSANTE RIZ1 KWA KUTUFANYA TUMJUE ZAIDI JK NA KWA UNDANI NA ANAYOFANYA KIMJINI MJINI.
 
WADAU
Mtu anayeishi kimjini mjini mara zote ni mtu asiyestahiri katika eneo husika. mfano, mbunge aliyeishia darasa la pili na nusu hasitahiri kuwepo bungeni maana hataweza kuusoma mswada wa katiba ulioandikwa kwa lugha ya kiingeleza tena lugha ya kisheria. Rz one kauhakikishia umma unaoongozwa na viongozi wasio na sifa stahiki maana mtoto haimbiwi nyimbo mbaya akiimbiwa tu basi humfunza mabaya therefore ndivyo alivyofunzwa kama alinyonavyo kapata kwanjia yoyote basi hiyo njia ndo kafundishwa?
 
Wengi mnaishi kimjinimjini mishahara na maisha yenu ni tofauti kabisaaa! Nchi hii ya madiri tuu!
 
Katika nchi zenye ustaarabu na ambazo watu wake wanalipa kodi,kuna mambo ambaye mtu yeyote hawezi kuyafanya,kwa mfano kujenga mahekalu au hekalu bila kukopa hela benki za kujengea hilo hekalu,lakini hapa kwetu mtumishi wa umma kwa mfano kwenye wizara,wakala(EWURA,TRA,SUMATRA n.k wafanyakazi wamejenga mahekalu ambayo ukimuuliza hiyo pesa kapata wapi hupati jibu ,kwa mshahara wa milioni 2 sio rahisi kujenga eti hekalu la 500m au hata 100m,hivyo ndio kuishi kimjini mjini
 
Hii JF inayoishia kujadiri watu badara ya issues imenichosha.
 
Huyu kijana bila kujitambua kaleta msamiati wa maudhi sana kwa ikulu na nchi nzima!...
HIVI HAKUNA SEMINA KWA wanafamilia wa Ikulu, maana ile ni taasisi ya aina yake!
 
Back
Top Bottom