Nchi haijengwi na chama cha siasa

Typhoid

JF-Expert Member
Feb 7, 2012
223
66
Hodi wanamagreat thinkers!
Mie ni mgeni kabisa wa hili jukwaa! Sio kwamba Leo ndo mara yangu kuliona ila namaanisha kushare ideas! Nimechoka kuwa msomaji ngoja na mie nijipatie ka-id ili tupeane mawazo!
Rai yangu ni kwamba ktk kuijenga nchi masikini kama Tanzania tusitegemee chama chochote cha siasa bali ni sie wenyewe kujitambua! Kama tutajitambua basi itatakuwa rahisi sana kwetu kupata viongozi bora wa kuijenga nchi yetu bila itikadi!
Mungu ibariki Tz!
 
Kwangu mimi nchi inajengwa na mtu mmoja,ambaye ni kiongozi wa nchi.Yeye akisimamia anacho amini na kukitekeleza kwa asilimia kubwa basi nchi itasonga mbele.Mifano ipo mingi ingawa sio mingine mizuri lakini ile dhana ya kiongozi kuindeleza nchi yake ipo.Mfano hai ni Hitler wa Ujerumani.Yeye dhamira yake ilikuwa kuitawala dunia,hivyo akaelekeza nguvu zake katika jeshi bora la kupigana vita.Mfano wa pili ni George Washington ,yeye aliamini katika umoja wa taifa la Marekani,alijieleza katika hilo na kufanikiwa kuunganisha zaidi ya nchi 50 kuwa moja.Yupo Mao ailyeamini katika Ukomonist wa utajiri amejieleza katika hilo na leo hii China inatisha kiuchumi.Hata hapa kwetu mwalimum alitutoa katika ubepari wa kurithi kwa Waingereza kutuleta kewnye ujamaa.Ni dhamira ya aliye juu, inasababisha ama nchi iendelee au irudi nyuma,muongozo wake ndiyo dira ya nchi.
 
Chama pekee ni uozo coz mfano CCM bila Chadema nchi itakuwaje?????Think twice,pamoja na kuwepo upinzani ila bado jamaa wamedinda kuibia nchi....Chama muhimu na chama chenyewe ni CHADEMA.
 
Hodi wanamagreat thinkers!
Mie ni mgeni kabisa wa hili jukwaa! Sio kwamba Leo ndo mara yangu kuliona ila namaanisha kushare ideas! Nimechoka kuwa msomaji ngoja na mie nijipatie ka-id ili tupeane mawazo!
Rai yangu ni kwamba ktk kuijenga nchi masikini kama Tanzania tusitegemee chama chochote cha siasa bali ni sie wenyewe kujitambua! Kama tutajitambua basi itatakuwa rahisi sana kwetu kupata viongozi bora wa kuijenga nchi yetu bila itikadi!
Mungu ibariki Tz!
Na iwe kweli.
 
Back
Top Bottom