Nchi haiendeshwi na mitandao ya kijamii!!-Salva Rweyemamu

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
8,313
13,277
msemaji wa ikulu,ktk kipindi cha jahazi,amesema nchi iko shwari kabisa,na imani ya wananchi kwa rais wao inazidi kukua kila cku!!tatizo la mfumuko wa bei sio tatizo la serikali ni tatizo la dunia nzima!na wale wanaopiga kelele kila siku juu ya mabdadiliko ya baraza la mawaziri sio kazi yao,na pindi rais atakapoona inafaa kufanya hivyo atafanya hivyo.Na magazeti yaache kutabili mambo kwani hata kwenye makubaliano yaliofikiwa kwenye mgogoro wa madaktari,ni baina ya serikali na ma dr,wala sio na magazeti.Na maisha ya mtanzania yanaboreka kila uchao!!kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa jamani.
 
nilichigundua ni kuwa Kibonde alimuuliza Rweyemamu maswali mazuri na yenye mustabali wa taifa ila huyu rweye akatoa majibu marahisi sana. hili ni janga la kitaifa kama hamjui
 
Ni kweli. Nchi ikianza kuendeshwa kwa kupitia mitandao ya kijamii ni hatari sana.

So Salva was right on point.
 
yaani sikuamini majibu ya huyu anaejiita msemaji wa ikulu,majibu ya ************ mepesi kwenye swali zito kuliko ambavyo sikukutegemea.ama kweli nchi yangu tanzania
 
Nchi iko shwari wakati maisha yanazidi kuw amagumu
Mfumoko wa bei ni tatizo la dunia kwani jamaa amekuwa gavana wa benki kuu anatupa taarifa hizo
Imani kwa rais amefanya research wapi kutupa data kuwa imani kwa rais wa nchi inazidi kupanda
maisha ya mtanzania yanazidi kuboreka kwa kipi kwa kutojua kesho anakula nini ndo maisha yanaboreka
Ahhh majibu mepesi kwa maswali magumu
 
Ni kweli. Nchi ikianza kuendeshwa kwa kupitia mitandao ya kijamii ni hatari sana.

So Salva was right on point.

Mkuu kweli ni hatari sana
Ila ni sehemu ya upashanaji habari pia
Maana kwa wale ambao hawana access na magazeti mitandao ndio kimbilio lao
Ila pia ikitumiwa vibaya ni hatari kubwa sana
 
Ni kweli. Nchi ikianza kuendeshwa kwa kupitia mitandao ya kijamii ni hatari sana.

So Salva was right on point.

Hatuko kwenye utawala wa kifalme tuko kwenye utawala wa kidemocrasia. Wananchi hawana mahala pa kusemea zaidi ya kwenye mitandao na pia habari nyingi zinapatikana kwenye mitandao ya kijamii. Salva aache ujuwa walileta utandawazi wanategemea nini, uwoga umewatawala sasa hivi kwa kuwa watu wamepata mahala pakukutana na kusemea.

CHANGE WE NEED
 
...japo mitandao hii imechangia kuleta mapinduzi sehemu nyingi duniani!
 
Hatuko kwenye utawala wa kifalme tuko kwenye utawala wa kidemocrasia. Wananchi hawana mahala pa kusemea zaidi ya kwenye mitandao na pia habari nyingi zinapatikana kwenye mitandao ya kijamii. Salva aache ujuwa walileta utandawazi wanategemea nini, uwoga umewatawala sasa hivi kwa kuwa watu wamepata mahala pakukutana na kusemea.

CHANGE WE NEED

mkuu kwanza umemsikiliza jinsi alivyokua anajibu!anazidiwa hata na msemaji wa wapigadebe hajielezi kama msemaji wa ikulu ya tanzania.kichwa kimejaa pumba tu
 
Kweli wanatufanya ma mbu mbu mbu. Wanadhani wanaweza kutuendesha kama trekta bovu. Mitandao kama hii yaweza kubadili mwelekeo wa jamii at a click of a mouse. CAREFULL !!!!!!!!!!!
 
nilisikiza kwa makini, salva aliulizwa maswali makini sana ila alijibu kwa jinsi wanavyomdanganya raisi mambo shwari ,ndio hawa washauri wa raisi na watendaji wake wa karibu tunao wbmini. Tumekiwisha.
 
viongozi wengi wasio makini wanaogopa mitandao ya kijamii kwa sasa kwa bongo ni jf pekee washaona mambo mengi yanawekwa humu na hutokea kweli. Na bado n4 mwanzo huo.
 
nikimpa salva sh 5000 aache nyumbani kwake asubuhi watoto watakula cha mchana na jioni?nyanya kisado sasa sh 8000
 
Salva atasemaje wananchi imani kwa Rais wao inazidi kupanda wakati ulinzi wa huyo mkweree ndio unazidi kuimalishwa kwa woga gani kama wananchi wake wanampenda? Wangekuwa wanampenda wasingempopoa na mawe wala kumpa maneno ya kumkashifu mitandaoni!! Rais anaependwa haogopi kuonana na wananchi, lakini huyu mkweree hana hata ratiba ya kuonana na wanachama wake kama ilivyokuwa enzi za Mwinyi ambapo wanachama walikuwa wanaonana nae pale ofisi ndogo ya chama Lumumba au hata Dodoma!!
 
Back
Top Bottom