Nccr ziarani kigoma

Charuka

Member
Oct 20, 2009
56
18
NCCR yataka wananchi Kigoma wapewe mamlaka ya kujiongoza


na Jacob Ruvilo, Kigoma


amka2.gif

MWENYEKITI wa Chama cha NCCR- Mageuzi, James Mbatia, ameitaka serikali kuwapa wananchi wa mkoa wa Kigoma mamlaka ya kujiongoza ili kujiletea maendeleo kwa kuwa viongozi wote wa awamu nne za utawala nchini wameutenga kimaendeleo mkoa huo.
Akizungumza na wananchi wa mkoa wa huo, maeneo tofauti, ikiwemo Mwandiga Nguruka na Kigoma mjini, juzi, Mbatia alisema miongoni mwa mikoa uliyotengwa katika huduma za kimaendeleo tangu kupatikana kwa uhuru mkoa wa Kigoma unaongoza na hatua za makusudi zinapaswa kuchukulia.
Mbatia alisema mkoa huo, una rasilimali nyingi za kiuchumi ambazo kama zikijengewa miundombinu bora inaweza kuleta maendeleo ya kasi kwa wananchi na wakazi wa mkoa huo kama ilivyo mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.
“Mkoa wa Kigoma una ziwa kubwa lenye kina kirefu zaidi duniani; kuna madini, kilimo cha kahawa, migomba, michikichi, pamba na mazao mengi mengine lakini miundombinu duni kama zana za uvuvi, kilimo barabara tangu ukoloni ndio uchawi wa mkoa wa kigoma kushindwa kupiga hatua kimaendeleo huku wananchi wakisingiziwa kila kukicha kuwa ni wavivu,” alisema Mbatia. Mbatia aliwataka wakazi wa mko huo kuungana wote katika upinzani bila kujali vyama kama ni CUF, CHADEMA au TLP kwa lengo la kupata viongozi bora wenye uchungu kuiongoza Kigoma badala ya kuanza kupigana vijembe. Naye Mkurugenzi wa Oganaizesheni wa Kampeni na Uchaguzi wa Chama hicho, Faustin Sungura, alisema wananchi hawana budi kuihoji serikali kuhusu ahadi ya maisha bora kwa kila mwananchi kama ambavyo sera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilivyoeleza wakati wa kampeni za mwaka 2005.
 
Back
Top Bottom