NCCR Mageuzi yamfukuza uanachama Kafulila na wenzake!

vipi kipindi hiki hawakurushiana viti kama ilivyotokea enzi za Mrema na Marando ukumbi wa ......................... nimeusahau!!!
Raskazone Tanga mkuu tulikwepa viti gizani sintosahau hiyo ilikuwa kazi ya Marando, leo Kafulila na Zitto wamechelewa kuwaita polisi maana ndio mbinu waliyokuwa wanatumia CCM kuvuruga mikutano ili vikao vishindwe kufikia maamuzi, walitufanya hivyo hivyo pale Manzese wakati TLP iko pale kwenye gorofa la Ngawaiya tulipoanza mkutano tu tukarushiwa mabomu ya machozi ukumbini.
 
Sasa huyu kafulila, kila chama anachokuwamo ni lazima azue mgogoro. Naye ni pandikizi la magamba nini!
Hapana, the way I see kijana huyu ni mwanaharakati wa mageuzi mwenye kasi na pupa pengine ni shauri ya ujana. Mimi naamini atakuwa mwanasiasa bora kabisa hapo baadae. Sijui kwa nini hakuomba radhi kule CHADEMA alipokosea maana kwa hakika anafit katika timu ya wapiganaji mradi arekebishe nidhamu. Ni Kafulila, Machali na Mkosamali walioigeuza tashwira ya NCCR baada ya kufubaa kwa muda mrefu.
 
Mfalme Suleiman aliomba apewe Hekima. Wabunge Vijana wanatakiwa kuomba Hekima kwa kipindi hiki. Wengi wanakengeuka. Zitto anaingizwaje kwenye hili saga la NCCR nijuavyo Zitto ni Mbunge kupitia CDM sasa hao polisi na simu ya Zitto sielewi.

Kafulila siasa ni muda na mazingira tamaa ya madaraka haiwezi kukupandisha juu haraka, anzisha chama chako uone kama ni rahisi. Wapo watu mashuhuri kutoka kigoma. Vyama vya upinzani vimepitia mambo mengi ila chama cha upinzani kitakachodumu ni CDM pekee.
 

Hata hivyo, wakati kikao kikiendelea likaja kundi lingine la askari polisi ambao walieleza kwamba wamepigiwa simu na Zitto Kabwe kwa ajili ya kuzuia vurugu zilizokuwa zikiendelea katika mkutano huo.

Zitto nae anaingiaje hapa?
 
Mimi ni mwananchi niliyeguswa na Kufukuzwa kwa Kafulila ndani ya NCCR, namjua Kafulila ni
Mwanasiasa kijana shupavu
Anayejua kujenga hoja
Msomi mwenye upeo mkubwa na maono ya kuwatumikia wananchi wake
Mwenye uchungu na nchi yake na maliasili ya taifa
Mzalendo wa kweli

Natambua vilevile udhaifu wake..
Si mvumilivu hasa anapotaka kutimiza malengo yake
Hii inapelekea atofautiane na viongozi wake mara kwa mara

Najua alitenda kosa ndani ya chama chako unachokiongoza
lakini kutenda kosa si kosa bali kurudia ni kosa
Please give him a second chance
Namuombea msamaha ili umpokee tena aendelee chini ya uangalizi wako kuwatetea
wananchi wa Kigoma Kusini walioachwa bila mtetezi bungeni.

Naamini ombi langu litakufikia

Asante.
 
arudi magamba ili awe ant magamba akiwa ndani ya magamba baadae akishawasoma atakuwa mpinzani mzuri
 
Mtu kama huyu hastahili kuwa kiongozi wa jamii. Hawa ndio watu wanaojiona wanaakili kuliko watu wengine na kuwasema ooooooooooowachaga oooooooooookaskazini, sasa mungu anawaumbua mmoja mmoja mpaka tupate wapambanaji wa kweli wa kuinusuru Tanzania yetu. CHADEMA msimpokeee, na akirudi asipewe uongozi wowote.
 
ila dah ndo ayo mambo tu lakini kafulila jembe, namkumbuka alitutetea sana sie wanyonge pale mjengoni, halafu kilo mbili ndo anazikosa hivi hivi, au sijui jina nalo limemsibu ata nashindwa nianzie wapi kumpa tafu kafulila.
 
Mkutano uliamua kuwatoa wajumbe wenye tuhuma mbalimbali kwa ajili ya kuwajili ambao wajumbe kwa kauli moja waliona kwamba ipo haja ya kuwapa adhabu ya kuwavua nafasi mbalimbali za uongozi. Hata hivyo, wakati kikao kikiendelea likaja kundi lingine la askari polisi ambao walieleza kwamba wamepigiwa simu na Zitto Kabwe kwa ajili ya kuzuia vurugu zilizokuwa zikiendelea katika mkutano huo. Kutokana na madai hayo, mkutano huo ulilazimika kumuita tena Kafulila na Hashim Rungwe ambao walitajwa kuwapokea askari hao kueleza msingi wa kuhusisha vyombo vya dola na watu wa nje wa chama hicho katika mkutano wa ndani wa chama hicho.
Hivi Zitto anahusika nini na mkutano wa NCCR? sometimes huwa simwelewi.

Kwa taarifa yako, Zito na Kafulila ni sawa na mchwa au pia wale wadudu wanaobangua mahindi. Ukiwakaribisha nyumbani kwako, hakikisha nguzo zote umepaka dawa. Kama nyumba yako ni ya nyasi, ujue umeliwa kwani watazishambulia na baada ya siku chache, nyumba itaanguka tu.

Kwa sasa Zito amezibitiwa CHADEMA ndiyo maana hajaweza sana kubangua sana chama. Subirini uchaguzi mkuu utakapo karibia mtayaona mambo !! Mark my words !

 
Kama alifukuzwa huko CHADEMA na akaenda kuharibu huko NCCR-MAGEUZI unadhani huyo ni mtu wa kujifunza na kujirekebisha?
Imeandikwa msamehe mtu saba mara sabini kwani Kafulila kaua mtu jamani si makosa tu ya kibinadamu?
 
sidhani kama hakupata nafasi ya kuomba msamaha lakini mpaka amefika hapo inaonyesha jinsi gani hakuwa tayari kuomba msamaha. Ajipange tuu vyama vpo vingi au aanzishe chake awe mkuu kama anavyotaka
 
sidhani kama hakupata nafasi ya kuomba msamaha lakini mpaka amefika hapo inaonyesha jinsi gani hakuwa tayari kuomba msamaha. Ajipange tuu vyama vpo vingi au aanzishe chake awe mkuu kama anavyotaka
Aliomba lakini hakusikilizwa..
Baada ya uamuzi huo kutolewa Kafulila alikwenda kupiga magoti mbele ya Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia huku akibubujikwa machozi na kuomba radhi akisema: "Naomba radhi, nimekosa mnisamehe..."

Baada ya hapo Mbatia alisimama na kumwombea msamaha kwa wajumbe wa kikao hicho, lakini walikataa na kumweleza (Mbatia) kuwa akisamehewa watarudisha kadi zao za uanachama."Hatutaki , Kafulila hatufai anakiharibu chama na akisamehewa sisi tutarudisha kadi zetu za uanachama ili ubaki naye kwenye chama...," walisikia wajumbe
 
kafulila is bright na anaweza kurudi cdm au kwenda xxm na kushinda tena ubunge. The boy is vital kwenye siasa za bongo
 
Back
Top Bottom