NCCR yameiva: Kafulila kuvuliwa uanachama Jumamosi!

najaribu kujikumbusha ile picha kupitia tbc kipindi kile kafulila anawashambulia chadema bungeni eti ,nanukuu eti kama wameshindwa kuungana na sisi eti watawezaje kushiriiana na watz kuuleta maendeleo eti cdm ni wabinafsi wakati anajuwa mkiti wake ni mccm halafu hata kanuni za bunge zinawaruhusu cdm kuwa kambi rasmi ya oppose eee bwana kutenda thambi kubaya
 
Hivi James Mbatia anafanya kazi gani? au biashara gani au anapataje kula yake ya kila siku?

Naomba majibu ya kweli kama hujui shut up!

Kazi yake ni siasa na biashara yake ni siasa!
Anakula kwa sababu ya siasa ndiyo maana
anahaha kulinda biashara yake isiingiliwe...
 
Halafu sijui upinzani unakuwaje tena! Hamad Rashid Mohamed naye kakalia kuti kavu huko CUF. Kamgusa mwenye CUF mwenyewe.
 
kazi kweli kweli, but hakuna mapinduzi bila fitna na hizi ndo fitna zenyewe, mchawi atatolewa tuu wakati ukifika
 
kazi kweli, kiongozi asipingwe hadharani kwani yy ni Mungu mtu, wacha kufundisha watu nidhamu za woga, kama hyo ni kanuni haifai
 
Kama habari hii ni ya kweli, si habari njema kwa mustakabali wa upinzani endelevu unaojiandaa kushika dola 2015. Kafulila naye ni muhimu atafute jinsi ya kuchukuliana na viongozi wake, hata kama wanaonesha aina fulani ya udhaifu kiuongozi - kama kweli upo.

Bwana aweda nasikia kuwa hayo yote ni Bwana sitta ili aweze kugombea kupitia NCCR 2015 na amewapa masharti NCCR kuwa mbatia aondoke kwanza
 
Hivi James Mbatia anafanya kazi gani? au biashara gani au anapataje kula yake ya kila siku? Naomba majibu ya kweli kama hujui shut up!
kazi yake ni Uenyekiti wa NCCR-Mageuzi, ndio maana kakaa pale zaidi ya miaka kumi na moja na hataki kuondoka. analipwa na CCM kwa jitihada za kuudhoofisha upinzani ili CCM iendelee kuwa madarakani. Project yake ya sasa ni kuhakikisha jimbo la Kawe na Kigoma kusini yanarudi CCM kwa kumuondoa Mh. Mdee kwa kesi na Kafulila kwa kumnyang'anya kadi ya uanachama wa NCCR-Mageuzi. Pia inasemekana alimpa Mkosamali wakili aliyefremu kesi yake vibaya, hivyo yaelekea Mkosamali akashindwa kesi ya kupinga ushindi wake mahakamani iliyofunguliwa dhidi yake na aliyekuwa mgombea wa CCM, ndio maana kuna wakati alikuwa akitishia kuwa atahamia CHADEMA. Hivyo hayo ndio madili na kazi za James mwana wa Mbatia, Injinia ambaye hajawahi practice kazi alosomea na dependant na mvivu wa kufanya kazi bali anaishi kwa fitina za siasa.
 
Kama habari hii ni ya kweli, si habari njema kwa mustakabali wa upinzani endelevu unaojiandaa kushika dola 2015. Kafulila naye ni muhimu atafute jinsi ya kuchukuliana na viongozi wake, hata kama wanaonesha aina fulani ya udhaifu kiuongozi - kama kweli upo.
we umeshajifunza kuvumilia ukwapuaji wa ruzuku ndio maana umetulia? au wanakusogezea kidogo? inabidi Kafulila aje kwako ili umpe uzoefu, na chonde usije ukaanza kutufunda namna ya kuvumilia wizi wa CCM, maana kitu cha msingi si kuvumilia bali ni hao wanaotuhumiwa kujirekebisha au kujiondoa na kuwaachia watu siriasi ili wafanye kazi.
 
Madiwani wa Arusha mliwafanyaje CHADEMA? Au umesahau mara hii!

Kilichofanyika kwa madiwani wa CHADEMA Arusha ndio kinachotakiwa kufanyika kwa James Mbatia sio kwa David Kafulila. Kama ilivyokuwa kwa madiwani wa CHADEMA, Mbatia naye anatumiwa na CCM kwa maslahi yao na yake binafsi. Mbatia ndio gamba linalotakiwa kuvuliwa NCCR-Mageuzi.
 
Kafulila kama ni kweli itakuwa ni pigo kwako sababu itaonyesha huwezi kuishi kwa kuvumiliana na wenzako ama huwa unajari maslahi yako kwanza kuliko ya wengine ndani ya chama. Pia ni ishara ya kutokuwa kiongozi mzuri. Anyway ngoja tusubiri hyo jmosi tuujue ukweli.
 
mbatia wacha yamkute amewatumikia ccm kwa muda mrefu ila pia kafulila ni pandikizi tu hawana mpango nccr=mageuzi ilishakuwan nccr-manunuzi wamehongwa na magamba kuhujumu upinzani
 
Hivi James Mbatia anafanya kazi gani? au biashara gani au anapataje kula yake ya kila siku?

Naomba majibu ya kweli kama hujui shut up!

Mbona unakuwa mkali? Au unajihami, hauko tayari kuulizwa swali hilo hilo kuhusu katibu wako siyo.
Anyways, mchungaji hula madhabahuni aisee. Pengine halipwi 7m, lakini kwa vyovyote Mbatia atakuwa anakula kupitia siasa meen!!
 
Itakuwa mara yake ya pili katika uanasiasa wake mchanga. Alishawahi kuvuliwa Gamba na Dr Slaa wakati yuko CDM kwa kula njama za kutaka kupora uenyekiti kwa Mbowe. Jasiri haachi asili.

CDM alivuliwa uofisa habari wa chama na si uanachama wake, kwenda NCCR ulikuwa ushauri aliopewa na mentor wake Zitto. Hivi hili la Mbowe kuporwa uenyekiti huko CDM nako uenyekiti ni utume kama kule CUF?
 
Hivi James Mbatia anafanya kazi gani? au biashara gani au anapataje kula yake ya kila siku?

Naomba majibu ya kweli kama hujui shut up!

Analipwa mshahara na chama ambao ni pegged kwenye Euro. Uki convert kwenye shilingi, ule wa Dr Slaa ni cha mtoto. Nisichojua na kwa hilo na shut up, ni kama ruzuku yao inatosheleza malipo hayo au wana sources zingine.
 
Moto anao bt kumbe cuf wanafki coz muungano waokati yao na ccm c wao ndo waliutaka sasa wanarumbana nin?
 
Kasheria haka ka kumvua mtu uanachama halafu anapoteza kila kitu kanakatisha tamaa kama sio kusikitisha. Tulidhani vyama hivi vipya visingekatumia kasheria haka kumbe hata wao kanaonekana kuwafaa! KATIBA MPYA inatakiwa haraka ili tukafutilie mbali. Wenzao CCM walishindwa kukatumia kwa akina Sitta. Wakabuni mpango wa kumwambia abadili jinsia yake ili aendelee na Uspika. Akashindwa. JUzi wamemnyima nishani.
Hapo kwenye red, mbavu sina. Ngoja nikapoze koo kidogo!

 
Back
Top Bottom