NCCR yaitaka Serikali kuwafutia kesi akina Mbowe

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
CHAMA cha NCCR –Mageuzi kimeiomba Serikali kuwafutia mashitaka viongozi na wafuasi wote wa Chadema waliokamatwa wakati wa maandamano yaliyozimwa kwa risasi, mabomu na virugu juzi mjini Arusha.

Karibu viongozi wote wa juu ndani ya Chadema, wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Willibrod Slaa, walikuwa miongoni mwa waliokamatwa, kuswekwa rumande na hatimaye juzi kufikishwa mahakamani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, Faustine Sungura alisema kuwa, kutokana na madai ya Chadema kuwa ya msingi, NCCR imemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhakikisha ndani ya siku tatu anachukua hatua za kumaliza mgogoro uliosababisha maandamano hayo.

“Ikiwa hatofanya hivyo tumepanga kufikisha hoja binafsi katika kikao cha Bunge kitakachoanza Februari 8, mwaka huu ambapo kwa kupitia muwakilishi wetu tutaiwasilisha hoja hiyo siku tatu baada ya kikao hicho kuanza ya kumtaka awajibishwe kwani matukio hayo yamechafua taswira ya taifa” alisema Sungura.

Katika mkutano na wanahabari, Sungura amedai kuwa, Chadema ilikuwa na sababu za msingi za kulalamikia uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha kwa kile alichodai ukiukwaji wa kanuni ikiwa pamoja na kuruhusu madiwani kutoka nje ya Jiji hilo.

Sungura alitumia nafasi hiyo kulaani matumizi mabaya ya madaraka yaliyofanywa na Jeshi la Polisi yaliyosababisha uvunjifu wa amani na haki za msingi za binadamu na hivyo kuitaka Serikali kuwalipa fidia wananchi wote walioathirika na uzembe huo wa polisi.

“Haiingii akilini na hasa kwa watu makini, polisi kuzuia maandamano kwa hoja hafifu kuwa hakuna askari wa kulinda maandamano, lakini polisi hao hao wakawa na askari wa ziada wakatumia risasi za moto, mabomu na marungu kuzuia maandamano ni vizuri nguvu hii ingetumika kulinda maandamano hayo” alisema Sungura.

Alisema kwa matumizi ya nguvu na mabavu hayajawahi kuleta suluhu katika migogoro ya kisiasa na kulitaka Jeshi la Polisi kuacha mara moja kutumika kulinda uharamia na ujambazi wa kisiasa unaofanywa na baadhi ya viongozi wa CCM.
 
kweli hapo vyama vya siasa tunaona mnaelekea kuwa na msimamo wa pamoja safi sana tuwe pamoja
 
Wanajua na wao ndoa yao na ccm ikivunjika hawana pa kukimbilia mkuu so lazima waje kwa wenye nchi
 
Thats a right move NCCR, vitu vingine viko wazi sana na hawa viongozi wa polisi na wa wizara ya mamno ya ndani wanatakiwa kuwajibika.
 
Wawe wamoja kwenye masuala yote yanayohusu watanzania,si kule bungeni tugeukane mara wao katiba wadai mahakamani........si kuchagua issue.good move lakini,we are impressed!
 
Serikali inajua wazi kuwa hakuna kesi hapo ndiyo maana Nahodha anabembeleza kuwa CHADEMA wakubali kufanya mazungumzo. Shitaka ni unlawful assembly, CHEDEMA wanazo mkononi barua za polisi kuruhusu maandamano sasa hapo unaiomba serikali nini tena? Wacha mahakama iamue.
 
misiba huunganisha watu jamani. hamkusoma kuwa heri kuwa katika nyumba ya matanga kuliko nyumba ya harusi. ndo kama hivyo sasa, posho zikianza kumwagwa dodoma, utaona urafiki na watawala unavyonoga! hata hivyo wanstahili pongezi. hongera zenu NCCR kwa kuweka utaifa mbele katika wakati huu wa majonzi na harakati dhidi ya udhalimu. Mungu awatie nguvu
 
Hahaha wameshtuka haihitaji kujipendekeza hata kufunga ndoa ili kuepuka kichapo kama mke mkubwa wa CCM.Bora mnazinduka kutoka kwenye sindano mliyokuwa mmedungwa mkafute na kesi pale kawe.
 
Back
Top Bottom