NCCR yafungua kesi Mahakama kuu kudai Tume huru ya uchaguzi

Kidudu Mtu

Member
Nov 7, 2009
64
0
Je, ni muhimu kuwa na tume huru ya uchaguzi?
Jadili ukitoa sababu kwa nini unadhani tume ya uchaguzi iliyopo haifai.
 
Je, ni muhimu kuwa na tume huru ya uchaguzi?
Jadili ukitoa sababu kwa nini unadhani tume ya uchaguzi iliyopo haifai.
We kweli kidudu mtu,kitu gani umeuliza hapa?jibu unalo hapo hapo lakini tena unauliza...Twende step by step uone,mosi umeuliza;je ni muhimu kuwa na tume "huru" ya uchuguzi?halafu hapo hapo unataka tujadili kwanini tume "huru" haifai?
Mjadala huu unaweza ukawa mzuri kama ukibadili namna ya kupresent hoja yako.
 
Unataka iwekwe na chama gani?
Mwenyekiti wake huwa anateuliwa na raisi! Je tulishakuwa na raisi zaidi ya wale wanaotoka CCM?

Ndio maana huwa nashangazwa sana,kama watu wanajuwa kuwa tume si huru na ni ya chama cha majambazi,then kwanini wanashiriki uchaguzi na kutegemea matokeo ya haki yatatangazwa?Ama ni ruzuku tu ndo cha muhimu kwa hivyo vyama?haya mambo ya upinzani kwa style hii ni upotevu wa muda na rasilimali za wananchi.System yote ni upuuzi mtupu,ni kama michezo ya kuigiza.
 
Asante Mushi, nisingeweza kusema zaidi ya ulivyosema, it is so sad!

at least hawa NCCR ,sijajua vyama vingine viko wapi, na je ni nguvu ya soda, na je mahakamani wataamua kwa sheria gani!
 
Tume iliyoko tunaiamini vilivyo mnajua siasa si lele mama hii tume inajitahidi sana ila inahitaji marekebisho kidogo kwa viongozi wake wa chini lakini kwasasa tume saffffffffffffiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

CCM Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Kidumu chama chaq mapinduziiiiiiiiiiiii jibuni sasa
 
Hii tume ni huru isingekuwa huru wasingeshiriki uchaguzi kwa miaka 15 sasa!. Unapoingia uwanjani kucheza mpira na timu nyingine maana yake umekubali kuwa refarii yuko huru na matokeo hayakupangwa. Lakini kila mechi ikichezwa unafungwa halafu unaondoka na kinyongo kuwa refarii kawabeba halafu mechi nyingine ikipangwa unakwenda na jezi yako na washangiliaji wako na nyimbo zako za ushindi halafu unabamizwa tena.. wewe tukuiteje?

Hawana haja ya kwenda mahakamani; wanachotakiwa kusema ni kuwa hatushiriki uchaguzi mkuu wowote na wabunge, madiwani n.k wote wanajiuzulu.. na kama CCM inataka nchi iwe ya chama kimoja basi na iwe mtaona wafadhili watakavyokuwa na nguvu na kuilazimisha CCM kubadili sheria.

Lakini ukiwaambia hili la kugoma wanakuwa wabishi utadhani luba!
 
Back
Top Bottom