NCCR yadai CCM wameiba kaulimbiu yao

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
NCCR yadai CCM wameiba kaulimbiu yao

CHAMA cha NCCR Mageuzi kimeitaka CCM kuacha kutumia kaulimbiu ya “Pamoja
Tutashinda” wakati wa kuhamasisha uchangishaji wa fedha za kampeni zao kwa madai
kuwa kaulimbiu hiyo ni mahsusi kwa ajili ya kampeni za NCCR za uchaguzi wa mwaka
2010.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkurugenzi wa Habari na
Uenezi wa NCCR Mageuzi, David Kafulila alisema chama hicho kinaomba CCM isitishe
mara moja kutumia kaulimbiu hiyo na kubuni kaulimbiu yake kwa kuzingatia Katiba na
sera za CCM.

Kafulila alisema kuwa kaulimbiu ya “Pamoja Tutashinda” ilipitishwa na Halmashauri
Kuu ya NCCR katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Msimbazi Centre Desemba 5
mpaka 6 mwaka jana kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2010.

Baada ya kaulimbiu hiyo kupitishwa, ilizinduliwa na Mwenyekiti wa NCCR Taifa James
Mbatia, Desemba 19 mwaka jana kwenye Tarafa ya Nguruka mkoani Kigoma.


“Hii ni kaulimbiu iliyopitishwa kwa kuzingatia misingi na itikadi yetu ya
Demokrasia ya kijamii iliyoainishwa kwenye Katiba yetu. Tunapenda kuutaarifu umma
kuwa chama kiliagiza vifaa vyote kwa ajili ya kampeni za uchaguzi 2010 vichapwe
vikiwa na kaulimbiu hiyo,” alisema Kafulila.

Kwa mujibu wa Kafulila, NCCR Mageuzi ilishaanza kutumia kaulimbiu hiyo tangu
Desemba mwaka jana katika mikutano yake iliyofanyika katika majimbo ya Kigoma
Kusini, Kigoma Mjini, Kigoma Kaskazini, Muhambwe, Kasulu Magharibi, Kasulu
Mashariki na Buyungu na hadi sasa wanaitumia.

Pia kaulimbiu hiyo ilitumika hivi karibuni katika mkutano uliofanyika katika
viwanja vya Tanganyika Peckers, Kawe ambapo waandishi wengi wa habari walishuhudia

ikitumika wakati Mbatia alipotangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kawe katika
uchaguzi wa 2010.

Akizungumza na HabariLeo kwa njia ya simu jana, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba
alisema kaulimbiu ya CCM kwa ajili ya kampeni za uchaguzi 2010 inasema “Ushindi ni
Lazima” na kuwataka NCCR Mageuzi kwenda mahakamani kama wanaona imeibiwa.



Source: Habari Leo
 
Pamoja na kwamba sili sahani moja na CCm, hapa nitawatetea kidogo. Huyu Kafulila vipi? Aliiandikisha kisheria hiyo kauli mbiu? sishangai kutimilwa kwake Chadema, ilikuwa sawa kabisa!
 
Kaulimbiu inayosahaulika haraka inaonyesha mapungufu ya walioibuni-kwamba haikuonyesha mwelekeo mahsusi, hakukuwa malengo yenye manufaa kwa nchi, na kwamba ilibuniwa kuwanufaisha wenyewe tu. Vyama vikianza kuibiana kaulimbiu maana yake haviongozwi kwa maslahi ya nchi bali kwa nia yao ya kushika madaraka tu potelea mbali kama taifa litayumba. Hayo ndiyo tunashuhudia sasa na zilizokuwa kaulimbiu za CCM. Hata wenyewe wamezisahau!
 
Hivi kuna hati miliki katika kauli mbiu?? NCCR jipange kwa hoja....CCM mbona ina matatizo mengi mkiyatumia mwaweza watowa madarakani?? Tatizo vyama vyetu viko bize na mambo yasiyo ya msingi na ndo maana CCM inaduma!!
 
Pamoja na kwamba sili sahani moja na CCm, hapa nitawatetea kidogo. Huyu Kafulila vipi? Aliiandikisha kisheria hiyo kauli mbiu? sishangai kutimilwa kwake Chadema, ilikuwa sawa kabisa!

Kwani hawa NCCR wameshachapisha ilani ya uchaguzi? Kama imo katika ilani yao ya uchaguzi wana haki ya kudai lakini wana kesi ya kujibu kwa kuanza kampeni kabla ya muda wake
 
Kwani hawa NCCR wameshachapisha ilani ya uchaguzi? Kama imo katika ilani yao ya uchaguzi wana haki ya kudai lakini wana kesi ya kujibu kwa kuanza kampeni kabla ya muda wake

Wanayo haki kwa sheria ipi? Acheni mambo ya kipuuzi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom