NCCR wamwonya JK mchakato wa Katiba; Mbatia asema NCCR walikuwa wa kwanza na hawajaitwa

kweli mbatia left hand, analalamika nn? Kwan CDM waliitwa au waliomba kukutana rais ingekuwa na wao wameomba then wakanymwa hyo nafac hapo sasa wangelalamika.
 
Kwanza Mbatia ajua hao wabunge alio nao wala si kwa ushujaa wa uwenyekiti wake..anaua Chama huyo..Yeye si Mwenyekiti wa Chama? ana nafasi atume barua kuomba kuonana na President au mwenyekiti wa CCM apeleke hoja yake.Angekuwa mpinzani wa kweli asingepinga ushindi wa Princes wetu Halima Mdee.Anatumia Masaburi kuandaa hoja huyu.....Piga Chainiiiiii RCCN piga chiniiiii.....
 
Na mie bora nicheke heheeee kwani sasa hivi hawezi kwenda mbona Nape alipendekeza wapinzani wote wakamuone mkuu?

Milango haijafungwa, si vizuri kulalama, aombe kikao au akumbushie labda atapewa nafasi ya kuwasilisha hoja zake. Sasa sijui kutakuwa na makubaliano mapya zaidi ya yale ya jana ?
 
Milango haijafungwa, si vizuri kulalama, aombe kikao au akumbushie labda atapewa nafasi ya kuwasilisha hoja zake. Sasa sijui kutakuwa na makubaliano mapya zaidi ya yale ya jana ?
Hivi CC ya NCCR ilikaa lini ikatoa tamko la kutoridhia rasimu ya mapendekezo ya katiba yaliyopitishwa kwa vishindo na wabunge wa ccm na wake zao cuf?
au ndio ile stahili kila mtu anabwabwaja kivyakevyake? halijulikani tamko la chama ni lipi?
 
Mashambulizi mengine mnayofanya si haki hata kidogo, Mbatia hajasema kwamba anataka kuonana na Rais, bali alikuwa akiitaarifu ikulu na watanzania msimamo wa chama, maana ikulu ina mpango wa kuandaa ratiba ya kuwaalika inaowaita wadau wengine. Alisema wazi, NCCR hakina imani na CCM wala serikali yake na hivyo hakiko tayari kuzungumza nao. Kumbukeni pia kwamba yanayoandikwa kwenye magazeti huwa hayaoneshi mhusika alisema jambo fulani baada ya kuulizwa nini na waandishi wa habari. Matharani, Mbatia alipoulizwa kama suala la katiba mpya kweli ni hoja ya NCCR, ndipo alipoeleza kwamba tokea kuanzishwa kwa chama hiyo ndio imekuwa ajenda kuu ya NCCR-Mageuzi. Someni ilani za uchaguzi muone. Mfano Ilani ya NCCR ya 2010, inataja sababu 18, kwa nini tuwe na katiba mpya.
Msipotoshe mambo, kauli ya Kafulila na kauli ya Mbatia hazikupishana.
Wana JF tunapoendelea kutawaliwa zaidi na ushabiki wa vyama tunaharibu hata radha ya jukwaa hili.
 
Hivi CC ya NCCR ilikaa lini ikatoa tamko la kutoridhia rasimu ya mapendekezo ya katiba yaliyopitishwa kwa vishindo na wabunge wa ccm na wake zao cuf?
au ndio ile stahili kila mtu anabwabwaja kivyakevyake? halijulikani tamko la chama ni lipi?

Sikiliza mkuu, awali ya yote NCCR-Mageuzi hatuna kitu kinaitwa CC. Vyombo vya chama ni Sekretarieti ya Halmashauri Kuu, Halmashauri Kuu yenyewe, na Mkutano Mkuu. Sekretarieti hufanya vikao vyake takribani kila siku ya kazi kwa niaba ya halmashauri kuu. Matamko ya vyama hutokana na mashauriano ya chombo hiki na uongozi wa juu wa chama. Nikufahamishe pia kwamba kikatiba mwenyekiti ndie msemaji mkuu wa chama, na mara zote anapozungumza na waandishi wa habari katika huambatana na wajumbe wa sekretarieti na baadhi ya wajumbe wa halmashauri kuu.
 
Nlisema jana Mh. Rais hakuwa na sababu zozote za msingi za kukutana na Chademu..sasa a can of worms imeshafunguliwa..kila mtu atakuja na ku-demand na yeye asikizwe na Mh. Rais. Nafikiri suala la katiba liachwe kama alivyopendekeza rais, watu wapeleke maoni yao kwa tume na bunge la katiba litaja yachambua..si rahisi kumridhisha kila mtu. Ni lazma tukuliane ktkk mambo ya msingi, lakini si lazma tukubaliane ktk YOTE. Wao Chademu / NCCR/CUF kaa wanaona wao ndo wanawakilisha maoni ya walio wengi basi wasubiri kushinda 2015 halafu waweke wao hiyo katiba wanayotaka wao. Wasitupotezee muda na nishati.

Yaonyesha una matatizo ya kusoma alama za nyakati...! Nenda kaombewe ukiamini utapona!
 
wingi wa mashabiki wa chama fulani humu unaleta shida, jadilini hoja alizotoa, mnashupalia tu mtu ati kwa sababu hayumo kwenye chama chenu

Kuna kipi cha kujadili hapo?Mbatia mwenyewe ni CCM sasa unataka watu wajadili unafiki wa mpumbavu kama huyo?
 
Nlisema jana Mh. Rais hakuwa na sababu zozote za msingi za kukutana na Chademu..sasa a can of worms imeshafunguliwa..kila mtu atakuja na ku-demand na yeye asikizwe na Mh. Rais. Nafikiri suala la katiba liachwe kama alivyopendekeza rais, watu wapeleke maoni yao kwa tume na bunge la katiba litaja yachambua..si rahisi kumridhisha kila mtu. Ni lazma tukuliane ktkk mambo ya msingi, lakini si lazma tukubaliane ktk YOTE. Wao Chademu / NCCR/CUF kaa wanaona wao ndo wanawakilisha maoni ya walio wengi basi wasubiri kushinda 2015 halafu waweke wao hiyo katiba wanayotaka wao. Wasitupotezee muda na nishati.

Wewe nae ni janga la kitaifa inaonekana umeshachakachuliwa masaburi.
 
Nafikiri NCCR na Mbatia watakuwa wanakosea sana kuleta Politics kwenye mchakato wa Katiba. Rais Kikwete hajafunga milango baada ya kuongea na CDM, Kinachotakiwa ni wao kuzihuisha hizo hoja walizozituma kwa rais April na kuomba kupangiwa muda wa kukutana na Rais kama wenzao. Haya si mashindano ya nani kaanza na nani kamaliza bali ni kuweka masilahi ya Taifa mbele.

Hakuna haja ya kuanza kuleta malumbano yasiyo na tija kwa watanzania. Watanzania wanataka Katiba mpya iliyo bora, unapoanza kuleta siasa za tulifanya hivi tukafanya vile kwa kulialia siyo tu unaporomosha umuhimu wako katika mchakato bali pia unaongeza u - irrelevance wako. Ulipopeleka hayo mapendekezo ulifanya nini baada ya hapo?. CHADEMA wao wameona kuwa 'KUAGIZA KUFYEKEZA' wameamua kutangaza nia yao ya kuenda kuonana na rais bila ya kusema in advance nini kinawapeleka. Agenda ikawekwa mezani wote wakiwa pamoja. Katika mazingira kama hayo mtu hawezi kuweka document yako kwenye kablasha, maana mbali na maandishi umefanya na oral presentation.

Huyu Mbatia anayumbisha NCCR sasa, Juzi alitoa kauli kuwa hatashirikiana na serikali ya CCM katika mchakato wa katiba kwani hawana nia, leo anakuja na kauli ya kusema amepuuzwa kwani yeye ndiyo wa kwanza kupeleka documents na hivyo alikuwa anasubiri kuitwa. Hivi kwa mtu mwenye busara kwenye hii ni kauli ya kuitia press conference?. Jiandaeni ombani nafasi mtapewa, kama wenzenu. Ningekuwa mimi ndiyo Mbatia ningeunanisha nguvu na CDM maana 'HAMNA HAMNA NDIMO MLIMWAMO'. CDM ina support ya Umma unapopingana nayo unajiongezea distance na umma.
 
kweli mbatia left hand, analalamika nn? Kwan CDM waliitwa au waliomba kukutana rais ingekuwa na wao wameomba then wakanymwa hyo nafac hapo sasa wangelalamika.

Mkuu nakuunga mkono kabisa na ninakubaliana na maoni yako, ila hata mimi huwa natumia mkono wa kushoto (left handed) lakini sina akili kama za mbatia hata kidogo. Hiyo utakuwa umepitiwa kidogo Mkuu! Otherwise, tuko pamoja!
 
Huyu Mbatia anayumbisha NCCR sasa, Juzi alitoa kauli kuwa hatashirikiana na serikali ya CCM katika mchakato wa katiba kwani hawana nia, leo anakuja na kauli ya kusema amepuuzwa kwani yeye ndiyo wa kwanza kupeleka documents na hivyo alikuwa anasubiri kuitwa. Hivi kwa mtu mwenye busara kwenye hii ni kauli ya kuitia press conference?. Jiandaeni ombani nafasi mtapewa, kama wenzenu. Ningekuwa mimi ndiyo Mbatia ningeunanisha nguvu na CDM maana 'HAMNA HAMNA NDIMO MLIMWAMO'. CDM ina support ya Umma unapopingana nayo unajiongezea distance na umma.

Mkuu, Hiyo unayoita juzi ndio siku hiyo hiyo habari unayoiona katika thread hii ilipatikana toka kwa mhusika. Mwandishi wa kilichobandikwa hapa hajaweka huo msisitizo ya kwamba NCCR hakina imani na CCM na kwa hiyo haitashiriki nayo mazungumzo. By the way, mswada ushakuwa sheria kwa mujibu wa taarifa za leo toka Ikulu. Labda tutafakari hilo badala ya kuendeleza matusi humu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom