NCCR waanza kuteremsha bendera kupinga kutimuliwa kwa Kafulila na wenzake

:lol:Kunaanza kupambazuka, tukifunguka macho namna hii democrasia ya kweli itakua ktk nchi hii. Kama viongozi wanavifanya vyama ni mali yao, kwa utaratibu huu wataelewa kuwa ni mali ya WANACHAMA. Na wanachama wanaoona wanapelekwa kusiko wataamua kutafuta vyama vitakavyowapeleka njia ya kweli hadi kieleweke :lol:.
 
KATIBU Mwenezi wa NCCR-Mageuzi Mkoa wa Arushana viongozi wengine wanane wa ngazi mbalimbali wa chama hicho mkoani hapa wamejiengua na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupinga kile walichodai uongozi wa kiimla na kuvuliwa uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David kafulila.Uamuzi huo ulitangazwa jana mjini Arusha na Katibu Mwenezi wa Chama cha NCCR-Mageuzi mkoani humo, James Ndarvoi,alipozungumza na waandishi wa habari na kushutumu uongozi wa taifa wa chama hicho kwa kuzitelekeza ofisi zake za mikoa, wilaya na majimbo bila kuzipa misaada yenye lengo la kuimarisha uhai wa chama.

Ndarvoi aliyegombea udiwani katika uchaguzi mkuu uliopita katika Kata ya Daraja II kupitia tiketi ya NCCR-Mageuzi alisema hoja ya ruzuku inayotolewa na serikali kupitia msajili wa vyama vya siasa nchini kupelekwa ofisi za mikoa, wilaya na majimbo iliyokuwa ikitetewa na Kafulila na wenzake ilikuwa ya msingi kwa masilahi na uhai wa chama, lakini ilitumika kama silaha ya kumuangamiza yeye na wenzake.“Hata kama ruzuku inayotolewa ni kidogo, ni lazima tugawane hako kasungura badala ya wajanja wachache wa makao makuu kutumia fungu lote kwa kulipana posho.

Fedha hizo ziende mikoani na wilayani kwa uchache wake ili zitumike kujenga chama kuanzia ngazi ya chini,” alisema Ndarvoi. Pamoja na katibu mwenezi huyo, viongoziwengine waliojivua unachama na kuhamia CHADEMA ni Katibu wa Kitengo cha Wanawake Wilaya ya Arusha, HelenKileo, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Wilaya ya Arusha, Mzee Haji Ramadhani, Mweka Hazina wa Jimbo la Monduli,Happy Ayub na mjumbe wa Kamati ya Ulinzi Wilaya ya Arusha, Gasper Kaaya.Ndarvoi aliwataja viongozi wengine waliojitoa NCCR-Mageuzi kuwa ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji Jimbo la Arusha, Stephen Daniel, Katibu wa Kata ya Daraja II, Peter Samuel,Mweka Hazina wa Jimbo la Lolingido Mary Mollel na mjumbe wa kamati ya utendaji kata ya Daraja II Joseph Tarangei huku akidai zaidi ya wanachama 3,000 watawafuata nyuma.

Alisema tayari yeye na viongozi wenzake wameandika barua ya kuomba kujiunga rasmi CHADEMA na kuiwasilisha kwa katibu wa chama hicho Kata ya Daraja II, Solomon Kitashu Desemba 29, mwaka huu na hivi sasa wanasubiri kujibiwa na kupangiwa taratibu za mapokezi na kukabidhiwakadi za uanachama ili waanze harakati za ukombozi kupitia chama hicho kilichojipambanua kama mtetezi wa haki za wanyonge. Akizungumza kwa njia ya simu jana, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro,alisema chama chake kinawakaribisha viongozi na wanachama hao kujiunga na chama hicho lakini akasisitiza taratibu, kanuni na katiba pamoja na maelekezo ya viongozi wa maeneo husika kufuatwa.Hata hivyo, Nanyaro alionya kuwa CHADEMA kama taasisi haiko tayari kuwa kokoro ya kuzoa kila kitu bali kinakaribisha na kiko tayari kupokea wanachama wapya wenye mapenzi mema taifa na walio tayari kutetea haki, usawa kwa wote bilakujali vitisho vya dola.

“Kama chama tuko tayari kumpokea yeyote anayetaka kujiunga ilimradi anakidhi vigezo, kanuni na katiba ya chama. Pia lazima wawe tayari kupokea, kutekeleza na kuzingatia maelekezo na maagizo yote yanayotolewa na vikao halali vya chama kwani kinyume chake hatutasita kama tulivyofanya kwa madiwani wetu watano waliokaidi maagizo ya kamati kuu kuhusu
muafaka wa umeya Arusha,” alisema Nanyaro. Wakati hayo yakitokea, tayari Kafulila amefungua shauri Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupinga kuvuliwa uanachama na kufanikiwa kupata amri ya muda wa kuzuia chama chake kuendelea na mchakato
wowote wa kumtimuahadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

NIMEIHARIRI ILI WATU WAWEZE KUISOMA. NEXT TIME BE CAREFULL.

 
wanasiasa wananchekesha sana!hivi juzi tulisikia diwani kata ya daraja 2 amefariki ghafla,leo tunasiki viongozi nccr wanahamia chadema-daraja 2!!!patamu sana hapa.
 
kafulila Kazi anayo ifahamu vizuri ni uzushi wa kwenye magazeti, kwani mimi binafsi niliamini kuwa alikuwa na nguvu ndani ya halmashauri kuu ya NCCR kama alivyo kuwa akijitapa kwenye magazeti kumbe ilikuwa ni uzushi akaishia kufukuzwa.


Leo ana endelea kuudanganya uma kuwa VIGOGO wa hama chama, Hao vigogo ni wapi? Nini maana ya Vigogo? yan leo hata katibu wa tawi amekuwa kigogo? wana habari acheni kujiaibisha kwa kununuliwa na Kafulila Binafi gazeti la Mtanzania naliheshimu

Du Kafulila ni balaaa balaaaaaaaaaaaaaaaaa na zito wake siku za za kisiasa na utepeli wao unaesabika
 
KATIBU Mwenezi wa NCCR-Mageuzi Mkoa wa Arushana viongozi wengine wanane wa ngazi mbalimbali wa chama hicho mkoani hapa wamejiengua na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupinga kile walichodai uongozi wa kiimla na kuvuliwa uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David kafulila.Uamuzi huo ulitangazwa jana mjini Arusha na Katibu Mwenezi wa Chama cha NCCR-Mageuzi mkoani humo, James Ndarvoi,alipozungumza na waandishi wa habari na kushutumu uongozi wa taifa wa chama hicho kwa kuzitelekeza ofisi zake za mikoa, wilaya na majimbo bila kuzipa misaada yenye lengo la kuimarisha uhai wa chama.

Ndarvoi aliyegombea udiwani katika uchaguzi mkuu uliopita katika Kata ya Daraja II kupitia tiketi ya NCCR-Mageuzi alisema hoja ya ruzuku inayotolewa na serikali kupitia msajili wa vyama vya siasa nchini kupelekwa ofisi za mikoa, wilaya na majimbo iliyokuwa ikitetewa na Kafulila na wenzake ilikuwa ya msingi kwa masilahi na uhai wa chama, lakini ilitumika kama silaha ya kumuangamiza yeye na wenzake.“Hata kama ruzuku inayotolewa ni kidogo, ni lazima tugawane hako kasungura badala ya wajanja wachache wa makao makuu kutumia fungu lote kwa kulipana posho. Fedha hizo ziende mikoani na wilayani kwa uchache wake ili zitumike kujenga chama kuanzia ngazi ya chini,” alisema Ndarvoi.

Pamoja na katibu mwenezi huyo, viongoziwengine waliojivua unachama na kuhamia CHADEMA ni Katibu wa Kitengo cha Wanawake Wilaya ya Arusha, HelenKileo, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Wilaya ya Arusha, Mzee Haji Ramadhani, Mweka Hazina wa Jimbo la Monduli,Happy Ayub na mjumbe wa Kamati ya Ulinzi Wilaya ya Arusha, Gasper Kaaya.Ndarvoi aliwataja viongozi wengine waliojitoa NCCR-Mageuzi kuwa ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji Jimbo la Arusha, Stephen Daniel, Katibu wa Kata ya Daraja II, Peter Samuel,Mweka Hazina wa Jimbo la Lolingido Mary Mollel na mjumbe wa kamati ya utendaji kata ya Daraja II Joseph Tarangei huku akidai zaidi ya wanachama 3,000 watawafuata nyuma.

Alisema tayari yeye na viongozi wenzake wameandika barua ya kuomba kujiunga rasmi CHADEMA na kuiwasilisha kwa katibu wa chama hicho Kata ya Daraja II, Solomon Kitashu Desemba 29, mwaka huu na hivi sasa wanasubiri kujibiwa na kupangiwa taratibu za mapokezi na kukabidhiwa kadi za uanachama ili waanze harakati za ukombozi kupitia chama hicho kilichojipambanua kama mtetezi wa haki za wanyonge.

Akizungumza kwa njia ya simu jana, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro,alisema chama chake kinawakaribisha viongozi na wanachama hao kujiunga na chama hicho lakini akasisitiza taratibu, kanuni na katiba pamoja na maelekezo ya viongozi wa maeneo husika kufuatwa.Hata hivyo, Nanyaro alionya kuwa CHADEMA kama taasisi haiko tayari kuwa kokoro ya kuzoa kila kitu bali kinakaribisha na kiko tayari kupokea wanachama wapya wenye mapenzi mema kwa taifa na walio tayari kutetea haki, usawa kwa wote bila kujali vitisho vya dola.

“Kama chama tuko tayari kumpokea yeyote anayetaka kujiunga ilimradi anakidhi vigezo, kanuni na katiba ya chama. Pia lazima wawe tayari kupokea, kutekeleza na kuzingatia maelekezo na maagizo yote yanayotolewa na vikao halali vya chama kwani kinyume chake hatutasita kama tulivyofanya kwa madiwani wetu watano waliokaidi maagizo ya kamati kuu kuhusu muafaka wa umeya Arusha,” alisema Nanyaro.

Wakati hayo yakitokea, tayari Kafulila amefungua shauri Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupinga kuvuliwa uanachama na kufanikiwa kupata amri ya muda wa kuzuia chama chake kuendelea na mchakato wowote wa kumtimua hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

NIMEIHARIRI ILI WATU WAWEZE KUISOMA. NEXT TIME BE CAREFULL.

 
Hizo ni ndoto za saa 6 mchana. mshara wa dhambi ni mauti tuu. NCCR wana onyesha ukomavu na umakini. wanapaswa kupongezwa.
hii ni ishara kuwa wakipewa dhamana hawatamtaza mtu kwa rangi, udungu unao tafuna taifa hili, uchama, wala ukabila. Kafulila nikweli alionyesha uwezo wakujenga hoja bungeni, lakini hiyo isiwe tiketi yake ya kudharau chama chake kukiita ccm na viongozi wake,mbona anaililia ccm/ tuu ache unafiki
 
Wasiwasi wangu ni huu,je hao wanaotaka kuhamia CDM sio mamluki?maana CCM kwa kupandikiza mamluki ni no. 1,anyway let us see what we shall see.
 
Nizamu ya NCCR, CDM ilipo mfukuza walidhania alionewa na Dr. slaa. CDM atumtaki hata kwa bure wa ende TLP na Kabwe.
 
Naomba Mnisaidie, Hivi nikitugani cha msingi kinacho mshawishi mtu kuwa ndani ya chama fulani? NI mtu au Itikadi? hao wanao tapatapa heti kafulila kafukuzwa na wao wanahama chama kwa hiyo huku CDM tukimtimua Zitto wataenda CUF?

Niujinga Mkubwa sana tutawaombea pamoja na wanao waunga mkono kama wapo..........................
 
mbatia na ruhuza wake wameshaiua nccr sasa masubiri kameruni akawahudumie
 
Ni kweli mfumo uliopo haukidhi matakwa ya kidemokrasia ya sas lakini kwa kuwa ndiyo utaratibu uliopo ni lazima utumike na kueshimia hadi hapo utakapobadilishwa, hivyo basi kafulila yupo kitanzini ameshanyooshwa hata TLS akina mpangala wakienda mahakamni, mwisho wa siku sheria ndiyo itakuwa mwarobaini wa hili tatizo la leo. Mimi ningetamani TLS waande hoja binafsi wamkabishi mbunge yeyeote aipeleke bungeni haraka sana ili sheria iekebishwe faster, sasa wanaposema wanaenda mahakamani kwani mahakama ndiyo inayotunga sheria, hawa wanajua fika kuwa sheria za sasa zinadai iwapo mbunge yeyeto atapoteza uanachama atakuwa amepoteza na ubunge wake pia, sasa wanaenda mahakamni ili kumpatia rushwa jaji au hakimu apindishe sheri za sasa?huu si ni ufisadi mwingine, mimi nakubaliana na wote waliosema kuwa sheria za sasa zina matatizo na TLS wanajua kuwa njia wanayotaka kuifuata siyo sahihi, wache nao kutudanganya
 
Haya sasa!
CHADEMA kiwe makini sana na wanachama wanao hamia coz wasipokuwa makini wanaweza kujikuta jalala la kuzoa kila uchafu!
LONG LIVE CHADEMA,LONG LIVE TANZANIA!
 
Back
Top Bottom