Mkuu Mtanzania,
Pamoja na factors nyingine, uongozi wa CCM mkoa wa Kigoma una matatizo. Kwenye baadhi ya majimbo kulikuwa na madai kwamba fedha nyingi zilitumika kwenye kura za maoni na hivyo kuna wagombea ambao hawana sifa walishinda. Nadhani kuna mgombea mmoja aliandikwa sana magazetini kwamba ana kashfa za ujambazi, mambo ya albino na ufisadi pia. Lakini mgombea huyo alikuwa kipenzi cha Mwenyekiti wa Mkoa. Kwenye jimbo hilo wananchi walionyesha hasira za wazi kwa kumpa mpinzani 97% ya kura, kitu ambacho ni nadra sana kwa mgombea wa CCM .... watanzania si mabwege tena.
Kama unakumbuka Katibu Mkuu wa mkoa alipewa barua ya uhamisho saa sita usiku, siku ambayo JK alienda kupiga kampeni mkoani Kigoma. Mama wa watu alitakiwa akaripoti Makao Makuu Dodoma. Sasa hivi huyo Mama atakuwa anashangilia tu maana alikuwa mstari wa mbele kuwapinga baadhi ya wagombea Ubunge na Udiwani kwenye majimbo ya mkoa na alikuwa na valid reasons ambazo Mwenyekiti wa mkoa hakuziona.
Tatizo la mafisadi wa CCM wanaamini kwamba fedha inaweza kununua kura, which is wrong maana watu wameamka na wana uelewa wa kutosha. Mgombea yeyote akienda kujikita huko vijijini kwa miaka 2 anawasomesha wapiga kura, ukija uchaguzi lazima wampe kura hata kama kuna mtu ataenda kumwaga fedha, khanga, fulana na kofia.
Mkuu Keil,
Lakini mbona hiyo haikutokea sehemu mbalimbali? Kwa mfano najua yule jamaa wa CHADEMA kule Mbeya vijijini ni mzuri sana na ni kiongozi wa CHADEMA wa mkoa na pia muda mwingi kajichimbia kule Mbeya lakini bado hakuweza kushinda. Kuna majimbo mengine pia ambayo kuna vijana ambao walipiga kampeni za nguvu lakini hawakufanikiwa.
Hii ya Kigoma naona kama ni pekee kwa siasa za Tanzania mwaka huu. Huenda kujijenga kwa hao vijana wakiwa ndani ya CHADEMA kumewasaidia maana tayari walikuwa wanajulikana lakini pia kuna hao wengine wawili ambao nao wameshinda.
Kama kuna mtu anajua matokeo ya udiwani kwenye hizo wilaya ingesaidia.
Kigoma Mjini CHADEMA alikuwa anagombea bwana mdogo mmoja ambaye tumesoma naye nchi moja. Nilisikitika kuona alishindwa dakika za mwisho tena kwa kura chache sana zenye utata. Nafikiri angelikuwa na muda wa kutosha wa kujijenga kule kama wenzake huenda angeshinda kwa kura nyingi.