Hivi NCC inatambulika?

Vijisenti

JF-Expert Member
Mar 11, 2011
544
328
Nilitembelea Center moja katika zile zinazotoa elimu ya Computer Nikakuta mfumo tofauti kidogo na mifumo tuliyozoea. Wao wanatoa Diploma kwa mwaka mmoja, Advanced Diploma kwa mwaka mmoja zinaitwa International Diploma & Advanced diploma na ziko chini ya NCC.

Ukimaliza hizo unafanya Bachelor degree ya Business studies au Bachelor ya Computer studies inayotolewa na Greenwich university. Ninachoomba kufahamu hapa ni kama Elimu ile ya NCC inakubalika na serikali yetu.

Vyuo hivyo viko viwili kimoja kinaitwa Learn IT na kingine kinaitwa Institute Of Information Technology Je nikifanya hiyo Degree kweli inakubalika hapa nchini?

Naombeni ufafanuzi wenu tafadhali.
 
Vyeti vya NCC vinakubalika wala usihofu, nimesoma hapo IIT NCC Advanced diploma na ninafanya kazi serikalini, wala usitishwe kama unataka kujiendeleza wewe nenda tu.
 
Nashukuru sana kwa majibu yako mayasa, nitajaribu huko!
 
wanachakachua elimu hao
najua diploma ni miaka miwili
waliosoma mwaka watakuwa weupe sana
 
Nashukuru sana kwa majibu yako mayasa, nitajaribu huko!

Nenda kaulizie NACTE au TCU, utapewa majibu sahihi zaidi. Hii ya kupata kazi serikalini isiwe kigezo cha cheti kukubalika, kuna watu walishapewa kazi kwa vigezo vya vyeti baadae wakaja kupata matatizo.

And more importantly, you are better off without a certificate (whether recognised or otherwise) BUT WITH KNOWLEGDE AND SKILLS. Angalia kama NCC watakupa unachokihitaji. Omba curriculum zao kwenye hicho unachotaka kukisomea na uangalie taaluma za waalimu.
 
jibu lajitosheleza vya kutosha
 
Vyeti vya NCC vinakubalika wala usihofu, nimesoma hapo IIT NCC Advanced diploma na ninafanya kazi serikalini, wala usitishwe kama unataka kujiendeleza wewe nenda tu.
Kwahio mpaka leo hii bado uko kazini na unatumia vyeti yako vya Ncc kazini?
 
Kuhusu NCC Education programs kwa sasa zina utata.Niliwasiliana na NACTE kanda ya Dar es salaam kuhusu hili. Kuna vyuo viwili vanavyotoa hiyo elimu kwa niaba ya NCC na vinatambuliwa na NCC Education. Tatizo linakuja kuwa NACTE haivitambui hivyo vyuo na wakasema kama hawatambui chuo kile cheti kinachotokana nahicho chuo nacho hawatakitambua.

Wao NACTE wanasema kama chuo hakina program za hapa ndani ambazo zinatambuliwa na NACTE hawawezi kukitambua (kwangu mimi hii ni sababu hafifu sana). Sasa chuo kimoja kina program za nje tu, na cha pili kina program za ndani lakini registration yake ilifutwa kwani kuna vigezo vingine hawaja vitimiza hapo wakitimiza basi mambo yanaweza kuwa shwari.
 
Mimi nilikua nahitaji kusoma program ya ncc kwa sasa hivi una nishauri nini nisome au ni achane na hilo wazo
Ni vigumu kutoa ushauri kwa hili. Labda uwapate Power Computers uwasikilize wamefikia wapi kuhusu hili jambo, kama wako karibu kulitatua unaweza kuisoma hiyo NCC kama hawana hakika huenda ikawa vizuri kusubiri.
 
Mkuu hivi iliweza kupata habari zaidi kuhusu hii ncc
 
Ni vigumu kutoa ushauri kwa hili. Labda uwapate Power Computers uwasikilize wamefikia wapi kuhusu hili jambo, kama wako karibu kulitatua unaweza kuisoma hiyo NCC kama hawana hakika huenda ikawa vizuri kusubiri.
Apia naomba kujua kuhusu course za foundation certificate yani (nta level3)je bado zinatolewa na vyuo husika?Naskia The open university wanazo course hizo,Ni kweli?
 
Naomba msaada kaka
 
Nime ku pm
 
Apia naomba kujua kuhusu course za foundation certificate yani (nta level3)je bado zinatolewa na vyuo husika?Naskia The open university wanazo course hizo,Ni kweli?
Hizi foundation certificate ni tofauti na za NTA levels za NACTE. Hizo mfano wake mzuri ni za NCC Education ambazo humtayarisha kijana kujiunga na vyuo vikuu kadha vya UK.

Kwa Tanzania kuna PCTL [Power Computers Training Institute] na Emerson Education ambao wanaoffer hizo courses.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom