NBC- Kichwele Customer care bure kabisa

TIQO

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
13,787
2,078
Hili tawi la NBC-Kichwele lipo mtaa wa Jamhuri opp. Sleep Inn hotel huduma zao mbovu kabisa.
Nimesimama pale Customer Services zaidi ya dk.50 kupewa jibu la account yangu natakiwa kuleta barua ya serikali za mitaa ili iendelee kufanya kazi. Imenisikitisha kwa kweli wahudumu wapo wengi lakini kila mtu yupo busy na kazi zake sasa wanakaa pale Customer service kuuza sura au kwa ajili ya kuhudumia wateja wenye matatizo? Kila unae muuliza yupo kimyaa au unaambiwa subiri utafikiri tupo wateja kibao wakati tulikuwa wateja 5 tu. Inasikitisha sana badilikeni jamani tembeeni hata kwenye Bank za wenzenu mjifunze kujali wateja.
Mtu unasimama mpaka miguu inauma.
Mtakimbiwa na wateja muanze kulalamika ooh biashara ngumu kumbe wenyewe ndo mnawafukuza.
 
Bank nyingi sasa hivi zisipo badilika watu wanahamia sana kwenye M.Pesa na Tigo pesa
 
Viongozi wa hizi Benki fungeuni macho na maskio. Ndiyo maana benki za nje zinapiga bao sana
 
Hili tawi la NBC-Kichwele lipo mtaa wa Jamhuri opp. Sleep Inn hotel huduma zao mbovu kabisa.
Nimesimama pale Customer Services zaidi ya dk.50 kupewa jibu la account yangu natakiwa kuleta barua ya serikali za mitaa ili iendelee kufanya kazi. Imenisikitisha kwa kweli wahudumu wapo wengi lakini kila mtu yupo busy na kazi zake sasa wanakaa pale Customer service kuuza sura au kwa ajili ya kuhudumia wateja wenye matatizo? Kila unae muuliza yupo kimyaa au unaambiwa subiri utafikiri tupo wateja kibao wakati tulikuwa wateja 5 tu. Inasikitisha sana badilikeni jamani tembeeni hata kwenye Bank za wenzenu mjifunze kujali wateja.
Mtu unasimama mpaka miguu inauma.
Mtakimbiwa na wateja muanze kulalamika ooh biashara ngumu kumbe wenyewe ndo mnawafukuza.

bank zipo kibao hapa jijini kwanini utese nafsi yako?

Similar Discussions

Back
Top Bottom