Nayeya ninapuyaga, ewe moyo nakuaga!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Mwenye kukupa furaha, ewe moyo mchague,
Asiyeleta karaha, ewe moyo mchukue,
Mwenye kukupa staha, ewe moyo uamue,
Moyo ukipenda moyo, moyo hutuliza moyo!

Mwenye kusimama nawe, ewe moyo usikie,
Asiyekutupa kamwe, ewe moyo mshikie,
Akupa nafasi uwe, ewe moyo mfuatie,
Moyo ukipenda moyo, moyo hutuliza moyo!

Yeye akufikiriaye, ewe moyo muwazie,
Mema akutakieaye, ewe moyo mtakie,
Naye akushakiaye, ewe moyo mshakie,
Moyo ukipenda moyo, moyo hutuliza moyo!

Maneno atamkayo, ewe moyo sikiliza,
Ya mtima akupayo, ewe moyo akujaza,
Karimu aso mchoyo, ewe moyo ashangaza,
Moyo ukipenda moyo, moyo hutuliza moyo!

Jitulize uwe tuli, ewe moyo nakuasa,
Furaha iwe ya kweli, ewe moyo usokosa,
Na hili busu la mbali, ewe moyo lakupasa,
Moyo ukipenda moyo, moyo hutuliza moyo!

Basi moyo nakuaga, ewe moyo upendwao,
Ya kwangu kinagaubaga, ewe moyo ujuao,
Nayeya ninapuyaga, ewe moyo utakwao,
Moyo ukipenda moyo, moyo hutuliza moyo!


Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
bravo!
i can see you TWITTERING!and so we are knowing a lots
 
Ni wa kwako huo moyo, ewe kaka usikie
Usiufanyie choyo, kilioche kisikie
Usijeupa unyayo, kilio ukisikie
Kamwe usiache moyo, ukenda usirudie
 
Mengi yananivutia, yenye kutoka moyoni,
Mazuri yalo tulia, msaada maishani,
Moyo umeniridhia, wanipa tele amani,
Kweli nitaweweseka, kuuaga moyo wangu.

Ninashindwa kuuaga, unanikosesha raha,
Hata nitake ubwaga, wanipa tele karaha,
Nikitaka kuusaga, wasiwasi nina haha,
Moyo nilivyoupenda, katu sitaweza aga

Pengine kwenu wajuzi, jambo mnifahamishe,
Hii ngumu iko kazi, tena yanipa kasheshe,
Nimeyaaga mavazi, nikakubali yaishe,
Kwenye kuuaga moyo, mwenzenu nina mashaka.

Ninashikwa na butwaa, niupendavyo mtima,
Kwa jinsi unavyong'aa, kwa maisha na uzima,
Aminia wanifaa, kwa zake bora hekima,
Moyo wangu utulie, Tudumu wote pamoja
 
Ni wa kwako huo moyo, ewe kaka usikie
Usiufanyie choyo, kilioche kisikie
Usijeupa unyayo, kilio ukisikie
Kamwe usiache moyo, ukenda usirudie

Naam!

Moyo nimeusikiza
Sasa wabaki niliza
Nifanye nini kupoza
Ya moyo mambo kuwaza?


Moyo wataka kupenda,
Kupenda asiyependa,
Umebaki kunidunda,
Mimi nimekosa nyonda!

Moyo ninakutafuta
Ni wapi nitakupata,
Niweze nami kuleta
Nami jina nikaita?

Moyo nilosema nimesema,
Nimebaki kutazama
Ninakuaga daima,
Kwa heri ewe mtima!
 

Ninashikwa na butwaa, niupendavyo mtima,
Kwa jinsi unavyong’aa, kwa maisha na uzima,
Aminia wanifaa, kwa zake bora hekima,
Moyo wangu utulie, Tudumu wote pamoja

Swadaktaaaa!!

U heri yako Ndahani, kwa wako huo mtima,
Si shaka ufurahani, mwenzako ninalalama,
Kamwe huko mashakani, moyo ukiutazama,
Tunza sana moyo wako, kuliko vyote utunzavyo!
 
Moyo wataka kupenda,
Kupenda asiyependa,
Umebaki kunidunda,
Mimi nimekosa nyonda!

Moyo ninakutafuta
Ni wapi nitakupata,
Niweze nami kuleta
Nami jina nikaita?

Wangu moyo, una jambo uupete
Wayowayo, liniveme kana Pete
Zangu mbio, nataraji tuwe sote


Si moyoni, jaraha kulla mahali
Na matoni, sipati lepe silali
Masikini, napenda kitu ki ghali


U kizani, moyo umefitamana
Na imani, viumbe huoneana
Swamahani, sinifanyiye khiyana


Hikuwaza, iwapo nala huata
Miujiza, muda ulala huota
Niuguza, maradhi yalonipata

6
Yomi bui, mwenziyo nimedangana
Hunijui, moyoni ninavyoona
Sinwi shai, nisikutaje kwa jina


Dr Hamza yousuf Al Naamani
Doha, Qatar
 
Moyo wataka kupenda,
Kupenda asiyependa,
Umebaki kunidunda,
Mimi nimekosa nyonda!

Moyo ninakutafuta
Ni wapi nitakupata,
Niweze nami kuleta
Nami jina nikaita?

Wangu moyo, una jambo uupete
Wayowayo, liniveme kana Pete
Zangu mbio, nataraji tuwe sote


Si moyoni, jaraha kulla mahali
Na matoni, sipati lepe silali
Masikini, napenda kitu ki ghali


U kizani, moyo umefitamana
Na imani, viumbe huoneana
Swamahani, sinifanyiye khiyana


Hikuwaza, iwapo nala huata
Miujiza, muda ulala huota
Niuguza, maradhi yalonipata

6
Yomi bui, mwenziyo nimedangana
Hunijui, moyoni ninavyoona
Sinwi shai, nisikutaje kwa jina

Dr Hamza yousuf Al Naamani
Doha, Qatar
 
Mkono nakuunga, nami nyota anitesa'
Angani haachi meta ndotoni yu mbali anipita'
Maisha ya leo tikatika mapenzi kote ni vita'

Japo si wote hali hii wanapita'
Wapo ilo kuja tabu mafua kuwapata'
Wakanywa kila dawa ikashndwa nayo kofta'

Ikabaki al hadith na ndoto ilofutika'
Ewe ndugu yangu fanya subira'
Muombe jalali akupe alo imara'

Alo pitiya kitabu na kuijua akhera'
Maishani isije kwasha harara'
 
Wangu moyo, una jambo uupete
Wayowayo, liniveme kana Pete
Zangu mbio, nataraji tuwe sote


Si moyoni, jaraha kulla mahali
Na matoni, sipati lepe silali
Masikini, napenda kitu ki ghali


U kizani, moyo umefitamana
Na imani, viumbe huoneana
Swamahani, sinifanyiye khiyana


Hikuwaza, iwapo nala huata
Miujiza, muda ulala huota
Niuguza, maradhi yalonipata

6
Yomi bui, mwenziyo nimedangana
Hunijui, moyoni ninavyoona
Sinwi shai, nisikutaje kwa jina


Dr Hamza yousuf Al Naamani
Doha, Qatar

Hakika nimepokea simu toka kwa maswahiba wawili wa humu jamvini pamoja na salamu zao walitaka kujua hii ni lugha gani.

Hakika hii ni lugha mwanana ya mwambao ya kiswahili na nimeweka kidigo kigodo na kimakunduchi katika llafudhi ya kiarabu.
 
Back
Top Bottom