Nafikiri inawezekana kabisa wewe ndiyo ukawa na matatizo ktk uwezo wako wa kufikiri. Unataka kukimbia ukweli.
Rosemarie amejaribu kujitathmini akagundua mapungufu, anatafuta msaada ili awe bora. Kuonyesha uwezo wake kufikiri ulivyojuu ametambua kuwa kiini cha mapungufu ni namna anavyofikiri; hakusema ni kwasababu hana kitu fulani. Perfect evaluation. Huwezi kufanya kwa ubora hata kama tukikupa kila kitu lakini uwezo wako wa kufikiri ukiwa chini.
Amefanya kazi na wazungu akaiona tofauti aliyoandika. Ni mkweli. Hujamjibu umemshambulia kwa kushuku uwezo wake wa kufikiri. Si vema.
Kiukweli Rosemarie, unaweza ukafikiri sahihi kwa kiwango kikubwa kupita wanaume wa umri wako. Tena unakufikiri kupita wazungu. Ngoja tusubiri inputs za Invisible. Lakini nitachangia machache: ya kuwa vikwazo vingi vipo ktk namna tunavyolelewa na vingine vipo ndani yetu. Katika malezi tunayolelewa/tuliyolelewa
1. Hayatufundishi kuthubutu bali woga
2. Hayatufundishi kujiamini bali kuwa tegemezi
3. Hayatufundishi kuona kosa ni fursa ya kujifunza bali ndiyo mwisho (kushindwa)
4. Hayatufundishi kuitambua na kuithamini kazi ndogo/mafanikio madogo kuwa ni mtaji wa kutuchochea kufanya makubwa.
5. Hutufundisha kuona kufanya kazi kuwa ni utumwa wakati kazi ni utoshelevu wa maisha ya mwanadamu.
6. Hutufundisha kuona kuwa sisi hatuwezi ila wao/yeye anaweza, na wakati kuwa hata yeye hawezi kamwe.
Orodha ni ndefu.
Wengi wa wazungu tunaowaona kuwa ni bora ni kwasababu ya uzoefu, exposure, uthubutu na kujiamini. Ukifanyakazi hata na mtanzania aliyekuzidi katika eneo lolote ktk hayo mengine mko sawa mara zote utamwona bora .
Nitarudi.
Unaweza ukawa umejaaliwa uwezo wa KUSOMA MANENO, lakini KUELEWA HABARI ikawa kwako ni tatizo:
Umerudia kosa lilelile, unaweza kunifafanulia maana ya MZUNGU? naona umelitumia neno hilo mara kadhaa kwa kujiamini kabisa.
Kwa kifupi wazungu ni watu weupe wenye asili ya bara la Ulaya (matupinkele).
nimelitumia neno hili nikiwa katika kuijibu/kuikanusha hoja yako na katika kumsaidia Rosemarie.
............................
invisible mimi ni 37 na ni mwanamke,uwezo wangu wa kuwaza unaweza kuwa sawa na wa mwanaume mwenye age yangu?halafu kwa nini wazungu uwezo wao uko juu sana,naongea hili kwa sababu nimefanya nao kazi na nimeona mwenyewe jinsi walivyo na uwezo mkubwa!!!!
A good diet improves your health, but also boosts your energy. Create a shopping list of these must-have endurance foods recommended by Dr. Mike Moreno, author of The 17 Day Diet: A Doctors Plan Designed for Rapid Results.kuna uwezekano wa binadamu kuongeza uwezo wake wa kufikiri,pls help
Labda kuongezea tu,
Neno Mzungu limetokana na neno Mzungukaji (Explorer/A person wandering about). Naamini tunafahamu jinsi wazungu akina Vasco da Gama, Ferdinand Magellan, Captain Cook, H. M. Stanley etc walivyokuwa wanachanja mbuga. Dhana hii ya Exploration/Movement ndiyo ilileta neno Mzungu. Hapa nazungumzia "neno" na si "nani."
Bado tuna kazi ya kujibu thread ya Rosemarie.
Yes U can, unatakiwa upate course ya critical thinking and argumentation, hii itakufunza mengi sana na itaongeza uwezo wako wa kufikiri!kuna uwezekano wa binadamu kuongeza uwezo wake wa kufikiri,pls help
Iko hivi, binadamu anauwezo wa kuongeza kufikiri kwa mfano uwezo wa mtu anayesoma vitabu vingi na asiyesoma ni tofauti,jifunze bila kikomo itapanua uwezo wa kufikiri pia jitahidi kutengeneza hoja za kwako mwenyewe wakati wa majadiliano na jifunze kuzitetea.
Kuna dawa ya mchanganyo wa matunda mbalimbali inaitwa brain activator kamuone dr ndodi