Naweza kujenga nyumba kwa TZS Milioni 20?

Mkuu nyumba haijengwi hivyo mara nyingi. Wewe anza na hicho kidogo ulichonacho hatimaye utashangaa unamiliki nyumba yenye thamani ya 100m na wewe hujawahi kuishika au ota ndoto za kuishika. Ukianza speculation hizo nakuhakikishia hutokaa ujenge, mwisho utajutia uzee wako kuwa huwezi miliki hata kibanda.
 
wakuu kwa kiasi icho nikaamua kujenga kule kijijini kwnagu moshi inatosha?asume kiwanja kipo flat level...matofali ya kuchoma....nyumba iwe ni ya kawaida ie. vyumba vitatu vya kawaida,choo cha public ndani,sehemu ya jiko,dining labda na sebule.mnasemaje wataalamu
 
wabongo maliwato anasa..lol

Nyumba Choo Chagua KIMOJA!
Asian Toilet.jpg bite_me_toilet_3001.jpg outhouse_garden.jpg toilet 2.jpg toilet.jpg
 
jamani siwezi kujenga nyumba ya vyumba vinne hapo dar kwa milioni 20????niambieni kama siwezi kabla sijaipoteza hii pesa...

Thanks,

anza kujenga achana na paper work nyumba hujengwa mdo mdogo si kwa siku moja au wiki wewe si fisadi bana.
Fyi- nunua matofari ya foundation, kokoto, mchanga na nondo. Ongea na fundi atakujengea sh.ngapi foundation! Akimaliza foundation elewana naye toka hapo hadi kwenye lintre baada ya hapo lintre then anamalizia.
Mafundi si waaminifu aise.
 
Kwa kuwa kiwanja unacho millioni 20 mbona unahamia kwenye nyumba lakini finishing hutamaliza. Angalia mgawanyo wa gharama ( I assume uko Dar es Salaam na nyumba unayojenga ni ya mtu anayejenga nyumba yake ya kwanza):
  1. Matofali 5,000 @700=TZS3,500,000
  2. Mafundi (kujenga toka msingi mpaka kuezeka)=4,000,000/=
  3. Cement mifuko 150 @15,000=2,250,000/=
  4. Mbao zote TZS4,000,000/=
  5. Bati 60 @ 15,000=900,000/=
  6. Fundi umeme na vifaa vyake=5,000,000/=
  7. Finishing (madirisha na milango)=5,000,000/=
  8. Finishing (plastering + ceiling works)=5,000,000/=

Umesahau gharama ya Msimamizi kama hauna muda HAKIKISHA unamlipa ndugu yako akae asimamie Mafundi wa Bongo Noma
 
Exactly.. Akiondoa gharama za msingi pengine million 20 inaweza labda kutosha, #justsaying

Unajua Abd. watu wengi wanapenda tu kusema nikiwa na shillingi kadhaa naweza fanya hiki? Ukweli ni kama yawezekana,lakini ujenzi ni fani kama fani nyingine kama vile utabibu,uwanasheria na kadhalika!

Nimekua kwenye industry ya kujenga kama mtaalamu na pia kama mjasiliamali kwa gd number of yrs,pamoja na pesa watu huwa wanasahau kitu cha muhimu kabisa na basic nacho tunakiita

Conception stage hii ni stage ambayo muhimu na ambayo anaetaka kujenga anatakiwa atoe idea yake nini anataka na kiwe wapi kulingana na mahitaji yake,bila hata ya kuenda stage nyingine wataalamu tutamshauri na kumwambia pesa inatosha au la!

Jamani is a professional thing!

Tunaamini kila mtu aweza kujenga lakini mtaaalum atajenga kwenye reasonable cost na acceptable quality!

Good day!
 
Unajenga ingawa finishing itakukwaza kidogo,nafikiri kwa kiasi hicho tayari una kiwanja,na ukizidi kuchelewa gharama zinaongezeka kwani hivi sasa vifaa vya ujenzi vinapaa ni kama vile bei ya sukari inavyopaa ,huu mdororo wa Tsh yetu kwa dolari ndio umefanya vifaa vya ujenzi vizidi kupanda bei kila kukichwa
 
Matofali ni kuanzia tsh 800 -tsh 900 hiyo tsh 700 imepitwa na pia weka ya usafiri kubeba na kushusha nafikiri ungeweka TSH 1200 kwa tofali(usafiri,kubeba na kupakia) mambo ya concept kwenye nyumba za uswazi wapi na wapi huku sisi hata ramani hatuchori unamwambia tu nataka chumba ft hizi kushoto vyumba viwili na kulia viwili choo nje ,jiko kwenye mwembe kazi kwishney,hayo mambo ya ramani sijui bwaa la kuogelea ni kwa wenye nazo
 
mkuu hapo namba5, na 7 hivi hizo bati unazoziongelea kwa laki9 ni zipi au madirisha na mirango yepi? Mi binafsi nimeupitia mchakato huo na kwa nyumba ya vyumba vi4 labda twaweza kutofautiana size ya madirisha lakini magrili zilinitoka m3.4 na aluminiums m4.3 total m7.7 na upande wa bati nilitumia zile za versatile bati tuu niliwaachia alaf kiasi cha m5.2 hapo hujazungumzia misumali wala mbao. Nadhani angeweka wazi nyumba ya aina gani

5: Simba dumu geji 30 zinc colgated kwa bei za jumla lakini uwe na jamaa wanaozijua. Madirisha + milango ni mbao tu kiongozi plan la paa liwe futi na ni mgongo wa tembo.
 
anza kujenga achana na paper work nyumba hujengwa mdo mdogo si kwa siku moja au wiki wewe si fisadi bana.
Fyi- nunua matofari ya foundation, kokoto, mchanga na nondo. Ongea na fundi atakujengea sh.ngapi foundation! Akimaliza foundation elewana naye toka hapo hadi kwenye lintre baada ya hapo lintre then anamalizia.
Mafundi si waaminifu aise.

Aisee kidogo kidogo bila kuwahusisha wataalamu unajikuta nyuma ya kujenga 50m unamaliza na 120m na sio imara although utaifurahiya na marangi!
 
wakuu kwa kiasi icho nikaamua kujenga kule kijijini kwnagu moshi inatosha?asume kiwanja kipo flat level...matofali ya kuchoma....nyumba iwe ni ya kawaida ie. vyumba vitatu vya kawaida,choo cha public ndani,sehemu ya jiko,dining labda na sebule.mnasemaje wataalamu

Mwezi uliopita nimemalizia ujenzi wa Nyumba ya Bedroom viwili maeneo ya KIA katikati ya Arusha na Moshi,
Chumba kimoja ni master pamoja na sebule iliyopo katikati ya hizo Bedroom .
Ukiacha madirisha, sakafu, milango na plasta,
Imenikula 3.6Mil mpaka sasa kwa matofali ya kuchoma, mota unaungia udongo wa kichuguu uliochanganywa na cement.
 
thanks wote kwa michango yenu,mliosema haitoshi mbona hamjasema ni shilingi ngapi ndio inatosha?lol anyway thanks nimeona nisijenge sasa hivi...mpaka nikiwa na hela lol
 
thanks wote kwa michango yenu,mliosema haitoshi mbona hamjasema ni shilingi ngapi ndio inatosha?lol anyway thanks nimeona nisijenge sasa hivi...mpaka nikiwa na hela lol

kweli mzaramo ni mzaramo tu.
 
thanks wote kwa michango yenu,mliosema haitoshi mbona hamjasema ni shilingi ngapi ndio inatosha?lol anyway thanks nimeona nisijenge sasa hivi...mpaka nikiwa na hela lol

Dada yangu wasikukatishe tamaa, kwa hiyo pesa anza kujenga hiyo nyumba mpaka itakapoishia ila kama ulivyoshauriwa nenda hatua kwa hatua. Utakapokwama utaendelea taratibu,kama ulipata 20ml huwezi kosa 5ml za kumalizia!
 
Unajua Abd. watu wengi wanapenda tu kusema nikiwa na shillingi kadhaa naweza fanya hiki? Ukweli ni kama yawezekana,lakini ujenzi ni fani kama fani nyingine kama vile utabibu,uwanasheria na kadhalika!

Nimekua kwenye industry ya kujenga kama mtaalamu na pia kama mjasiliamali kwa gd number of yrs,pamoja na pesa watu huwa wanasahau kitu cha muhimu kabisa na basic nacho tunakiita

Conception stage hii ni stage ambayo muhimu na ambayo anaetaka kujenga anatakiwa atoe idea yake nini anataka na kiwe wapi kulingana na mahitaji yake,bila hata ya kuenda stage nyingine wataalamu tutamshauri na kumwambia pesa inatosha au la!

Jamani is a professional thing!

Tunaamini kila mtu aweza kujenga lakini mtaaalum atajenga kwenye reasonable cost na acceptable quality!

Good day!

Then Hapo ndio mnaposhindwana na wanye pesa ndogo....kwa kuwa Eng wa ujenzi wameshasoma kwa magumu waliyo pitia hawako tayari kumsaidia mtu kwenye kiwango cha chini cha pesa kama huyu mhusika...Charges za kukuona kwa office na kumshauri utataka ubambike laki mbili
kwanini mtanzania huyu asikimbie kwa mafundi wa mtaani au wazoefu wanoa jenga nyumba bila ma Qualified Eng?

Tena the worse thing atakapo kwambia ana hizo 20m...Ndio hapo na wewe utakapo taka kuhakikisha unakula hata laki tano...Hapo ndio Eng. Wanapo kimbiwa na watu wengi mnabaki kulalamika watu wanajenga nyumba za kiwango cha chini....Mie nina watu nawaafahamu kilicho mgharimu zaidi ni mchoro baada ya hapo anakwenda kwa fundi wa mtaani alishajenga nyuma kama 20 hivi anamjengea kwa resonable price.

Eng. wa bongo kwanza kumkuta site ni kazi sana anaamka saa nne kama ndio ana office yake anapita break point saa tano ndio ofisini site atafika saa ngapi? Kazi kwa simu tu........Yaani mpaka tubadilike sana tuwe na proffesionalizim kutumikia kile unacholipwa...huyu fundi wa mtaani utamkuta na yeye ana beba zege na vibarua wake which is little impresive
kwa wenye pesa yake...Eng wa bongo pls spare me sometime kama kuna wazuri out there ni vyema ila wengi wenu mkishapata kianzio huwezi muona site yaani ni wa kutafuta kwenye simu which add more cost.
 
Back
Top Bottom