Nawaza tu.

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
7,637
4,521
Sijui ni kwanini katika ulimwengu wa mapenzi ni wachache sana wanaokubali kubeba lawama?Wapenzi wengi wanapotofautiana au kugombana basi kila mmoja atamshutumu mwenzake kuwa ndio chanzo cha ugomvi huo,na wengine hufika mbali kabisa na kuanza kutangaza kwa watu kuwa yule bwana si lolote si chochote na ni mkorofi sijapata kuona,huyu naye atasema mwanamke gani yule mkorofi sijapata kuona,najiuliza kama wawili mnaopendana mkiamua kukaa chini na kumaliza tofauti zenu na penye makosa,mkosaji akakubali kubeba lawama itamgharimu nini?Nimesukumwa kuwaza hivi kwa kilichomtokea jamaa yangu ambaye kwa sasa ni marehemu.Alikuwa ameoa na kubarikiwa watoto wawili na cheo kikubwa kazini.Lakini mke wake alijaliwa wivu wa ajabu,na mbaya zaidi katika usichana wake alikuwa championi wa judo katika chuo alichosomea,hivyo jamaa yangu kila akirudi kachelewa kidogo basi ni ngumi mtindo mmoja.Kila wiki jamaa yangu alikuwa na kazi ya kununua fanicha mpya kufidia walizovunja,mwisho baada ya jamaa kuona nyumba haina amani akaamua kuwa mlevi.Na kwa bahati mbaya akaharibika maini na figo hali iliyopelekea kupoteza maisha.Na mke bado alimlaumu marehemu kuwa ulevi wake ndio umemuua asingeendekeza ulevi angekuwa bado hai.Sasa katika mawazo yangu ninajiuliza kama wawili hao wangekuwa na maelewano mapema yote hayo yangetokea?Msomaji nakuomba ujitathmini na kujiuliza,je uko tayari kubeba mzigo wa lawama ili kuokoa mahusiano yako?Nawaza tu wakuu,asanteni kwa kunisoma na nawatakia wote mapumziko mema katika sikukuu hii inayokuja na heri ya mwaka mpya pia.
 
kwa mwenye akili na ufumbuzi kichwani mwake wallah topic yako ina mafunzo makubwa sana hususan kwa walioko ndani ya ndoa,,,,
 
Kama ni kweli huyo mama anatisha!Alafu huyo mume kwanini hakumuacha?Mwanaume anaekubali kupokea kichapo kutoka kwa mwenza wake sijui anakua kapewa nini!! Nwyz watu wengi wanapenda kuombwa zaidi ya kuomba msamaha hata kama kosa ni lao!Kama wote mkiwa mmejiweka levo moja ni rahisi zaidi kuelewana kuliko ambao kila mmoja anajiona ni zaidi ya mwenzake!Hapo ndipo mtafaruku unapoanzia!
 
Shukrani Nilham kwa kunielewa maana wakati mwingine mimi mwenyewe huwa najishangaa kwa watu kutonielewa.
 
why not wasikuelewe???? and beside u ur self u know dat u are a great thinker,,let them understand u if they can,,,,and leave them if they cant,,,na ambao hawatakuelewa kwa post yako ilivyo clear basi hawafai kuwa humu sio magreat thinkers hao we kaa pembeni anza kucheki watu hapa,,,,u are wellcome..
 
Hebu mpe hilo somo huyo mama ili asiendelee kuchafua hali ya hewa kwa wasichana wengine wachumba wetu.
 
Sijui ni kwanini katika ulimwengu wa mapenzi ni wachache sana wanaokubali kubeba lawama?Wapenzi wengi wanapotofautiana au kugombana basi kila mmoja atamshutumu mwenzake kuwa ndio chanzo cha ugomvi huo,na wengine hufika mbali kabisa na kuanza kutangaza kwa watu kuwa yule bwana si lolote si chochote na ni mkorofi sijapata kuona,huyu naye atasema mwanamke gani yule mkorofi sijapata kuona,najiuliza kama wawili mnaopendana mkiamua kukaa chini na kumaliza tofauti zenu na penye makosa,mkosaji akakubali kubeba lawama itamgharimu nini?Nimesukumwa kuwaza hivi kwa kilichomtokea jamaa yangu ambaye kwa sasa ni marehemu.Alikuwa ameoa na kubarikiwa watoto wawili na cheo kikubwa kazini.Lakini mke wake alijaliwa wivu wa ajabu,na mbaya zaidi katika usichana wake alikuwa championi wa judo katika chuo alichosomea,hivyo jamaa yangu kila akirudi kachelewa kidogo basi ni ngumi mtindo mmoja.Kila wiki jamaa yangu alikuwa na kazi ya kununua fanicha mpya kufidia walizovunja,mwisho baada ya jamaa kuona nyumba haina amani akaamua kuwa mlevi.Na kwa bahati mbaya akaharibika maini na figo hali iliyopelekea kupoteza maisha.Na mke bado alimlaumu marehemu kuwa ulevi wake ndio umemuua asingeendekeza ulevi angekuwa bado hai.Sasa katika mawazo yangu ninajiuliza kama wawili hao wangekuwa na maelewano mapema yote hayo yangetokea?Msomaji nakuomba ujitathmini na kujiuliza,je uko tayari kubeba mzigo wa lawama ili kuokoa mahusiano yako?Nawaza tu wakuu,asanteni kwa kunisoma na nawatakia wote mapumziko mema katika sikukuu hii inayokuja na heri ya mwaka mpya pia.

Alikosa wa nje?
 
Kwangu mimi hua nakaa kimya tu, hua akianza kuongea simjibu, hata hivyo nae pia nikianza kuongea mm hua hajibu, so network inakata kwa mda flani hivi then baadae mood inarudi hasa tukiwa kitandani...nashukuru kwa hili
 
ubarikiwe sana kwa somo la unyumba,siwezi kuongeza kitu ila ktk ndoa jamani ukweli na uwazi ni muhimu sana,
 
Kwa kweli somo zuri sana hili la kufungia mwaka sema 2 hapa kwa 4ne kidubwashika cha senks sikioni ila nimejifunza ki2
 
Sijui ni kwanini katika ulimwengu wa mapenzi ni wachache sana wanaokubali kubeba lawama?Wapenzi wengi wanapotofautiana au kugombana basi kila mmoja atamshutumu mwenzake kuwa ndio chanzo cha ugomvi huo,na wengine hufika mbali kabisa na kuanza kutangaza kwa watu kuwa yule bwana si lolote si chochote na ni mkorofi sijapata kuona,huyu naye atasema mwanamke gani yule mkorofi sijapata kuona,najiuliza kama wawili mnaopendana mkiamua kukaa chini na kumaliza tofauti zenu na penye makosa,mkosaji akakubali kubeba lawama itamgharimu nini?Nimesukumwa kuwaza hivi kwa kilichomtokea jamaa yangu ambaye kwa sasa ni marehemu.Alikuwa ameoa na kubarikiwa watoto wawili na cheo kikubwa kazini.Lakini mke wake alijaliwa wivu wa ajabu,na mbaya zaidi katika usichana wake alikuwa championi wa judo katika chuo alichosomea,hivyo jamaa yangu kila akirudi kachelewa kidogo basi ni ngumi mtindo mmoja.Kila wiki jamaa yangu alikuwa na kazi ya kununua fanicha mpya kufidia walizovunja,mwisho baada ya jamaa kuona nyumba haina amani akaamua kuwa mlevi.Na kwa bahati mbaya akaharibika maini na figo hali iliyopelekea kupoteza maisha.Na mke bado alimlaumu marehemu kuwa ulevi wake ndio umemuua asingeendekeza ulevi angekuwa bado hai.Sasa katika mawazo yangu ninajiuliza kama wawili hao wangekuwa na maelewano mapema yote hayo yangetokea?Msomaji nakuomba ujitathmini na kujiuliza,je uko tayari kubeba mzigo wa lawama ili kuokoa mahusiano yako?Nawaza tu wakuu,asanteni kwa kunisoma na nawatakia wote mapumziko mema katika sikukuu hii inayokuja na heri ya mwaka mpya pia.
nafahamu Mhadhiri mmoja alikuwa mchapa kazi na mkewe akawa anagombana nae kila siku akirudi naiti...maji yalipozidi unga msomi kachia mwanamke nyumba.... akatafuta hela akajenga nyingine...!!Hapo lawama abebe nani?
 
Join DateFri Sep 2010.........
Mkulu Utamashika lini huyo panya unaemkimbiza??:whoo:
 
ukweli mtupu hapo paka.....
huo mfano wa huyo rafiki yako unatisha kwakweli
na mi nashukuru kwa kuuweka hapo kwani tumejifunza kitu ambacho tunafanya lakini huwazi kama inaweza kumpeleka mtu kubaya kihasi hicho..

uwi Paka harusi lini sasa....
na dhani umesha jua mengi kuhusu maisha.....:party:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom