Nawaunga Mkono Madaktari

Hvi kwa kinacho endelea bungeni tangu uchaguz wa mwaka juz ni nini tumesikia cha kuufaidisha umma wetu zaidi ya kusikia mishahara ya wabunge,umeme,maji,mafuta kuongezeka kwa fujo? Kwanini daktari asiongezwe mshahara mara dufu kuliko hawa maswahubu kujimegea mishahara isiyo kifani bila jipya hapo ndani?
 
Wajibu wa kuhudumia afya ya Taifa ni mgumu sana - unatoa imani ya kuhudumia wananchi wakati uwezo wa kuhudumia wagonjwa ni mdogo.

MallipoSerikali ya Tanzania sio tajiri, wala sidhani kama inayouwezo wa kutimiza masharti ya madaktari - maana yanaambatana sana na madai ya wafanyakazi wengine wa umma. Nadhani swala hapa sio fedha tu, ni uwezo na utashi wa Serikali kutambua na kuelewa madai yao na mazingira ya madaktari na kujaribu kutoa heshima kwa kazi yao na yale yanayoweza kufanyiwa marekebisho yafanyike.

Mfumo wa Tiba
Mfuo wa afya umebinafsishwa kiasi kikubwa hatuwezi kusema majukumu hayo yaendelee kubebwa na sekta binafsi - huku tukibaki na hospitali moja ya kitaifa. Serikali inawajibu wa kuhudumia afya za wananchi wake kwahiyo ni lazima iwekeze kwenye afya, na kuunda mfumo utako wasaidia wasio jiweza.
 
Kwanza rais mwenyewe kuonyesha hajali maisha ya watu ameenda kuhudhuria mkutano wa uchumi huko ulaya.
Yupo na kundi la wapambe wanatumbua zaidi ya mil 300 kwa siku chache watakazokuwa huko.Sasa sijui ndio kaenda kuomba apewe hela aje awaongezee madakitari ! Kweli m.kwere huyu ana nazi kichwani sio ubongo.

Mungu ibariki Tanzania
 
MOds,
kwa nini michangio hii isiunganishwe sehemu moja ili mtiririko wa mawazo ueleweke. Hivi sasa kuna usumbufu kufuatilia mawazo mazuri yanatolewa kuhusu sakata hili kwenye threads tofauti
 
Wajibu wa kuhudumia afya ya Taifa ni mgumu sana - unatoa imani ya kuhudumia wananchi wakati uwezo wa kuhudumia wagonjwa ni mdogo.

MallipoSerikali ya Tanzania sio tajiri, wala sidhani kama inayouwezo wa kutimiza masharti ya madaktari - maana yanaambatana sana na madai ya wafanyakazi wengine wa umma. Nadhani swala hapa sio fedha tu, ni uwezo na utashi wa Serikali kutambua na kuelewa madai yao na mazingira ya madaktari na kujaribu kutoa heshima kwa kazi yao na yale yanayoweza kufanyiwa marekebisho yafanyike.

Mfumo wa Tiba
Mfuo wa afya umebinafsishwa kiasi kikubwa hatuwezi kusema majukumu hayo yaendelee kubebwa na sekta binafsi - huku tukibaki na hospitali moja ya kitaifa. Serikali inawajibu wa kuhudumia afya za wananchi wake kwahiyo ni lazima iwekeze kwenye afya, na kuunda mfumo utako wasaidia wasio jiweza.
Mkuu waadam mfumo wa AFYA ni wa Biashara, serikali haitakiwi kabisa kuingiza mguu wake. Makosa yapo ktk mfumo wenyewe maana wananchi wengi na hata hawa wafanyakazi wanafikiria ni jukumu la serikali lakini huwezi changanya vitu hivi ili kupata huduma nzuri. Maadam ni biashara basi hospital zinachukua jukumu hilo na ndiuo maana tunawalipa madaktari Tsh 50,000 kumwona halafu bado gharama za operation au kuandikiwa cheti cha kuchukua dawa. Hwa hawa wana zahanati nje wakikimbia huko na huko kutafuita utajiri..

Ni wananchi wanaoumia sio madaktari wanaodai Posho wakionyesha tu Tsh 10,000 wakati sisi wananchi tunalipa kila mmoja wetu anapomtembelea dakltari.. Kwa siku anaweza ondoka na Tsh 500,000 mbali kabisa na mshahara wake halafu ana zahanati yake nje ambayo wamekubaliwa ili kuongeza pato lao..Nchi hii imeharibika sana kuchanganya Ujamaa na Ubepari hatujui tumesimama wapi na mnashindwa kabisa kutetea maslahi ya wananchi badala yake mnatetea biashara za watu. Mbona Chuo Kikuu wakitaka kugoma huanza na Mukandala na manejimenti ya chuo kikuu kwanza..
 
Tatizo la sasa katika sekta ya afya, haliwezi kupatiwa ufumbuzi wa kuduma hata kama watawekwa pale Wizarani, the best Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu kutoka nchi za jumuiya ya madola. Hii ni kwa sababu we always fail to make the right diagnosis, na badala yake kuachia suala hili lijiendesha katika mazingira ya ‘siasa huru'.

Nia yangu ni kutoa maoni yangu kuhusu kiini cha tatizo hili, lakini kubwa zaidi, tusaidiane jinsi gani ya kulikabili sasa na kwa siku za usoni.

Katika Tanzania, Sekta ya afya inajengwa na 3 Tier System:

1. Basic Clinics, Dispensaries = First Level
2. District Hospitals = Second Level
3. Referral Hospitals and Specialty = Third Level. (e.g. of Referral Hospitals = Muhimbili, KCMC, Bugando, Mbeya) and Speciality (e.g. Specialities = Taasisi ya Moyo, Kansa etc).

Baadhi ya Mapungufu Yaliyopo katika mfumo/mpangilio huu ni pamoja na yafuatayo:

Pamoja na kwamba 75% ya mahitaji ya wananchi ya afya (health needs) yapo katika first level (i.e. basic clinics and dispensaries), huku asilimia 25% tu ya health needs zikiwa katika higherlevel i.e. referral hospitals and specialty, katika kupanga bajeti za wizara ya afya na ustawi wa jamii kila mwaka, serikali huwa haitengi fedha kwa kufuatana na mahitaji haya. Badala yake, asilimia 75% of Resources (madawa, vifaa, mishahara, posho, education and training etc) huwa zinapelekewa kwenye level ya juu (referral hospitals na Specialties). Jambo hili ni la kushangza kidogo kwa sababu kuu ifuatayo:

Katika kila siku ya mwenyezi mungu, outpatient diseases in Tanzania (magonjwa yasiyohitaji mgonjwa kulazwa zaidi ya kuonana tu na daktari kisha kurudi nyumbani), ni yafuatayo:

Malaria; Acute Respiratory Infection ; Numonia ; Kuhara; Eye infection; Skin Infection; Anaemia; na UTI.

Magonjwa ya kulala hayapo mengi kama yake ya kutohitaji kulala na haya ni pamoja na complicated malaria (ambayo huwa haitokei mara nyingi sana). Complicated malaria accounts for about 70% ya magonjwa yote yanayohitaji mgonjwa kulala. Mengine katika the remaining 30% ni TB, Ukimwi, ajali, na kuhara.

Hoja ya msingi hapa ni kwamba asilimia 90% ya magonjwa yote Tanzania yanaweza kupatiwa tiba katika vituo vya afya (dispensaries and clinics), iwapo vitapatiwa tu wataalam wa kawaida, vifaa basic tu vya diagnosis, na madawa. Lakini kutokana na serikali kutojali eneo hili in terms of budget and resources allocation, matokeo yake ni wataalam wengi kurundikana kwenye higher levels of the 3 tier health system, na kupelekea uwepo wa hali ya - Too Much Manpower Chasing Too Few Resources.

Kwanini Serikali inaendekeza jambo hili?

Sijui, lakini ningekuwa Waziri wa Afya ningeweza kutetea kwa hoja zifuatazo:

· Moja, kuna umuhimu wa serikali to train train wataalaum ili kupata wataalam wa kutosha kwenda kutoa huduma at the lower levels i.e. district hospitals, and clinics and dispensaries, ndio maana kila mwaka tunatenga fedha nyingi sana kwa ajili ya zoezi hili.
· Pili, Tanzania hakuna Health Insurance Market yenye kuweza kuwasaidia walio wengi, kwani walio wengi cannot insure themselves against the risk of serious illnesses, injury and the consequent need for very expensive treatment. Kwahiyo kuna umuhimu wa serikali kutenga fedha nyingi kwenye level ya juu (Referral hospitals and specialty hospitals – moyo, saratani, n.k), kuliko level za chini, kutokana na kutokuwepo kwa health insurance market kwa maskini.

Lakini majibu haya yanazaa maswali mengine. Kwa mfano:

1. Suala la kwanza - pamoja na resources nyingi kwenda to higher level, kwanini magonjwa yote makubwa uhitaji serikai kupeleka wagonjwa India na kwingineko. Fedha zinazotengwa kila mwaka hazitoshi kuzuia hili?

2. Suala la pili ni juu ya mahitaji ya fedha nyingi kwa serikali to train wataalaum wanaohitajika mikoani/wilayani/vijijini. Pamoja na fedha za walipa kodi kutengwa kwa wingi sana kila mwaka kwa ajili ya zoezi hili, kwanini Tanzania bado inabakia kuwa moja ya nchi yenye the highest ratio ya population per doctor. Requirement ya World Health Organization (WHO) ni kwamba, kila daktari anatakiwa ahudumie watu wasiozidi 10,000 (elf kumi). Lakini sasahivi, hali ipo vipi Tanzania?

Kwa hali ya Sasa, kwa wastani (national average Tanzania) ni wastani wa watu 64,000 per doctor. Na kuna mikoa ambayo hali ni mbaya sana, kwa mfano:

· Mkoa wa Mara = 167, 000 people per doctor.
· Kigoma kwa Mheshimiwa Zitto na Kafulila, 308, 000 people Per Doctor.
· Mwanza = 144, 000 per doctor
· Rukwa kwa Mh. Pinda = 121, 000 people Per doctor
· Tabora kwa Mh. Sitta = 132, 000 people per doctor.

Inakuwaje hakuna uwiano wa wingi wa fedha zinazotengwa kila mwaka kwa ajili ya zoezi hili, hazina uwiano na takwimu hizi za afya kitaifa? Ni mikoa michache sana yenye ahueni katika hili, nayo ni:

· Arusha = 22,000 people per doctor
· Pwani = 32, 000 people per doctor
· Morogoro = 56,000 people per doctor
· Dar-es-salaam = 24,000 people per doctor
· Ruvuma = 57,000 people per doctor.

3. Suala la tatu: Katika Tanzania ya leo, karibia 50% (nusu) ya hospitali zote ni za NGOs, huku nusu iliyobakia ni mchanganyiko wa serikali na sekta binafsi. Na hali hii imekuwa hivi miaka nenda miaka rudi. Kwanini hali hii haibadiliki kulingana na wingi wa fedha za walipa kodi zinazotengwa miaka nenda, miaka rudi, kwa ajili ya bajeti ya wizara ya afya?

4. Suala la nne: Katika Tanzania ya leo, karibia 25% ya clinics na dispensaries ni za NGOs, huku zilizobakia zikiwa ni za serikali. Nyingi ya hizi zipo vijijini. Lakini kama tulivyokwisha ona, ni asilimia 25% tu ya bajeti ya serikali ndio uelekezwa kwenye mahitaji ya vijijini ambako asilimia 70% ya watanzania ndio wanaishi. Ndio maana, kwa ujumla, Clinics na Dispensaries zote Tanzania zilizo chini ya serikali hazina wataalam wa kutosha, vifaa, wala madawa. Matokeo yake ni kwamba, asilimia 70% ya Watanzania wanategemea huduma za afya zinazotolewa na NGOs, Waganga wa Kienyeji, huku wengine wengi wakiamua kupotezea tu magonjwa mengi na kumwachia mungu awaongoze.

5. Na suala la mwisho: Madaktari wengi wanaosomeshwa na fedha za walipa kodi hutumia muda mwingi sana kutoa huduma za afya katika hospitali binafsi, kuliko kule walipoajiriwa na serikali. Je, ni nini kinawasukuma kufanya hivi? Ni mishahara midogo au kuna sababu nyingine?
 
ikiwa takribani siku ya tatu mfululizo madatari tanzania kuigomea serikali kutoa huduma kwa wagongwa kwa madai:

1. Kuitaka serikali kuboresha huduma kwa wagonjwa ( kutokulala chini, kukosa vipimo muhimu, dawa, oxygeni, vitendea kazi vinavyopelekea kutoa huduma duni)

2. Kuipiga marufuku serikali kutumia hospitali kuu nchini kama stand za kuwapeleka wakubwa nje ya nchi kutibiwa na kutelekea kutohamasika kuboresha hospitali nchini.

3. Kupewa masilahi yao kama ilivyoandikwa kwenye nukuu za serikali.

4.kupewa huduma bora za afya pale wanapougua kama wawatendeanyo wagonjwa. (green card)

5. Kuwatoa madarakan wakuu wa wizara maana ndio kikwao.

6. Kuwarudisha interns waliofukuzwa bila hatia muhimbili bila mashariti.

Mimi binafsi kwa tafasiri ya haraka yote yalianisha ni madai halali na ni haki ya mgonjwa na daktari pia wanachofanya ni wajibu wao, naiomba serikali isijifanye kiziwi ndugu zetu wanaumia, ilishungulikie shala hili bila ubabaishaji.
naunga mkono madai ya madaktari ni taifa la ajabu ambalo linaona fahari ya viongozi wao kuwa na ndege binafsi wakati wajawazito wana share kitanda wannne wanne, wabunge wanakuwa highest paid employees , wakati wataalamu na wazalishaji wanaachwa wajihangaike wenyewe, watoa huduma iwe daktari mwalimu, transporter na wahudumu wa hotel wanachwa waibe vifaa au bidhaa kazini kwao ili maisha yaende.
 
Duh, kaka sina hata nyongeza, lakini napenda tu kuwaomba mods waiache nyuzi hii hadi kesho niisave ili niifanyie utafiti zaidi. Good analysis...
 
MOds,
kwa nini michangio hii isiunganishwe sehemu moja ili mtiririko wa mawazo ueleweke. Hivi sasa kuna usumbufu kufuatilia mawazo mazuri yanatolewa kuhusu sakata hili kwenye threads tofauti

This is a very valid observation. Huko nyuma moderators walikuwa smart na flow ya michango ilikuwa bayana. Nadhani siku hizi kumekuwepo na watu kwa makusudi wana anzisha a parallel topic na matokeo yake ni kuleta fujo mwishowe some hot threads are just buried. We can introduce a black box where members I mean pure Great Thinkers can contribute in Shilings to cover/ pay mods vinginevyo some of us are finding life very difficult. Ni bora zikawekwa a few but burning issue then they are discussed for a defined period of time and then closed of course with priority. Let us discuss this issue.
 
ikiwa takribani siku ya tatu mfululizo madatari tanzania kuigomea serikali kutoa huduma kwa wagongwa kwa madai:

1. Kuitaka serikali kuboresha huduma kwa wagonjwa ( kutokulala chini, kukosa vipimo muhimu, dawa, oxygeni, vitendea kazi vinavyopelekea kutoa huduma duni)

2. Kuipiga marufuku serikali kutumia hospitali kuu nchini kama stand za kuwapeleka wakubwa nje ya nchi kutibiwa na kutelekea kutohamasika kuboresha hospitali nchini.

3. Kupewa masilahi yao kama ilivyoandikwa kwenye nukuu za serikali.

4.kupewa huduma bora za afya pale wanapougua kama wawatendeanyo wagonjwa. (green card)

5. Kuwatoa madarakan wakuu wa wizara maana ndio kikwao.

6. Kuwarudisha interns waliofukuzwa bila hatia muhimbili bila mashariti.

Mimi binafsi kwa tafasiri ya haraka yote yalianisha ni madai halali na ni haki ya mgonjwa na daktari pia wanachofanya ni wajibu wao, naiomba serikali isijifanye kiziwi ndugu zetu wanaumia, ilishungulikie shala hili bila ubabaishaji.
hasa namba mbili
 
huyu ni Mkandara kweli!!?? this is too low kwa level yako, hivi hapa tunaweza kukutofautisha na Maralia Sugu? kwa hiyo solution ya matatizo haya ni kuwa na Mahakama ya kadhi na tujiunge na OIC?
Well kuanzia sasa hivi Mkandara siye yule umjuaye tena. Mimi nalilia maslahi ya wananchi na sio ya Kanisa wala Msikiti. Tunalipa kodi zetu sasa wanagoma ili iweje kama sio tufe sisi, wakati wameshakatiwa fungu na serikali. nani anayepanga matumizi ya uendeshaji biashara zao kama sio kamati ya CSSC. Na hata wangekuwa Bakwata ningewashambulia kama navyofanya hapa maadam nachokitazama ni maslahi ya wananchi sio dini wala dhehebu.

Kama madaktari wanataka kugoma waanze na kwenda ktk menejimenti zao kujua kulikoni. Tena tunatakiwa kabisa kudai CSSC watupe matumizi ya ruzuku zetu maana mkuu wangu hata wewe Mkristu unalipia fedha hizi ktk kodi na bado unatozwa kumwona daktari. Hakuna nafuu kwako wewe wala mimi sote tunaumizwa, hivyo unapolifanya swala hili liwe la Udini ndipo napowashangaa wakati linakuumiza hata wewe. Hawa ni watu tu binadamu kama wewe mnawaogopa kitu gani?... kwa sababu viongozi wa dini!... Upuuzi mtupu ndio maana CCM itatawala milele kwa kuwagawa.
 
Wananchi ndio walisaini mkataba na serikali kupata huduma za afya katika mchakato wa upigaji kura. Hivyo waelewe basi kuwa madakitari ni sehemu yao na sio kama wana hila na maisha yao. Ni wakati ambao wanaweza kufunguka na kuchukua tahadhari siku za usoni.
 
Well kuanzia sasa hivi Mkandara siye yule umjuaye tena. Mimi nalilia maslahi ya wananchi na sio ya Kanisa wala Msikiti. Tunalipa kodi zetu sasa wanagoma ili iweje kama sio tufe sisi, wakati wameshakatiwa fungu na serikali. nani anayepanga matumizi ya uendeshaji biashara zao kama sio kamati ya CSSC. Na hata wangekuwa Bakwata ningewashambulia kama navyofanya hapa maadam nachokitazama ni maslahi ya wananchi sio dini wala dhehebu.

Kama madaktari wanataka kugoma waanze na kwenda ktk menejimenti zao kujua kulikoni. Tena tunatakiwa kabisa kudai CSSC watupe matumizi ya ruzuku zetu maana mkuu wangu hata wewe Mkristu unalipia fedha hizi ktk kodi na bado unatozwa kumwona daktari. Hakuna nafuu kwako wewe wala mimi sote tunaumizwa, hivyo unapolifanya swala hili liwe la Udini ndipo napowashangaa wakati linakuumiza hata wewe. Hawa ni watu tu binadamu kama wewe mnawaogopa kitu gani?... kwa sababu viongozi wa dini!... Upuuzi mtupu ndio maana CCM itatawala milele kwa kuwagawa.

Kwahiyo unapendekeza waislamu wanyang'anywe yale majengo ya morogoro ambayo ndio Muslim University? hivi pesa za EPA, RADA, Ndege ya Rahisi, Meremeta, Kiwira, Richmond/ Dowans haya madudu yote yanasababishwa na kanisa?
Hivi hata wewe umeingia kwenye mkumbo wa kuleta soga za kwenye kahawa? hivi hata Petrol inayopitia Bandari ya Dar es salaam kwenda Rwanda inauzwa bei ya chini kuliko Tanzania hivi bado hujui tatizo ni nini? pole sana unazeeka vibaya mno.
 
Back
Top Bottom