WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
I smell udini, missionary haijawahi kujenga hospitali zimjengwa naserikali ya kikoloni ambao walikuwa wakiongoza kikristo; walitumia kodi za wananchi wote wa Tanzania, "Hakuna hospitali ya missionary" kuna hospitali za zilizojengwa na serikali za wakoloni wakristo
Kumekucha!
Je zipo zilizojengwa na wafuga watumwa ambao hawakuwa wakristo?! Jamani udini huu mbona utatumaliza!KWANINI kila kitu tunajaribu kumtafuta mchawi na mara zote ni mkristo? Sasa hizo zilizo za serikali ya sasa zimeongeza ubora upi? Kwanini leo madaktari wanagoma? Kwanini huduma zimekuwa "mbovu" kwenye hospitali za serikali? Inakuwaje hospital za misheni za sasa hivi zimeendelea kuwa kimbilio la kila mtu hata asiyekuwa mkristo?
Back to the issue:
Huu mgomo wa madaktari una mengi ndani yake. Madai yao kama yatatekelezwa itakuwa faida hata kwa wagonjwa maana wananchi na serikali watakuwa na HAKI ya kuwataka wawajibike kikamilifu.Huwezi kutegemea huduma bora kutoka kwa daktari mwenye njaa, asiye na vifaa, mwenye hasira na uchungu!Tena ni hatari sana kuhudumiwa na daktari mwenye hasira.Hata wasingegoma, watu bado watakufa kwa kukosa huduma iliyotolewa kwa "moyo mmoja".Daktari anayetumia "ofisi" yake kujitafutia chochote siyo daktari mzuri hata kidogo na ni daktari hatari sana.Serikali ituepushie vifo visivyo vya lazima kwa kuwasikiliza madaktari.
Serikali itende haki kwa kila kundi na siyo kubagua baadhi. Huwezi kusema Wabunge kwa mfano ni bora kuliko madaktari au waalimu. Madhara ya madaktari kugoma ni kupoteza uhai.Madhara ya waalimu kugoma ni kushuka kwa elimu, madhara ya wabunge kugoma ni nini? ITAKULA KWAO WENYEWE!