Nawaunga Mkono Madaktari

hii ni siasa tu
Tanzania haipo sawa na Egypt wala Libya

kama wanasiasa wameshindwa kutoa shinikizo kwa watala
madaktari wasitumike kufanya siasa huku 'watu wasiokuwa na hatia' wanakufa...

serikali iliyopo ni kama viziwi

walijaribu chama cha wafanyakazi na wakazimwa.....

kilichopo sasa ni kujaribu kutoa maji kwenye jiwe while wasio husika ndo watakufa.....

tunajidanganya mno na kuiga Misri na Egypt.....ukweli sisi bado saana.....

wamefukuzwa wanafunzi chuo kikuu hakuna mwanasiasa aliekwenda kuwasaidia.....
tusiwaponze hawa madaktari

utawala huu unahitaji 'political interverntion...na sio madaktari'

The Boss,

Pamoja na ukweli kwamba watu wasio na hatia wanateseka na kuumia sana, inasikitisha kuona watekelezaji wa huduma za afya wanachukuliwa kirahisi rahisi tu kama hawana mpango. Hii ni moja ya professional lulu, sio Tanzania tu, bali ulimwenguni kote. Tunajidanganya kuwafanya kama si lolote si chochote kwasababu ya kupanda ndege haraka haraka kwenda India.

By the way, Nchi hii mtu anayeonekana wa maana ni nani? Au wote tukajazane foreign affairs na ikulu, maana pengine those are the areas given the required attention.

Kama tunawanyanyapaa hapa, watatukimbia....ndio yale yale ya kichwa cha mwendawazimu ambacho kila mtu anajifunzia kunyoa. Akishajua kunyoa anaenda kufungua saloon yake mbele ya safari.
 
Madaktari waliogoma walianza kubeep baada ya kudai madaktari waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo warejeshwe, Isitoshe Serikali mnajua fika kuwa Madaktari wana madai yao wanaidai Serikali.

Katibu Mkuu Blandina Nyoni aliwajibu kwa kejeli baada ya kusikia madai yao, Sasa na nyie Serikali mkajifanya viziwi msiojua kula la vipofu mkawashika mikono na sasa wamegoma kabisaaaa wanadai Mnofu wao.

Hamkuona mwisho wake ni wapi?? Mbona serikali inajifanya haisikii na sasa wamegoma mnataka tena kuwafuata??? Jifanyeni viziwi hivyo hivyo,
sometimes kinga bora sana kuliko Tiba...

I am tired of this...Ni bora ingetokea ghafla ningeelewa sana ni ghafla na nguvu ya dharura itakiwe..Nyoni na yeye kazi imemshinda.
Ipo siku.
 
Uamuzi wa madaktari kugoma haukuwa uamuzi rahisi; ni uamuzi ambao umekuja ukiwa na gharama kubwa kwao na kwa taifa vile vile. Lakini uamuzi ambao umekuja kwa sababu umelazimishwa. Sera ambazo zimekuwa zikisimamia sekta ya afya zimeonekana kushindwa na sasa haya ni mavuno yake. Upo mgogoro katika sekta hiyo na licha ya kuongezwa kwa vitu bado inaonekana watawala wameshindwa kabisa kujenga mfumo wa kisasa wa afya.

Hivyo, naamini madai ya madaktari ni hatua ya mwanzo ya kudai huduma bora na mfumo wa kisasa. Siamini kama ni suala la mishahara na maslahi ya madaktari tu; binafsi naamini ni suala linalohusiana na a comprehensive healthcare reform.

a. Hatuwezi kuendelea kuwa na serikali inaendesha mahospita mengi ambayo haina uwezo wa kuyahudumia - wakati umefika wa kufikiria serikali kuachia hospitali - ibakie na hospitali kama za jeshi n.k Tunaweza vipi kuzitoa hospitali kutoka kwenye mikono ya serikali na kuzileta kwenye sekta binafsi au ushirikiano wa sekta binafsi na ya umma?

b. Mfumo wa sasa wa centralized policy ya afya kwa taifa zima hata kwa mambo madogo umepitwa na wakati. Ipo haja katika kuangalia mfumo wetu wa afya kufikiria jinsi ya kufanya healthcare kuwa na a local outlook zaidi na hivyo kuwa ni ya sehemu ilipo.

c. Kuboresha maslahi ya watendaji wa sekta ya afya kwa kuweka motisha zaidi, uhuru zaidi na vile vile kuinua elimu. Mojawapo ya matatizo ambayo ni wazi yapo ni jinsi gani madaktari na wauguzi wetu wanakuwa upgraded katika ujuzi na elimu yao.

Ni kwa sababu hizi na nyingine naamini kuunga mkono mgomo wa madaktari ni jambo la kizalendo zaidi kuliko kuendelea kukaa kimya. Wao madaktari wanapodai maslahi zaidi na mafao zaidi wajue kabisa kuwa wananchi nao wanajiandaa kuwadai wao zaidi katika huduma na ubora wa huduma wanazotoa. Hivyo, wasikubali kuachilia kirahisi hadi wawe na uhakika kuwa madai yao ya msingi kabisa yameangaliwa na yanalenga katika kuboresha sekta ya afya nchini.

Nawaunga mkono madaktari katika mgomo wao!

Hapo penye red mkuu haiwezekani labda CCM itoke madarakani kwani huo ndio mtego wao kwa ndugu zetu ingawa nao hawaoni kama hawapatiwi kile kilichotakiwa, kumbuka kwenye ahadi zake mkuu kwenye uchaguzi karibu kila mkoa aliahidi Hospitali ya rufaa? kweli ukiwa na ufahamu wa jinsi tu Muhimbili, KCMC, Bugando, Mbeya, zilivyo kimajengo tu achilia mbali vifaa vyao duni basi utatambua kuwa alitoa ahadi gani na wapi tunaelekea
 
SASA WAINGIA DODOMA, MBEYA, PINDA AWAANGUKIA ATAKA WAZUNGUMZE

Waandishi Wetu | Mwananchi
25 January 2012

MGOMO wa madaktari ulioanza juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), umesambaa na kuingia katika Hospitali za Mwanyamala na nyingine katika Mikoa ya Dodoma na Mbeya.

Kutokana na hali hiyo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ametoa tamko akiwataka wawakilishi wa madaktari hao wafike ofisini kwake wakati wowote ili wazungumze naye na kupata suluhu ya tatizo hilo.

Katika hospitali ya Muhimbili, mgomo huo jana uliingia katika siku ya pili huku madaktari wastaafu wanaofanya kazi kwa mkataba, wakipanga kuwasilisha pendekezo kwa uongozi wa hospitali hiyo kutaka kuwapunguzia kazi kwa kuondoa shughuli za upasuaji.
 
Uamuzi wa madaktari kugoma haukuwa uamuzi rahisi; ni uamuzi ambao umekuja ukiwa na gharama kubwa kwao na kwa taifa vile vile. Lakini uamuzi ambao umekuja kwa sababu umelazimishwa. Sera ambazo zimekuwa zikisimamia sekta ya afya zimeonekana kushindwa na sasa haya ni mavuno yake. Upo mgogoro katika sekta hiyo na licha ya kuongezwa kwa vitu bado inaonekana watawala wameshindwa kabisa kujenga mfumo wa kisasa wa afya.

Hivyo, naamini madai ya madaktari ni hatua ya mwanzo ya kudai huduma bora na mfumo wa kisasa. Siamini kama ni suala la mishahara na maslahi ya madaktari tu; binafsi naamini ni suala linalohusiana na a comprehensive healthcare reform.

a. Hatuwezi kuendelea kuwa na serikali inaendesha mahospita mengi ambayo haina uwezo wa kuyahudumia - wakati umefika wa kufikiria serikali kuachia hospitali - ibakie na hospitali kama za jeshi n.k Tunaweza vipi kuzitoa hospitali kutoka kwenye mikono ya serikali na kuzileta kwenye sekta binafsi au ushirikiano wa sekta binafsi na ya umma?

b. Mfumo wa sasa wa centralized policy ya afya kwa taifa zima hata kwa mambo madogo umepitwa na wakati. Ipo haja katika kuangalia mfumo wetu wa afya kufikiria jinsi ya kufanya healthcare kuwa na a local outlook zaidi na hivyo kuwa ni ya sehemu ilipo.

c. Kuboresha maslahi ya watendaji wa sekta ya afya kwa kuweka motisha zaidi, uhuru zaidi na vile vile kuinua elimu. Mojawapo ya matatizo ambayo ni wazi yapo ni jinsi gani madaktari na wauguzi wetu wanakuwa upgraded katika ujuzi na elimu yao.

Ni kwa sababu hizi na nyingine naamini kuunga mkono mgomo wa madaktari ni jambo la kizalendo zaidi kuliko kuendelea kukaa kimya. Wao madaktari wanapodai maslahi zaidi na mafao zaidi wajue kabisa kuwa wananchi nao wanajiandaa kuwadai wao zaidi katika huduma na ubora wa huduma wanazotoa. Hivyo, wasikubali kuachilia kirahisi hadi wawe na uhakika kuwa madai yao ya msingi kabisa yameangaliwa na yanalenga katika kuboresha sekta ya afya nchini.

Nawaunga mkono madaktari katika mgomo wao!

Unawaunga mkono kwa sababu haujauguliwa, Mwaswala ya siasa tusichanganye na afta za binadamu
 
kwa nini iwe mpaka wagome ndo akutane nao.haya matatizo ya madaktari yatatuliwe kwa mazungumzo nasio kwa maneno ya kisiasa.
 
Mkuu MM...katika hili wacha nafsi ipingane na dhamira,
Mgomo wa Madaktari ni hujuma,ni hujuma dhidi ya uhai wa binadamu...na ni imani yangu kwamba kuna influency nyuma ya hili ombwe! Nidhanivyo kuna aliyelipia zumari hii na seem wimbo huu wa kugoma ni chaguo lake... Sijui ni utaratibu gani hasa walitakiwa kutumia ila frankly njia waliyoichagua ni msiba na simanzi kwa masikini wasijikimu kwenda India...Ni hujuma...ni kukosa ubinadamu!
 
I smell udini, missionary haijawahi kujenga hospitali zimjengwa naserikali ya kikoloni ambao walikuwa wakiongoza kikristo; walitumia kodi za wananchi wote wa Tanzania, "Hakuna hospitali ya missionary" kuna hospitali za zilizojengwa na serikali za wakoloni wakristo

Pumbafu wewe... umejaaa udini tuuu pasipo kujua unachoandika... Yaani nia yako ilikuwa kuuponda ukristo na mfumo wa kikrustu uliokuwepo kisa wakoloni wa kijerumani walikuwa wakristo... Hujui kama na waarabu walitawala... wao wameacha nini ambacho kinaonekana??

Wameacha shule ngapi au hospitali ngapi.... iwe Znz au Bara... Acha uzuzu kabisa... Na by the way hospitali za missionary si lazima ziwe za wakristu hata waislam wanazo... ni charitable institutions, mwehu wewe..
 
hii ni siasa tu
Tanzania haipo sawa na Egypt wala Libya

kama wanasiasa wameshindwa kutoa shinikizo kwa watala
madaktari wasitumike kufanya siasa huku 'watu wasiokuwa na hatia' wanakufa...

serikali iliyopo ni kama viziwi

walijaribu chama cha wafanyakazi na wakazimwa.....

kilichopo sasa ni kujaribu kutoa maji kwenye jiwe while wasio husika ndo watakufa.....

tunajidanganya mno na kuiga Misri na Egypt.....ukweli sisi bado saana.....

wamefukuzwa wanafunzi chuo kikuu hakuna mwanasiasa aliekwenda kuwasaidia.....
tusiwaponze hawa madaktari

utawala huu unahitaji 'political interverntion...na sio madaktari'
Mkato wa tamaa!! kila mtu anafanya siasa! Maisha ni siasa!tunakula na tunaishi siasa! Usitudanganye kungoja wanasiasa wepi!?
Some of us we have nothing to loose!! hakuna kuogopa hapa!!
 
GreatThinkers

Again Members of parliament have been pushing do hard to get their allowances increased claiming that the cost of living has gone up(as per speaker justification ), now I wonder has this being the case only for MP?

What about the doctors and nursies out there? The teachers and the rest? Are they not affected with high living costs? This signifies poor performance by the government which is biased to only few;

I strongly support them doctors for their strike.

Doctors even Teachers Go-Please Go ahead life is Tough to all.
 
​Napinga migomo ya madaktari lakini naunga mkono kama wangefanya maandamano baada ya kazi kwani mwisho wa siku katika mgomo wao watanzania wa kipato cha chini ndio wanaoteseka na si viongozi wa serikali kwani wao wataenda kutibiwa nje ya nchi na kuacha wanyonge wakifa

Mkuu Godwine,

Ninalo swali moja tu,

Hospitali zote za Dar es Salaam ambazo nimewahi kwenda kuwatembelea marafiki zangu kitanda kimoja wanalala 3 na wengi wao wako chini. Huduma ni mbovu hakuna dawa, seuse maslahi ya madaktari? Wamesahauilika kabisa. Madaktari wenyewe wanasema tunawabadilishia wagojwa magonjwa. Ukija na Malaria unapewa dawa ya Malaria halafu unaondoka TB kwa sababu ya msongamano. Hali hii mpaka lini?

Madaktari maslahi yao yamebanwa - wako frastrated na hawawezi kutoa huduma bora, hali hii mpaka lini?

Rafiki yangu na ndugu yangu wa karibu alifanyia mama mjamzito operation kwa tochi ya simu majuzi hapo mwananyamala baada ya umeme kukatika. Alipomfuata Mganga mkuu wa hospitali aliambiwa, Sina pesa na Serikali imesema haina pesa. Sasa ameniambia anataka kuacha kazi kuliko kuona wagonjwa wanakufa mbele ya macho yake kwa magonjwa yanayotibika na maslahi yake duni sana. Hali hii hadi lini?

Ifahamike hapa Tanzania hao wagonjwa wa kipato cha chini unaowatetea kwa taarifa ambazo serikali inakubali yenyewe ni kwamba, kwa siku mmoja tu wanakufa wamama wajawazito kati ya 24 hadi 36( within 24 hrs) Sasa kuna vifo gani vipya unavyosema vitasababishwa na mgomo wa madaktari? Vifo vya kizembe vipo tu kabla ya mgomo.

Mkuu MM...katika hili wacha nafsi ipingane na dhamira,
Mgomo wa Madaktari ni hujuma,ni hujuma dhidi ya uhai wa binadamu...na ni imani yangu kwamba kuna influency nyuma ya hili ombwe! Nidhanivyo kuna aliyelipia zumari hii na seem wimbo huu wa kugoma ni chaguo lake... Sijui ni utaratibu gani hasa walitakiwa kutumia ila frankly njia waliyoichagua ni msiba na simanzi kwa masikini wasijikimu kwenda India...Ni hujuma...ni kukosa ubinadamu!
Haisadii ndugu maisha ya watanzania tayari ni kifo!! Wakati madaktari wanagoma unajua 300bn zimetumika kwa safari ya rais.
Kazi ya Serikali ni kutoa huduma hizo kwa wananchi wake wanawalipa kodi!! siyo kazi ya mtu mmoja mmoja!!

Kila ukiona tatizo unahisi mkono wa mtu!!!Angalia katika pande nne na ufanye uchambuzi: Say; Kodi za watanzania zilitakiwa zitatue matatizo ya afya, elimu, maji nk. kwa njia ya kuwalipa vyema watoa huduma kama madaktari.

Sasa kama umetoa kodi yako; kipaumbele kikawa kumtembeza mkuu wa nchi dunia yote!!! wewe unataka kuwalaumu madaktari! au" wachawi" waliowashawishi madaktari unawaona gizani.

Hali tuliyofikia inahitaji kila mtanzania apate uchungu na kodi na raslimali za nchi na jinsi zilivyotumika siyo kuona na kusingizia "wachawi" walio gizani.
 
Mimi nilidhani Taasisi kama Muhimbili inajitegemea katika mambo mengi kama mashirika mengine ya UMMA. Kwamba:
-Wangejipangia mishahara yao na malipo mengine.
-Wangekuwa na "scheme of service" yao wenyewe.
-Mapato wanayokusanya pale ni yao, kwa ajili ya uendesha wa taasisi hii.

Kama hivyo ndivyo sioni ni vipi serikali inaingia kwenye sakata hili. Kama sivyo ilivyo ni vizuri sasa Muhimbili, hospitali za rufaa, hospitali za mikoa na wilaya zikaingizwa kwenye mfumo huu kisha serikali ikatenga RUZUKU kubwa tu kwa ajili yao. Tunapelekaje ruzuku kwenye vyama vya SIASA halafu tushindwe hili?

Kubinafsisha huduma hii kwa sasa ni balaa. Bora akina mama waendelee kulala mzungu wa nne pale Amana na kwingineko huku wakipata angalau kidogo kama ilivyo sasa. Mwalimu aliyawezaje haya kwa kodi zile enzi hizo?
 
Pumbafu wewe... umejaaa udini tuuu pasipo kujua unachoandika... Yaani nia yako ilikuwa kuuponda ukristo na mfumo wa kikrustu uliokuwepo kisa wakoloni wa kijerumani walikuwa wakristo... Hujui kama na waarabu walitawala... wao wameacha nini ambacho kinaonekana?? Wameacha shule ngapi au hospitali ngapi.... iwe Znz au Bara... Acha uzuzu kabisa... Na by the way hospitali za missionary si lazima ziwe za wakristu hata waislam wanazo... ni charitable institutions, mwehu wewe..
Very good!! some of the nasty heads must be shattered when we are going serious!! thanks for shattering the religious marijuana corrupted heads!!
 
Unawaunga mkono kwa sababu haujauguliwa, Mwaswala ya siasa tusichanganye na afta za binadamu

Inawezekana unaamini kabisa kuwa unesema kitu profound! Kweli unafikiri nimechukua msimamo kwa sababu sijawahi kuuguliwa? Kwa vile ndugu zangu wameumbwa kwa mawe? Hivi tunapuzungumza ndugu yangu wa karibuanatakiwa kufanyiwa upasuaji ijumaa hii hapohapo nyumbani. Sasa nichukue msimamo tofauti baada ya kuangalia maslahi yangu kwanza?
 
Back
Top Bottom