Nawaunga mkono madaktari na wafanyakazi wengine wa sekta ya afya

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Mara zote mgomo wa madaktari ni jambo la mwisho kabisa katika jamii; ni ishara ya mambo kuwa mabaya na ushahidi wa kushindwa kwa sera za walioko madarakani. Kuanzia mwaka 2006 wakati ule mgomo wa kwanza kuikumba serikali ya JK wengi wetu tulitarajia kuwa wangeonesha ubunifu na uthubutu wa kutatua matatizo yanayokabili sekta ya afya nchini. Hata hivyo, miaka zaidi ya sita baadaye madai yale yale, yenye kuhusu mambo yale yale yakielekezwa kwa viongozi wale wale yamekuwa yakitolewa na karibu mara zote majibu yamekuwa yale yale "tukae mezani tuzungumze".

Kilele cha haya ni mazungumzo ambayo wengine kwa kweli tuliyabeza kwa sababu hayakufikia makubaliano ya jumla. Naamini wakati huu serikali ni lazima ioneshe kuwa inaweza kutatua matatizo na madaktari waoneshe msimamo kuwa wanachogombania ni maslahi makubwa zaidi - nafuu kwa wagonjwa. Binafsi, naunag mkono mgomo huu endapo hatima yake itafikia kwenye kufanya mabadiliko makubwa ya sekta ya afya ambayo itaonekana kumjali mgonjwa na yenye kuhakikisha huduma ya kisasa, nafuu inapatikana kwa urahisi na kwa uhakika kwa watu wote.

Nikijua uzito wa mgomo huu na matokeo yake kwajamii nashindwa kujizuia bila kuunga mkono nikiamini kuwa viongozi hawana uwezo wa kutatua matatizo haya hadi yabane kweli kweli kama tulivyoona mgomo wa mwisho. Madaktari wakikaa tena chini kunywa soda Ikulu watakuwa wamepoteza uhalali wao; mazungumzo yoyote sasa ni lazima yafikie kukubaliwa kwa madai namabadilikombalimbali tena kwa maandishi na yaonekane kwenye bajeti ya afya.

Hatuwezi kuwa kwenye mgomo wa sekta hii kila baada ya miezi sita!!! Suluhisho la kudumu liwe tokeo kuu la mgomo huu.

I support the doctors!
 
Mzee MM
Wale watetezi wa serikali watakushambulia, ukweli ni kwamba serikali haikuwa na nia ya kuatatua matatizo ya msingi

Kila wanapoomba mazungumzo ya mezani wanafanya hivo si kwa nia njema ndiyo maana mikutano sita kati kamati ya madakatri na serikali hawakufikia suluhu hata moja

Hata mazungumzo watakayoomba safari hii yatakuwa na sura hiyo hiyo
 
JK fanya michezo na hii migomo, baadhi ya nchi migomo ilianza kidogo kdigo mwisho Serikali ikaanguka.
 
Madaktari wamefanya ambacho PINDA,KIKWETE ,MKUU WA MKOA DSM...Hawakukitaarajia.wao waliamini kuwa wangeweza kuzima mgomo kwa kuitumia mahakama.....mahakama imetumika vibaya na madakitari wamepuuza....sasa nani bado anabisha kuwa jk ni dhaifu?
 
Kwa kweli uongozi unapimwa kwa jinsi mtu anatatua matatizo. Sasa watawaka wako kimya hakuna outrage lakini wakianza kuona machela na drips mitaani na kina Ananilea Nkya wanawashambulia ndio utaona hadi nawaziri wanaanza kutembelea mahospitali. Hii itabidi serikali nzima kujiuzulu.
 
Hivi nyie mnaamini tuna viongozi?
Kwa taarifa yenu walioko mbele yetu wakivaa heshima ya kuitwa viongozi ni wafanyabiashara za magendo tena waliokubuhu.
 
madhara ya huu mgomo utakuwa mkubwa kuliko hata ile iliowahi kutokea, madaktari wanafanya mgomo baridi, we support them,
 
Wakuu naunga mkono hapa.Madaktari wanagoma kwaajili yetu.Serikali "inajifanya" haina hela ya kuboresha afya.UFISADI TU!!
 
FRESH NEWS: UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI.
Leo ningependa turudijamvini kujadili kidogo kuhusu huu mgomo wetu, awali katika sehemu ya kwanza yamada hii, nilijaribu kuainisha madaiyetu, makubaliano na kuacha kwako mwanya wa kufikiri utendaji wa serikali yetu"SIKIVU" ilivyo na inavyofanya hadi sasa (kamahukubahatika kusoma hebu itafute facebook na Jamii forum ili upitishe machoKIDOGO TU ikiwa na thread title UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI)..leonilifikiri si vibaya tukijadili kuhusu madhara ya mgomo huu.
HALI HALISI HOSPITALINI:
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Ocean Road Institute, Temeke,Mwananyamala, Amana, Bugando, Mbeya, KCMC, ST.Francis, Haydom, Dodoma n.k. huku kote hakuna kinachoendelea..madakatarikwa maana ya General practitioner na Specialist, sio Assistant Medical Officer,AMO(KWANI KUNA UTOFAUTI KATI YA NGAZI ZAUDAKTARI KUTOKANA NA KISOMO/ELIMU-nisingependa kwenda katika hili) .. Hii ni TOTAL TOOLS DOWN,(TTD), episode III..
Kama tulivyosema awali hatudai posho, na ongezeko la mishaharatu(hii si priority hata katika madai), ila eti kulingana na majibu ya serikali,tutegemee madai hayo katika next next fiscal year(2013/2014) lakini hebu jiulize
1. Madai ya madaktari yalianza lini?
2. Madiwani waligoma ama kudai mshahara/posho lini??!
3. Priority ya Taifa ni wananchi(kupitia madai ya madaktari) au viongozi(kupitia poshompya za madiwani zilizotangazwa Bungeni)?
4. Nyongeza ya posho ya madiwani imetokea wapi?? ilipangwakatika bajeti?
5. Viongozi au wananchi hamuoni haya??

SISEMI TUNAHITAJI MISHAHARA YETU ILINGANE NA WABUNGE, MAWAZIRI, WAFANYAKAZI WATRA, BOT, n.k..LA HASHA!! ILA UNAPODAI MAZINGIRA BORA YA KAZI, NYONGEZA YAMSHAHARA,POSHO NA UNAPEWA MAJIBU YA DHARAU,.. NA WENGINE KAMA VIONGOZIKUJIONGEZEA(duringthe same period of our claims), HAPO NDIPO COMPARISON INAPOTOKEA, NAKULAZIMISHA TUFANANE NA NYIE!!
Katika hospitali tajwa hapo juu, Wakurugenzi, wakuu wa idarawamekuwa wakifanya vikao na kulipwa 50,000/=TSHS@SIKU toka mgomo kuanza23.06.2012.., Je, wananchi mnayajua haya? Jiulize kuna idara ngapi katikahospitali hizi? Nani anayetoa pesa hizi? Zitatoka hadi lini? Lengo kuu nikushawishi, kushurutisha madaktari turudi kazini… !!

VYOMBO VYA HABARI:
Katika "episode" mbili za "series" yetu hii ya Mgomo waMadaktari, vyombo vya habari vilianza kuripoti kuwa hakuna migomo, hadi palewatu wa HAKI ZA BINADAMU walipoingilia kati!!
Nasikititishwa sana na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC),kutotoa taarifa halisi wakati watu wanazidi kupoteza maisha, kweli hawaoni? Hawajuiau wanapuuzia?
Halafu mnatuitamadaktari si wazalendo? KWELI?? Napata shida sana kuelewa inakuwaje watanzaniawanaumia na viongozi kutotilia maanani madai yetu, ni kweli uhai wa mtuhauwekwi rehani lakini hatukuingiakatika mgomo huu kwa kuweka maisha ya watanzania wenzetu katika mizani, na ndiomaana muda wa mazungumzo ulikuwepo nahata kabla ya mgomo, muda wa wiki mbili ulitosha kujipanga, kwamba kama Serikaliikishindwa kutekeleza madai, AU kuonyesha njia mbadala ya kuyatatua basiijipange kuhudumia wananchi.
Kama leo hii tunaangalia luninga(TV-mfano Mh. W/Afya paleStar TV kukimbia), tunasikiliza redio lakini mambo yanayofanya na serikali nihaya, umekwisha jiuliza ingekuwaje, ama Serikali yetu ingetutendea nini kamatungekuwa hatuwaoni wanachofanya pale Bungeni(Mfano Takwimu za uongo), nakwingineko? Hali hii itaendelea hadi lini?
MKAKATI:
Usalama wa taifa wako kila hospitali, swali ni hili
1. Ni usalama wa Taifa au wa chama tawala?
2. Wanatumia pesa ya nani?
3. Last‘episode" walileta wanajeshi,
KAMA MADAI YAMADAKTARI SI YA MSINGI NA SERIKALI IKOSAHIHI KWANINI WANAJESHI HAWAJATOA HUDUMA KAMA WALIVYOTOA HAPO MWANZO??
KWANINI HAWAKUWA TAYARI HATA WALIPOOMBWA KUFANYA KAZIMNAYYOIITA KAZI YA WITO????

MAKOLIGI (colleague)??
Ni lini wananchi waliingia mkataba na sisi juu ya afyazao??sasa mbona wanatulalamikia na kutushambulia??..nadhani wananchi mnakoseakidogo, dhamana ya afya zenu ni kwa hiyo serikali "sikivu", hivyo lawama, maombi, na hisia zotepelekeni huko….ila sisi kurudi ni hadi pale madai yataposikilizwa, this time sikwenda kazini halafu yafanyiwe kazi? HAPANA..HII IELEWEKEVIZURI..HATUDANGANYIKI… hadi yafanyiwe kazi na kuthibitishwa au njia mbadala.
Najua wanasema when you get in a fight you should dig, twograves but I guess you should not fightwith someone who has NOTHING to loose,..We either overestimated the power of Government's responsibility orThey(Government) underestimated our power, and I really doubt of the latter because they KNOW they cant stopus.. you cant stop what you cant catch,because the more they will push us the worse this is going to get…
..Solidarityforever..
 
Kwa kweli uongozi unapimwa kwa jinsi mtu anatatua matatizo. Sasa watawaka wako kimya hakuna outrage lakini wakianza kuona machela na drips mitaani na kina Ananilea Nkya wanawashambulia ndio utaona hadi nawaziri wanaanza kutembelea mahospitali. Hii itabidi serikali nzima kujiuzulu.

MM,natamani sana ktk mgomo huu ambao ww unaushadadia,augue mama yako mzazi au baba yako na akose huduma ateseke kama wanavyoteseka mama zetu maskini.wewe upo nje ya nchi nyamafu,huoni pinch ya huu mgogoro kwa wananchi maskini
 
Unajua ni wangapi wanaoteseka tangu awali mpaka sasa?
mimi naona mateso yako na wanaoona mateso kwa wananchi
ni hawa madaktari.
 
Unajua ni wangapi wanaoteseka tangu awali mpaka sasa?
mimi naona mateso yako na wanaoona mateso kwa wananchi
ni hawa madaktari.

tunaoona mateso ni sisi wagonjwa,tunaokosa huduma wakati watu wanaopaswa kutupatia huduma hawataki huku wanapokea mishahara inayotokana na kodi zetu sisi maskini
 
Mara zote mgomo wa madaktari ni jambo la mwisho kabisa katika jamii; ni ishara ya mambo kuwa mabaya na ushahidi wa kushindwa kwa sera za walioko madarakani. Kuanzia mwaka 2006 wakati ule mgomo wa kwanza kuikumba serikali ya JK wengi wetu tulitarajia kuwa wangeonesha ubunifu na uthubutu wa kutatua matatizo yanayokabili sekta ya afya nchini. Hata hivyo, miaka zaidi ya sita baadaye madai yale yale, yenye kuhusu mambo yale yale yakielekezwa kwa viongozi wale wale yamekuwa yakitolewa na karibu mara zote majibu yamekuwa yale yale "tukae mezani tuzungumze".

Kilele cha haya ni mazungumzo ambayo wengine kwa kweli tuliyabeza kwa sababu hayakufikia makubaliano ya jumla. Naamini wakati huu serikali ni lazima ioneshe kuwa inaweza kutatua matatizo na madaktari waoneshe msimamo kuwa wanachogombania ni maslahi makubwa zaidi - nafuu kwa wagonjwa. Binafsi, naunag mkono mgomo huu endapo hatima yake itafikia kwenye kufanya mabadiliko makubwa ya sekta ya afya ambayo itaonekana kumjali mgonjwa na yenye kuhakikisha huduma ya kisasa, nafuu inapatikana kwa urahisi na kwa uhakika kwa watu wote.

Nikijua uzito wa mgomo huu na matokeo yake kwajamii nashindwa kujizuia bila kuunga mkono nikiamini kuwa viongozi hawana uwezo wa kutatua matatizo haya hadi yabane kweli kweli kama tulivyoona mgomo wa mwisho. Madaktari wakikaa tena chini kunywa soda Ikulu watakuwa wamepoteza uhalali wao; mazungumzo yoyote sasa ni lazima yafikie kukubaliwa kwa madai namabadilikombalimbali tena kwa maandishi na yaonekane kwenye bajeti ya afya.

Hatuwezi kuwa kwenye mgomo wa sekta hii kila baada ya miezi sita!!! Suluhisho la kudumu liwe tokeo kuu la mgomo huu.

I support the doctors!

kuwa kichaa sio lazima uokote makopo.kushabikia vifo vya watu wasio na hatia pia ni kichaa
 
MM,natamani sana ktk mgomo huu ambao ww unaushadadia,augue mama yako mzazi au baba yako na akose huduma ateseke kama wanavyoteseka mama zetu maskini.wewe upo nje ya nchi nyamafu,huoni pinch ya huu mgogoro kwa wananchi maskini

well.. huwezi kutaka mabadiliko kama mara zote unajifikiria wewe mwenyewe utakosa nini mabadiliko hayo yakitokea. Kama kweli una uchungu huo kwanini usiilalamikie serikali ya CCM na sera zake mbovu za afya ambazo zimeshindwa? Huu wala haukuwa mgomo wa lazima; umetokea kwa sababu ya watu kama nyinyi kuwaendekeza watawala walioshindwa; kuwapepea, kuwaimbia nyimbo za sifa na sasa badala ya kutaka serikali iwajibike kutatua mgogoro umekaa unawawakia watu ambao hata hawana uwezo wa kuanzisha au kuzuia mgomo!!
 
Nami naunga mkono mgomo wa madaktari. nashauri hata secta nyingine za wafanyakazi ziige ujasiri wa madaktari. Si kweli kwamba serikari haina hela, ukweli ni kwamba serikari inajari wanasiasa tu, haitambui mchango wa wengine.
 
Back
Top Bottom