Nawatakia EID Mubarak

Alhamdulullaah, nadhani imekuwa ni historia katika uislam, kufunga pamoja na kula Eid pamoja, huu ni muunganiko alioupanga Mwenyezimungu
ahhh historia gani unazungumzia?

wenzio SHIA BOHORA leo wamekula EID wao wanahesabu Tarehe badala ya Mwezi

all in all hata wale ANSAR kesho ngoma droooo

Hata lile baraka kuuu la waislam Tanzania (BAKWATA) hawajatia neno juu ya hili kwani zama za internet zimewapita kabisa
 
Last edited by a moderator:
Mina-al'idina Minalfaidhina. Umeconfirm kivipi? kwa uuona, kusikia kwenye redio, tv, rafiki, tujulishe zaidi. Thanks.
 
TAQABBALA ALLAAHU MINNAA WA MINKUM.


Jumapili Inshaa-Allaah ni tarehe 1 Shawwaal 1430H (20 Septemba 2009) na ndio Siku kuu yetu ya ‘Iydul-Fitwr.


Namuomba Allah Aliyetukuka Awajaalie furaha, amani, mapenzi, siha, Iman, karama na utukufu katika masiku yote ya uhai wetu.


Mwisho, bila kuwasahau wenzetu katika du'aa zetu leo na kila siku. Ndugu zetu Waislam waliopo palipokuwa Qiblah cha kwanza cha Uislam, na Msikiti wa tatu kwa utukufu na hadhi, Palestina. Na walio katika dhiki za ukandamizwaji, vita, njaa na machafuko huko Afghanistan, ‘Iraaq, Sudan, Somalia, Chechnya, Bosnia-Herzegovina, Kosovo, Philippine, Nigeria, Ethiopia, Eritrea, Kashmir na pote walipo Waislamu ulimwenguni.


Tunamuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutakabalie du'aa zetu na za Waislam wote duniani, Aamiyn

 
.... walio katika dhiki za ukandamizwaji, vita, njaa na machafuko huko Afghanistan, ‘Iraaq, Sudan, Somalia, Chechnya, Bosnia-Herzegovina, Kosovo, Philippine, Nigeria, Ethiopia, Eritrea, Kashmir ....

Pemba je? (charity starts at home)
 
TAQABBALA ALLAAHU MINNAA WA MINKUM.

Namuomba Allah Aliyetukuka Atujaalie furaha, amani, mapenzi, siha, Iman, karama na utukufu katika masiku yote ya uhai wetu.
 
Pemba je? (charity starts at home)
...bila kuwasahau wenzetu katika du'aa zetu leo na kila siku....pote walipo *Waislamu ulimwenguni.

*Ikiwemo Unguja na Pemba zote mbili, Tanganyika, Kenya haswa kule Mandera...
 
Aaamin! Eid mubaraka to ol. Natamani ningekua home shamrashamra nazikosa jamani. Ooh! Natamani ningerudi utotoni nguo za iddi si ki2 cha kuulza. Zinakua zimeshanunuliwa zamaniii. Suruali ya mchelemchele na shati ya bahama. Lol.
Enjoy your day
 
Leo unatukimbia, Tumeingia huzuni.
Bado twakuhitajia, Ubakie duniani.

Tulikwisha kuzoea, Kutukusanya nyumbani.
Ndugu marafiki pia, Mpaka na majirani.

Baraka kutupatia, Umoja pia amani.
Sote tunafurahia, Bila kinyongo moyoni.

Nawausia jamii, Bora tujitakaseni.
Kwa siku zilizobakia, Msamaha tuombeni.

Salam nawapatia, Eid na sitatu karibuni.
Ukifika kwa Jalia, ujue asema nini.

Kwaheri mgeni twalia, Mtukufu Ramadhani
 
Eid is the combination of 3 meaningful words

E - Embrace with open heart
I - Inspire with impressive attitude
D - Distribute pleasure to all

Happy~Eid Mubarak~
 
Kila la Kheir tuzidi kuyaendeleza yale mema tuliyokuwa tunayatenda katika mwezi wa Ramadhani na kuacha yote maovu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom