Elections 2010 Nawasihi viongozi wa vyama vya siasa msiruhusu tunayoyasikia kuendelea

Mtaka Haki

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
492
149
WASWAHILI WANASEMA MAJUTO NI MJUKUU.
Laiti viongozi wa Rwanda walipokuwa wanahimiza visasi kupitia radio wangeweza kujua ukubwa wa madhara yake. Laiti wanadamu wangepewa kuona kesho itakavyokuwa.
Ninapenda kuchukua nafasi hii kuwakumbusha wagombea wote kuwa kipindi hiki ustaarabu wenu utaonekana kwa jinsi mnavyothamini uhai na utu wa raia. Naamini hakuna mmoja wenu mwenye nia ya kutaka kuja kutawala maiti za watu. Kama mkiruhusu vurugu hizi ziendelee na mkaacha kuzikemea matunda yake hayatakuwa ya kungojea muda mrefu.
Nawasihi viongozii wa vyama vya siasa. Nawasihi viongozi wa dini tuhubiri amani.
Tutafarijika sana kama tutamsikia mgombea yeyote atakayetamka kuwa kuliko damu imwagike basi ni aheri akose nafasi ya uongozi.
Hekima na busara ya viongozi huonekana katika kipindi hiki. Ni vigumu kuficha uchu wa madaraka katika kipindi hiki kwa kuwa vipaumbele vya moyo wa mtu huonekana katika maneno yake na uamuzi wake wa dhati.
Uongozi ulimaanisha watu walioweza kuwafia watu lakini sasa hivi uongozi watu wako tayari kuufia na hata kuona wengine wakifa.
Uongozi uliotukuka ulifurahia kuona wazo lolote hata bora kuliko la kwako linaloweza kuwa la maslahi kwa watu. Uongozi wa sasa wazo lolote la maendeleo ya watu litatafutiwa kila uongo wa kulipinga ili mradi tu halitakupatia wewe sifa.
Rais mmoja aliwahi kusema “ TUNGEWEZA KUTIMIZA MENGI SANA KWA WANANCHI KAMA TUSINGEJALI NI NANI ATAKAYEPATA UTUKUFU AU SIFA”.
Ushujaa wa kweli wakati huu ni ule wa ni nani atakayetanguliza amani ya taifa na umoja wa taifa juu ya tama ya uongozi?
Ni nani atakubali hata kutamka tu kuwa niko tayari kuyakubali matokeo ya kweli hata kama nitashindwa na mwenzangu basi nitamuunga mkono katika hoja za kulijenga taifa?
TUNAKUSUBIRI RAISI WETU MPENDWA MH: JAKAYA MRISHO KIKWETE USEME TU NENO KUWA UNAPINGA KWA NGUVU ZOTE VURUGU ZINAZOFANYWA NA WAFUASI WA CHAMA CHAKO HATA KAMA WANAKUTETEA WEWE. PIA KAMA WANANCHI HAWATAKUPA RIDHAA YA KUONGOZA PAMOJA NA UGUMU WA UKWELI WOTE LAKINI UKO TAYARI KUSHINDA KWA KISHINDO UBINGWA WA KUTETEA AMANI HATA KAMA HUTASHINDA KURA.

TUNAKUSUBIRINI MHE DR. WILBROAD PETER SLAA NA MH. PROF. IBRAHIM LIPUMBA NA WAGOMBEA WENGINE WOTE KUTAMKA KUWA MKO TAYARI KUSHINDA USHINDI WA AMANI HATA KAMA MKIKOSA KURA MTAKUWA TAYARI KUPOKEA MATOKEO YA HALALI NA KUMUUNGA MKONO MGOMBEA ATAKAYESHINDA. NAOMBA MUWAKEMEE WANACHAMA WA CHAMA CHENU KUWA HAMKO TAYARI KUONA WANAMWAGA DAMU WAKIWATETEA NINYI. Hamtaki kuwa viongozi wa wafu bali viongozi wa Tanzania yenye walio hai.
Shime wenye kupeleka ujumbe. Naomba muufikishe ujumbe kwa viongozi wa dini na wa siasa. HATUKO TAYARI KUSIKIA TENA VURUGU. NINAAMINI KAMA KIONGOZI MMOJA TU ANGETAMKA MANENO YA HEKIMA NA HASA RAISI WETU MPENDWA BASI VURUGU ZINGEPUNGUA.
Wanachama wanafanya vurugu kwa imani kuwa wanawatetea viongozi wao. Ni mpumbavu tu anayeweza kufurahia kutetewa kwa damu. Ni ubinafsi uliokithiri endapo tutafikiwa mahali pa kufikiri kuwa watu wanastahili kufa ili sisi tuongoze au watu wanastahili kutufia wakitutetea.
Yupo wapi shujaa wa AMANI TANZANIA?
 
:A S thumbs_up: HUWEZI KUFIKA UNAKOTAMANI KUWA KWA KUBAKIA PALEPALE ULIPO.
KWA HIYO ........
WALE WALIOZOEA KUFANYA MAMBO NAMNA ILEILE WATAPATA MATOKEO YALE YALE WALIYOZOEA KUPATA.
KWA HIYO ......
 
Back
Top Bottom