Vipele na Muwasho sehemu ya siri (Uke, Uume): Chanzo, Ushauri, Kinga na Tiba

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
15,819
22,921
Msaada wana JF,

Mimi jinsia yangu ni ya kiume,huwa kuna vipele vinanitokea kwenye eneo la nywele za chini karibu na mdudu wangu,huwa vinaanza na muwasho taratibu ndani ya siku mbili vinajikusanya vinajiunga na kujaa maji halafu baada ya siku tatu au nne vinapotea.

Ninaweza kukaa miezi mpaka sita bila kuvipata lakini then huwa vinajirudia,nilichogundua ni kuwa vinanitokea nikifululiza tendo la ndoa au nikinyoa kipara huwa vinatokea.

Nina karibu miaka sita sasa tokea vilipoanza mara ya kwanza.

Kama kuna mdau mwenye ufahamu na aina hii ya ugonjwa anijuze.

Samahani, nahitaji msaada kwa wenye ujuzi wa haya mambo ya afya ya mwili.

Kila mara nikishanyoa sehemu zangu za siri natoka na vipele vingi sana ambavyo hunikosesha raha maana najikuna kila saa hata nikiwa kazini.

Naomba msaada kama kuna cream ambayo naweza kutumia wakati wa kunyoa au baada ya kunyoa ili vipele visitoke.

Huwa natumia vimashine vya kawaida vyenye kuweka wembe.

---------------------------------------------------------------------------------------
Ushauri kutoka kwa wadau

Mkuu kwanza nikupe pole,lakini hata hivyo sikushangai kwa kukosa amani kutokana na tatizo hili. Ni ukweli kwamba watu wengi hawana shaka na vijipele vinavyokuwa sehemu nyingine za mwili. Isipokuwa kwa uzoefu wangu wa miaka kadhaa ktk hii nyanja, nimegundua kuwa watu wengi wako makini sana na vipele vinavyotokea sehemu za siri.

Watu wengi wamekuwa nahusisha vipele hivyo na magojwa ya zinaa hasa kaswende(syphilis). Ni kweli kaswende inaanza na dalili za vipele/vidonda katika mwili isipokuwa sio lazima viwe sehemu za siri. Vinaweza kujitokeza sehemu yoyote hata mgongoni au hata kwenye makalio na vikapita bila mtu kujitambua.

Ikumbukwe kwamba vipele kama magonjwa mengine mengi havichagui sehemu ya kukaa ilimradi tu ni ngozi. Vipele vinaweza kutokea kwenye uso,ndani ya pua,kwenye vidole, hata kwenye masikio;mbona watu wengi hawajali?! Kwa hiyo kutokea kwa vipele sehemu ya siri sio jambo la ajabu,na hata kama vitapona leo,siku nyingine vitajitokeza tu.

Uzoefu unaonyesha kwamba mtu akinyoa kwa wembe wa kawaida,vipele lazima hujitokeza nywele zinapoanza kuota. Hapa nina maana ya nywele aina zote,ziwe za kichwani,makwapani au hata huko unakolalamikia. Na hili halihitaji cheti cha udaktari ili kuthibitisha,na ndio maana utakuta saluni wana dawa fulani wanampaka mteja baada ya kunyolewa. Kwani mkuu,vipi ukinyoa ndevu,hivyo vipele havitokei?!

Kiukweli kama hakuna tatizo lingine, kufanya tendo la ndoa hakuna uhusiano wowote na hivyo vipele. Huenda ikawa vilikuwepo kabla ya tendo hilo,wewe tu ndio hukuviona. Na hata kama ni ugonjwa wa zinaa,haiwezekani ukaupata na hapo hapo vipele vikatokea muda huo,sio rahisi.

Zipo sababu kadhaa zinazo sababisha vipele sehemu za siri:
-Magonjwa ya zinaa eg. Herpes Simplex,syphilis,etc
-Chawa(zinazopatikana kwenye nywele za huko chini)
-Kufuga nywele nyingi za huko chini(na bila kuzifanyia usafi wa kuridhisha)
-Kunyoa nywele za huko chini katika mazingira ambayo si ya usafi(hasa ukitumia wembe kwa mkono)
-Kuvaa underwears kwa muda mrefu bila kuzisafisha
-Kujifukizia perfumes kali kali huko chini
-Sometimes vipele vinaweza kujitokeza hata bila sababu yoyote ya msingi.

Nimetoa maelezo marefu hivi kutokana na kwamba kuna mahusiano mengi yamevunjika kutokana na uelewa mdogo juu ya jambo hili. Watu wamekuwa wakiwaona wenza wao wana tatizo hili moja kwa moja wanafikiria kuwa ni ugojwa wa zinaa. Na mara kadhaa watu wamekuwa wakitibiwa kwa gharama kubwa kwa kudhaniwa kuwa ni magonjwa ya zinaa.Biashara hii inafanyika sana katika zahanati na maduka mengi ya dawa ya mjini na vijijini.

Njia pekee ya kukaa kwa amani ni pale unapoona hali hiyo,mara moja unakwenda unafanyiwa uchunguzi/vipimo ili kujua uhakika wa vipele hivyo. Usikubali kutumia dawa kabla ya vipimo,utaibiwa na wakati mwingine unaweza kupata madhara kiafya kutokana na dawa hizo.

Kwa leo naona niishie hapa. Asanteni sana.

------
SWALI
Habari ndugu zangu,

Nina tatizo.Kuna vipele vidogo vidogo kama viwili vitatu na kadri siku zinavyozidi kuendelea naona kuendelea naona kuna vingine kwa mbali vinachipukia.

Nimejaribu kugoogle nione vinasababishwa na nini sijapata majibu coz mengi naona yanaelekeza kwenye magonjwa ya zinaa.

Vya kwangu mimi haviwashi but vinanipa wakati mgumu sana, na kuhusu mwananume ninaye mmoja tu na mara nyingi huwa tunatumia kinga.

Je, hili tatizo langu linasababishwa na nini? Au ndo nimeshapata magonjwa ya zinaa maana kuna wakati nahisi kama vinachoma choma kwa mbali. Au ni nyembe ninazotumia ktk shuhuli zima za kupunguza hizi nywele za ukeni?

Na je ni njia gani sahihi ya kupunguza nywele ukeni bila kupata madhara yoyote.

MSAADA PLZ!

JIBU/USHAURI
Habari na pole

Vipele sehemu za siri viko very trick, kuna vipele za joto kuna vingine zinatokea nyakati fulani katika mzunguko wako wa mwezi, nyingine kwa kushave, nyingine ni magonjwa.

Tukizungumza magonjwa ni mengi ila kwa maelezo mafupi uliotoa kwamba vi2 /3 na haviumi hayatoshelezi kukupa ushauri au kujua tatizo lako.

Kuna vipele nyingi lazima utueleze vilianzaje, vinaendeleaje, vimekuapo kwa muda gani, vinawasha haviwashi, vinatengeneza usaha au lah,Vina uhusiano na mens flw yako. Hakuna dalili zozote nyingine mkojo, maumivu au kuongezeka idadi uchafu ukeni any discharge.Masuala ya ngono salama.

Ukitaka nufaika zaidi muone mhudumu wa afya aviangalie magonjwa ya ngozi mara nyingi mwelewa akiona tu kwa macho anajua tatizo.

Epuka kwenda kwa madaktari wa uchochoroni watakupoteza
 
Mkuu kwanza nikupe pole,lakini hata hivyo sikushangai kwa kukosa amani kutokana na tatizo hili. Ni ukweli kwamba watu wengi hawana shaka na vijipele vinavyokuwa sehemu nyingine za mwili. Isipokuwa kwa uzoefu wangu wa miaka kadhaa ktk hii nyanja, nimegundua kuwa watu wengi wako makini sana na vipele vinavyotokea sehemu za siri.

Watu wengi wamekuwa nahusisha vipele hivyo na magojwa ya zinaa hasa kaswende(syphilis). Ni kweli kaswende inaanza na dalili za vipele/vidonda katika mwili isipokuwa sio lazima viwe sehemu za siri. Vinaweza kujitokeza sehemu yoyote hata mgongoni au hata kwenye makalio na vikapita bila mtu kujitambua.

Ikumbukwe kwamba vipele kama magonjwa mengine mengi havichagui sehemu ya kukaa ilimradi tu ni ngozi. Vipele vinaweza kutokea kwenye uso,ndani ya pua,kwenye vidole, hata kwenye masikio;mbona watu wengi hawajali?! Kwa hiyo kutokea kwa vipele sehemu ya siri sio jambo la ajabu,na hata kama vitapona leo,siku nyingine vitajitokeza tu.

Uzoefu unaonyesha kwamba mtu akinyoa kwa wembe wa kawaida,vipele lazima hujitokeza nywele zinapoanza kuota. Hapa nina maana ya nywele aina zote,ziwe za kichwani,makwapani au hata huko unakolalamikia. Na hili halihitaji cheti cha udaktari ili kuthibitisha,na ndio maana utakuta saluni wana dawa fulani wanampaka mteja baada ya kunyolewa. Kwani mkuu,vipi ukinyoa ndevu,hivyo vipele havitokei?!

Kiukweli kama hakuna tatizo lingine, kufanya tendo la ndoa hakuna uhusiano wowote na hivyo vipele. Huenda ikawa vilikuwepo kabla ya tendo hilo,wewe tu ndio hukuviona. Na hata kama ni ugonjwa wa zinaa,haiwezekani ukaupata na hapo hapo vipele vikatokea muda huo,sio rahisi.

Zipo sababu kadhaa zinazo sababisha vipele sehemu za siri:
-Magonjwa ya zinaa eg. Herpes Simplex,syphilis,etc
-Chawa(zinazopatikana kwenye nywele za huko chini)
-Kufuga nywele nyingi za huko chini(na bila kuzifanyia usafi wa kuridhisha)
-Kunyoa nywele za huko chini katika mazingira ambayo si ya usafi(hasa ukitumia wembe kwa mkono)
-Kuvaa underwears kwa muda mrefu bila kuzisafisha
-Kujifukizia perfumes kali kali huko chini
-Sometimes vipele vinaweza kujitokeza hata bila sababu yoyote ya msingi.

Nimetoa maelezo marefu hivi kutokana na kwamba kuna mahusiano mengi yamevunjika kutokana na uelewa mdogo juu ya jambo hili. Watu wamekuwa wakiwaona wenza wao wana tatizo hili moja kwa moja wanafikiria kuwa ni ugojwa wa zinaa. Na mara kadhaa watu wamekuwa wakitibiwa kwa gharama kubwa kwa kudhaniwa kuwa ni magonjwa ya zinaa.Biashara hii inafanyika sana katika zahanati na maduka mengi ya dawa ya mjini na vijijini.

Njia pekee ya kukaa kwa amani ni pale unapoona hali hiyo,mara moja unakwenda unafanyiwa uchunguzi/vipimo ili kujua uhakika wa vipele hivyo. Usikubali kutumia dawa kabla ya vipimo,utaibiwa na wakati mwingine unaweza kupata madhara kiafya kutokana na dawa hizo.

Kwa leo naona niishie hapa. Asanteni sana.
 
Mie hilo tatizo ninalo mpaka sasa zaidi ya miaka 13 nilikwisha fanya vipimo vya kila namna na kwa gharama kubwa kila kitu nilipima kila hospital nikiambiwa na rafiki zangu nakwenda zaidi ya mara 7 mpaka sasa nikifanya uchunguzi nikitu gani lakini hakuna majibu..nimeamua kuachana navyo huwa vinakuja nakupotea..kabla sijaoa na baada ya kuoa pia mambo ni yale yale..vinaweza kupotea baada ya miezi 6 vikaja vikaa 2 weeks vikapotea hivyo hivyo maisha yanakwenda..

Nakutia moyo usidhani huko peke yao tuko wengi tu..usafi nafanya tena wa hari ya juu..kama underwear nabadilisha kila siku..na kutumia medicated soap lakini hakuna kitu.
 
wewe ulikwisha wahi kupakaa spirit sehemu nyeti kama hizo?inawasha wewe asikwambie mtu,jaribu uone mwenyewe..
 
Poleni sn ndg zangu. Mimi nilikuwa na hilo tatizo kwa zaidi ya miaka 8 ktk seh hizo za siri. Dalili ni hizohizo, upele kutoka na kupotea. Nilianza kula na kupaka vitungu saumu pamoja na malimao. Nina zaidi ya miaka4 sijaona tena hilo tatizo.

Jaribuni inaweza kuwa msaada.
 
ndg wana jamvi nimekuwa nkipata vipele ving kila nitoapo nywele sehem za sir na hali hiyo inaninyima raha sasa naomba kuuliza je kupaka spirit sehem za siri kuna madhara gani?
 
ndg wana jamvi nimekuwa nkipata vipele ving kila nitoapo nywele sehem za sir na hali hiyo inaninyima raha sasa naomba kuuliza je kupaka spirit sehem za siri kuna madhara gani?

Sioni tatizo kwa sababu it's just the same skin, cha muhimu ujiandae kusikia maumivu from the affected areas.

That's my view..huenda wengine wakatofautiana nami..
 
Wewe ni me/ke?
Chonde isije ikaingia sehemu nyeti coz zingine ni kama vidonda.
 
Dawa ni kujiongeza ununue tu mashine ya kunyolea,achana na kiwembe cha mkono.Maana hata ukipaka spirit bado vipele vitatokea tu kutokana nahali ya unyevu unyevu ktk mitaa hiyo.Kama wewe ni me jiandae kuwashwa kwenye viazi vyako hapo chini,lakini kama ni ke jiandae kuwashwa ndani ya eden ikiwa kwa bahati mbaya inaingia miataa hiyo.
 
Tibu chanzo na si matokeo, vipele ni matokeo. Kujua chanzo nenda kwa daktari!
 
ndg wana jamvi nimekuwa nkipata vipele ving kila nitoapo nywele sehem za sir na hali hiyo inaninyima raha sasa naomba kuuliza je kupaka spirit sehem za siri kuna madhara gani?

Usitumie kiwembe zaidi ya mara moja yaani ukishakitumia unatupa ukitaka kunyoa kwa mara ya pili hakikisha unatumia kiwembe kipya na kuna viwembe vya siku hizi ni fake na butu tokea umekinunu dukani hivyo hakikisha unapata brand ambayo iko njema vinginevyo unaweza sababisha hata mpenzi waka wakati wa lile tendo letu lile akawa anaogopa kukupa maadhi ya mambo
 
kwani hasa ni njia ipi nzuri ya kuyoa nywele sehemu za siri.. naona mambo ya viwembe yanakasoro
 
Si lazima unyoe hadi kuwe kama upara ...halafu jaribu kutumia nyenzo maalumu kama zile za kunyolea ndevu na shaving foam.
 
Habari!

Nina tatizo la kutokewa na vipele sehemu za siri na kuacha alama nyeusi. Vinatokea pale napokuwa nimeshave, sasa vinyweleo vikianza kuota tu natokewa vipele vinawasha na kuweka alama!

Je, dawa yake ni nini? au nifanyeje nisitokewe na tatizo hilo?
 
Back
Top Bottom