Pole sana kamanda feki kwa kufiwa na mbunge wako,ni kweli inauma bana.
Kwa akili yako timamu unadhani hata jambazi akifa unataka tuseme R.I.P.? Be matured mazee!
Kumbuka kuwa siasa ni vitu vya kusadikika, hakuna dunia hii kiongozi hata mmoja ambae hana mpinzani, lakini upinzani wetu wa kisiasa usihusishe vitu ambavyo mimi na wewe havipo katika uwezo wetu, kama kifo. "Kifo Hakina Huruma" si kwa CCM wala CHADEMA.
Kila mmoja wetu ambae sisi tunapingana nae kuna wengine wanaomshangilia, mshabikia, mtegemea, mfatilia na wanao mpenda kiasi cha kwamba hata akifanya kosa wako tayari kumkingia kifua.
Sisi hatuna ugomvi na yoyote anaetutangulia mbele ya haki, ikiwa kaacha mema tutayataja, ikiwa kaacha uovu tutautaja, mradi isije jamii ikajifunza mabaya na kuacha mema.
Kumbuka kuwa "siasa" ni neno linaloashiria amani na kutumia njia za kufikia malengo kwa kukinaishana kwa mema zaidi, ikiwa leo tutaanza kususiana hata wafu, sasa inakuwa siasa au vita? Hata kanuni za kivita zinatoa mwanya kwa wafu kuheshimiwa.
Wana Chadema wanao mbeza marehemu kwa kuwa tu alikuwa Mbunge wa CCM hao si watu wa kawaida na sidhani kama wanaiwakilisha CHADEMA, hao ni wanazi na washabiki wasio kuwa na fikra hata kidogo na siwezi kuilaumu CHADEMA nzima kwa mapungufu ya wajivuni wachache.
Kijana we2 alikuwa bado mbichi, mzee sumari alikuwa mzee ni haki yake mzee kufa!