Nawapongeza police wa dar es salaam

kamili

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
1,213
849
Sitaki kusema lolote juu ya Mkutano waliofanya waislam kulaani mkanda uliokuwa unmkashifu Mtume Muhamad SAW. Lakini jambo moja lipo wazi kuwa kusanyiko lile lilifanyika licha ya katazo la Bakwata na pia police. Nasisitiza siungi mkono katazo hilo au kulikubali. Hata hivyo nawasifu police kwa kutokuingilia mkutano ule. Police wangekuwa na hekima hii tusingekuwa na historia mbaya ya mauaji yasiyo na sababu. Mauaji ya waislam wa mwembechai, ya kisiasa Zanzibar, ya Arusha, ya Mbeya, Songea, Morogoro, Iringa nk. (orodha ni ndefu). MKUKTANO ULE UMETHIBITISHA KUWA WATU WASIPOCHOKOZWA NA MABOMU YA MACHOZI AU RISASI WANAWEZA KUFANYA MIKUTANO YAO KWA AMANI NA KUTAWANYIKA BILA MAWE KURUSHWA AU MATAIRI KUCHOMWA. Nawapongeza police na mkiendelea na hekima hii Tanzania itabaki kuwa kisiwa cha amani.
 
Polisi waliogopa suicide bombers, maana walisha sema kuwa"wako tayari kufa kwa kutetea didni yao". Wewe unadhani muuaji haogopi kufa?!
 
Back
Top Bottom