nawapeni za jioni mgawo wa umeme umepunguzwa makali

Lukwangule

Senior Member
May 25, 2009
157
2
Shirika la Umeme nchini, Tanesco, kupitia meneja wake wa mawasiliano Badra , wamesema kwamba mgawo wa umeme upunguzwa makali yake baada ya mashine ya Kihansi iliyokuwa imetema mzigo kupona na IPTL kuingiza umeme wake katika gridi.
Mashine hiyo ya Kihansi ilikuwa inatoa megawati 60.
Meneja huyo hata hivyo hakusema IPTL imeingiza kiasi gani katika gridi.
hata hivyo alisema kwamba mgawo huo umepunguzwa makali kutokana na kiwango kikubwa cha umeme kuingia.
Alisema pia mafundiw anaendeleza harakati za mkukamilisha matengenezo ya mashine zilizobaki za New Pangani,Mtambo wa gesi wa Ubungo na kidatu.
Mashine hizo zinaweza kurejea kazini wakati wowote ule alisema Badra.
kwa wastani watanzania wanatafuna megawati 700 za umeme.
 
Hivi kwa nini IPTL wasiingie rasmi kwenye soko wakawa washindani wa TANESCO?
 
hapa kwangu umeme umekatika kuanzia saa tatu asubuhi mpaka sasa huu sijui ni mgao baridi ?boring Tanesko,Naona koroboi yangu inaishiwa mafuta
 
hapa kwangu umeme umekatika kuanzia saa tatu asubuhi mpaka sasa huu sijui ni mgao baridi ?boring Tanesko,Naona koroboi yangu inaishiwa mafuta

...........Pole FL1, nakuonea huruma na koroboi maana inatoa moshi si mchezo......jipinde shost ununue hata portable generator .
 
Hivi kwa nini IPTL wasiingie rasmi kwenye soko wakawa washindani wa TANESCO?

Wabongo bwana wala hata waga wahaeleweki wanataka na kutotaka nini...sasa leo hihi IPTL inayopigiwa kelele kwamba ni ya kifisadi tena ingiie kwenye ushindani wa kibiashara......yaani ni kweli kabisa VIONGOZI WETU NI PURE REFLECTION YETU WATANZANIA HALISI...
 
...........Pole FL1, nakuonea huruma na koroboi maana inatoa moshi si mchezo......jipinde shost ununue hata portable generator .

Pretty niko busy nasaka money angalau ninunue generator lakini pesa haionekani ,anyway angalau najitahidi kutimiza malengo yangu,weekend njema Pretty
 
Wabongo bwana wala hata waga wahaeleweki wanataka na kutotaka nini...sasa leo hihi IPTL inayopigiwa kelele kwamba ni ya kifisadi tena ingiie kwenye ushindani wa kibiashara......yaani ni kweli kabisa VIONGOZI WETU NI PURE REFLECTION YETU WATANZANIA HALISI...

Wewe hujui unachoongea. Shida ya "one track mind"

Ufisadi ulishatokea upende usipende na IPTL ipo, Dowan's ipo. Kuliko sisi kupitia TANESCO kuwalipa mamilioni wanayopata sasa si bora waingie kwenye ushindani halali?

Jaribu kufikiria nje ya boksi!!
 
kaka umebamiza baaaaaaaaam
 
Back
Top Bottom