Nawapenda watoto kuliko mume

afazali umewapenda watoto wako na sio serengeti boy au bosi wako wa kazini. big up.

analysis ya klorokwini: kwavile unawapenda watoto ina maana kila atakaewapenda watoto wako basi na wewe utajikuta unampenda automatically (hii ni psaikolojikal rule no.4).

ushauri wa klorokwini: mshirikishe baba watoto katika shuhuli za watoto na hakikisha watoto wanamfurahia baba yao, hii itakuathiri wewe umpende baba watoto kwa vile saikolojia yako itabadilishwa kupitia msingi wa penzi lako kwa watoto.

-THE END-
mkuu,
SWALAMA?

hivi world cup nyingine tena lini?
 
Tafuta washauri wa masuala ya ndoa au wanasaikolojia watakusaidia. Zaidi ya hapo, mpe nafasi. I mean, akichelewa kurudi nyumbani au asiporudi kabisa usimsumbue, usichunguze simu yake, mwache akapewe yale ambayo kwako hayapati na ni haki yake. Ni ushauri tu.
 
pole sana mdada....nadhani umeathirika na kitendo kilichotokea kwa mumeo, naomba nikuulize kama kabla hujamfumania pia ilikuwa hivi?
 
Tafuta washauri wa masuala ya ndoa au wanasaikolojia watakusaidia. Zaidi ya hapo, mpe nafasi. I mean, akichelewa kurudi nyumbani au asiporudi kabisa usimsumbue, usichunguze simu yake, mwache akapewe yale ambayo kwako hayapati na ni haki yake. Ni ushauri tu.

mbona umetoka nje ya ulingo kaka Mdoe? Lewisky hajafikai huko.
 
Habari zenu waheshimiwa mabibi na mabwana

Naomba ushauri wa jinsi ya kutatua tatizo langu la mapenzi ambalo mwenyewe linanikera na nahisi mwenzangu anakuwa mnyonge.

Ninahisi nawapenda zaidi watoto kuliko ninavyompenda baba yao. Muda wangu mwingi nautumia na watoto, kuanzia asubuhi kuwatayarisha kiusafi, kuwapa kifungua kinywa, na kuhakikisha wamekwenda shule kwa wakati stahiki. Baada ya hapo ni zamu yangu kujiandaa na kutoka nyumbani. Wakati mwingine nasahau hata kumwamsha baba watoto, kumwandalia nguo za kuvaa etc.

Nikirudi kutoka kazini jioni, nakuwa busy kutayarisha chakula cha jioni na baada ya hapo kuwasimamia na kuwasaidia watoto kufanya homework, na kuhakikisha kuwa wamelala wakati muafaka. Baada ya watoto kuwa wamelala naanza kufanya usafi wa nyumba, na kufanya maandalizi ya shule kwa watoto siku inayofuata, kunyoosha nguo zao, kuhakikisha kila mtu kaweka sawa vifaa vyake vya shule kwenye begi, na kuandaa snacks zao. Baada ya hapo huwa nahisi kuchoka mno na ninapoingia kitandani nalala fofofo.

Weekends niko busy na watoto kufanya shopping ya groceries, kutengeneza bustani, kufua, kucheza nao, kufanya homework na wakati mwingine kutembelea ndugu,jamaa na marafiki . Sina muda ambao naspendi na mume huyu na sijisikii kumpa attention ya kutosha. Mara nyingi huna naona ni wajibu wake kujimudu kwani ninahisi majukumu ya kuwalea na kuwasaidia watoto ndio ya kupewa kipaumbele, na wakati mwingine yananizidi.

Huwa nahisi anakuwa mnyonge. Hata nikijilazimisha, najikuta niko nae lakini mawazo yangu yote yako kwa watoto, huyu nahitaji kile, huyu kakosea hivi, huyu kafanya utundu huu na mawazo kama hayo. Wiki yangu huwa imekwisha na wiki inayoanza mchakamchaka wake ni hivyo hivyo.

Je kuna ambao hali hii inawatokea? Je mnakabiliana nayo vipi au ni mambo ya kawaida?
Naomba ushauri wa kukabiliana na hii hali kama sio ya kawaida, ili ni balance mapenzi.

Kwa nini usimueleze mkawa busy wote wawili kuwahudumia hao watoto? Mbona ni kazi ya wote wawili na pia mtakuwa mnamaliza kazi haraka. Au yeye hana mapenzi na hao watoto? Kama baba wa ki-leo anayeelewa majukumu yake, anapaswa kufanya yote ambayo unayafanya kwani hata watoto watajenga maadili ya kusaidiana.

Sijui mume wako ana umri gani au amelelewa kwa malezi yepi bali anapaswa kutambua kuwa mida hii siyo ya zamani ambayo mke anafanya kila kitu wakati mume amekaa au anakunywa kahawa. Malezi ya pamoja yatajenga pia upendo katika ndoa yenu. Mtakuwa mnazungumza lugha moja wakati wote.
 
duuu, ndoa yako ina miaka mingapi?? nina mfanyakazi mwenzangu ofisini ana ndoa ya miaka kumi na moja mke wake ni mzuri sana mchapa kazi ana adabu na huyo mfanyakazi mwenzangu anasema anampenda sana mkewe.Lakini ana nyumba dogo ambayo watu wote ofisin tunaijua kasoro mkewe. sasa huwa tunamuuliza hivi mkeo ana kasoro gani ya wewe kumcheat hivyo?? majibu yake ndio kama hiyo hadithi yako!mke yuko busy na watoto hana muda na mume so anakuwa lonely though ameoa!!!!!
ushauri: tafuta house gal uwezi kufanya vyote wewe uende job, watoto, usafi nyumba na mume unajidanganya !!
pili kilichowafanya muoane ni nini? lazima kuna common interest kati yenu tafuta hiyo anza nayo ili kumfanya awe karibu na wewe...
pia ongea na mumeo mwambie kwa ajili ya watoto ni vyema na yeye akawa anapata nao muda so kuwe na dady's day out na watoto na mum's days
vinginevyo blv me kuna mrembo anakusaidia mumeo kwa raha zake! ingawaje unaweza fanya yote hayo na bado akatoka nje ya ndoa but prevention is much better!!!
 
Muombe MUNGU akupe hekima na busara za kuweza kubalance upendo kati yako na mumeo na kati yako na watoto ili ndoa yako idumu na iwe na furaha, upendo na amani

Back
Top Bottom