Nawaombeni tumshauri huyu mtanzania mwenzetu

heshimu maamuzi yake, shika hamsini zako.lipitalo hupishwa kwani mchama ago hanyeli,huenda akauya papo na zaidi ya hapo, mtoto akililia wembe mpe.

Ukilazimisha unaweza kukutana na makubwa, madogo yana nafuu.

Heri nusu shari kuliko shari kamili, na asiyekubali kushindwa si mshindani. Vile vile tafuta mwingine wako kwani kila chombo kwa wimbile, ibilisi wa mtu ni mtu, pia dawa ya moto ni moto na avumaye baharini papa kumbe wengine wapo.usihofie mwanako kwani kuku havunji yai lake, wala usimtelekeze kwani damu nzito kuliko maji, na juu ya yote mshale kwenda msituni haukupotea.kumbuka mtupa jongoo hatupi na mti wake na mwana mpe mwanga kulea.

Usiwe na kisebusebu wala kiroho papo kwani kwa kila asemaye mla mla leo mla jana kala nini kuna jeshi la kusema ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno.

Mwapiza la nje, hupata la ndani ilhali usije kushangaa mwenda tezi na omo kurejea ngamani na ng'ombe avunjikapo guu hurejea zizini.

Kwa sasa ni hayo tu


ubarikiwe sana kwa kweli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom