Salama wakuu. Habari za jioni na poleni sana na majukumu ya ujenzi wa taifa? Natumai mu wazima. Niko karibu na kijana mmoja hapa anahitaji ushauri juu ya shida iliyomkuta ndani wiki mbili zilizopita. Hebu nivae koti lake na kuwaeleza kilichomsibu.
Naitwa X naishi na kufanya kazi mkoani Mbeya. Nina mchumba wangu aitwaye Y mabaye tulianza urafiki tangu mwaka 2009 ambaye kwa sasa anaishi Dar. kutokana na sababu ambazo wote hatukuzielewa mapema tulijikuta tuna mtoto mmoja amabaye sasa ana anakaribia kufunga mwaka wa pili. Tumeendelea kushirikiana kumlea huyo mtoto hadi leo na tumeendelea kupendana na kuheshimiana kama kawaida japo kuna mambo madodo madogo ambayo yalitufanya tugombane lakini tuliyaongea yakaisha.
Kutokana na hali ya kipato kuwa duni nimechelewa kukiri mbele ya wazazi wake kuwa mtoto ni wangu na kwamba mama yake(yaani mchumba wangu) nitamwoa, Japo wazazi wake wote wananifahamu na nahusiana nao vizuri lakini nilikuwa sijafanya ile mila.
Mara chache nimejaribu kufanya hivyo lakini nilishindwa kwa sababu ya kipato.(mimi ni fundi seremala) Miezi michache iliyopita nimejikusanya na kujikaba kila kona ili niweze kutimiza mila na hatimaye niweze kukabidhiwa mke na mtoto. Wazazi wangu wote wawili na wazazi wake wanajua juu ya maandalizi haya na kwa upande wa wazazi wangu, wameshajiandaa kwenda dar kutekeleza hili jambo. Mawasiliano yameenda vizuri lakini wiki mbili zilizopita mchumba wangu Y amesema tusitishe hii safari, unless kama naenda tu kuona mtoto wake, ila kwa upande wake yeye tayaria na mtu mwingine.
Sasa nimechanganyikiwa. nadhani hii imekuwa ghafla kwangu.
Naomba ushauri wenu, nifanyeje?