Nawakumbusha tu............!

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,709
Ni karibu wiki tatu zimebakia ifike ile tarehe ambayo watu huambiwa waoneshane upendo(hata kama mlikua mnavurugu inabidi muache siku hiyo)Najua siku hiyo watu hujiandaa kwa mambo mengi,ila jamani siku hiyo nyumba ndogo zimekuwa zikifurahia zaidi kuliko nyumba kubwa,nawakumbusha bado mapema,jitahidini siku hiyo jitahidini mjiandae mapema mburudike na familia zenu kwa mliooa,na wale wenye wapenzi waandaeni vyema mapema msitafute watu wapya wa kutoka nao siku hiyo,Na zaidi dumisheni upendo KILA SIKU.Kwa wale ambao hamjaoa wala hamna wapenzi kama mimi,kuweni makini nyakati hizi,wengi wanatafuta kampani na kuwezeshwa kimatumizi siku hiyo!Zaidi nawatakieni mahusiano/ndoa imara na upendo kila siku,ifanyeni siku ya WAPENDANAO kama changamoto ya kupima uhusiano/ndoa yenu ili iwe bora zaidi kila panapokucha! KILA IITWAPO LEO NA MZIDI KUPENDANA ZAIDI!......
 
Uko sawa,ila kwa watu wenye mapenzi ya kweli hawana haja ya kusubiri tarehe 14.2 ndio aonyeshe mapenzi siku hiyo.
 
Mkuu umenikumbusha shukrani...wacha nitafutie miwani mama Gaude wangu kuficha kengeza zake ambazo kimsingi naridhika nazo...ili nitoke naye,unajua bwana hakuna mkamilifu ndo maana wenye busara hawazungumzi kuridhishwa na wapenzi wa wengine kwa kutambua kua hao wapenzi wao wapya nao wamekosa uaminifu kwa walio nao ndo wakaja kuonesha mbwembwe kwao.
Regards!
 
Uko sawa,ila kwa watu wenye mapenzi ya kweli hawana haja ya kusubiri tarehe 14.2 ndio aonyeshe mapenzi siku hiyo.

Ndo maana nimesema zaidi mpendane kila siku!
 
Dah.....wiki tatu naona nyingi atii!! Eiyer umewaza nini mpaka kulikumbuka hilo au posa yako imekubaliwa??
 
Dah.....wiki tatu naona nyingi atii!! Eiyer umewaza nini mpaka kulikumbuka hilo au posa yako imekubaliwa??

Hata sijui,nimewaza tu kisweat,hakuna cha posa wala nini!
 
Sio utamaduni wa kibongo lakini umeshaweke mizizi. Ndiyo maana tunajisahau kuwa tuna matatizo taifa zima. Afew hours living in a PIMPERS PARADISE ndiyo tutalo ambulia.
 
Sio utamaduni wa kibongo lakini umeshaweke mizizi. Ndiyo maana tunajisahau kuwa tuna matatizo taifa zima. Afew hours living in a PIMPERS PARADISE ndiyo tutalo ambulia.

Hata kama tupo kwenye nyakati mbaya,zipo zile nyakati za kufurahia pia!
 
Thanks be to GOD, everyday its valentine in my life. :A S-coffee:
 
kwenye upendo wa dhati mapenzi ni kila siku wala hatuna haja na hiyo valentine coz haibadishi chochote!
 
Mapenzi ni kila siku
ila siku hiyo wanaopenda maua wapewe
tunaopenda fungu la mchicha tupewe
 
Mapenzi ya kuonyeshana siku moja ndani ya mwaka mzima sio mapenzi.

Umeona eheee? Kwangu mimi nashindwa kuelewa kabisa. Mi nadhani watu wanapaswa kuonyeshana upendo siku zote za maisha yao.
 
Back
Top Bottom