Nawakumbuka na siwezi kuwasahau

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
9,366
11,154
Nilipata ndoto juzi usiku iliyohusisha familia yetu, Leo asubuhi nikawa natafakari nayoyakumbuka wakati walipokuwa hai na pia kushare na wanajamvi nayoyakumbuka:


Baba
Ni marehemu takribani miaka 16 imepita. Mkimya na mkarimu…….mchapakazi hasa, alikuwa anakula "ngano" lakini ni wachache mno wangejua kama ni mtumiaji. Nakumbuka utotoni alishawahi kunichapa mara moja tu…..nilipokataa kunyoa nywele.


Mama
Mama yangu alifariki takribani miaka 13 iliyopita. Asubuhi ya leo nikawa nakumbuka jinsi alivyotulea familia ya watoto watatu na nyakati zingine extended family inaongeza idadi na hata kufikia saba au nane.


Maisha yalikuwa ya kupanda na kushuka lakini angalau hatukuwahi kulala njaa. Nakumbuka enzi hizo Baba alipokuwa hana kazi jinsi mama alivyokuwa anapiga hesabu zake ndani….mboga kiduchu, unga haba lakini tunamshukuru Mungu tunamanga nguna bila kumbagua yeyote ndani na kila mtu anaridhika.


Mpole na anyependa sana watoto wake, lakini si kwamba fimbo hatukuzipata la hasha panapo makosa hasa mimi nakumbuka alikuwa ananichapa on the spot ingawa sikuwa mtukutu viile.


Kaka yangu
Naye marehemu. Katika simulizi za mama mara kwa mara tukiwa wadogo alikuwa akisema wakati huyu kaka yangu akiwa mdogo kama umri wa miaka 3 alikuwa akimsumbua na kumuuliza kila wakati kwa nini yeye hana mdogo wake wakati wenzie wanacheza na wadogo zao?


Baada ya kuzaliwa mimi pengine kuliko watoto wote nilipata mapokezi ya kifalme kutoka kwa kaka yangu………..naambiwa ikiwa nitalia kdogo tu nitabembelezwa na kupewa nachotaka. Alinibeba, kuniosha na kunipikia, Kusema ukweli kaka yangu alinilea vizuri sana (wakati mwingine wazazi wangu walikuwa wanenda kutafuta rizki na kuniacha).


Sijui wewe unawakumbuka kwa lipi watu waliokupenda
 
Pole sana mpendwa
hapa duniani sisi tunapita lakini hatuwezi kuyasahau mema ya wapendwa wetu waliotangulia.
 
Kweli mkuu, sometims yanaumiza sana, mpaka unahisi uko pekeyako ulimwenguni.
Kikubwa ni kusubiri kwa kila linalotukutu, aliyetuumba anasababu ktk kila linalotusibu.

Nilishasahau na kuweka majonzi kando.......Ila kumbukumbu kama hiz si mbaya kuzirudia
 
Duu pole ndugu yangu! Ni vizuri kuwaenzi kwa kuchukua na kutenda mazuri yote waliyokuwa wanayafanya(hasa upendo wa kakaako) ili hata na wewe ukiondoka duniani upate wa kukukumbuka. Nami huwaenzi wale waliotangulia kwa kujitahidi kufanya mazuri waliyoyafanya wao.:A S cry:
 
Back
Top Bottom