Kiroroma
JF-Expert Member
- Feb 6, 2009
- 370
- 114
Mnataka iweje? ukikosowa utoe na ushauri kifanyike nini?
Tuwe waa kweli kidogo. ni Raisi gani aliyeshughulikia ufisadi Tanzania zaidi ya Kikwete? na bado anaendelea kazi yake haijesha, lakini tukubali kuwa Kikwete sio Dikteta na anafanya kazi zake kufata sheria, sasa nyinyi mlitaka akamate hovyo, aweke ndani hovyo, kama alivyofanya yule mmasai? enzi za Nyerere? au ule ndio mnaona utawala bora? wa kusweka watu ndani hovyo?
Yapo mambo ya kushabikia hili la kumshabikia Rais aliyeshindwa siyo jambo la kuchekelea kabisa ,haina tofauti na Shujaa aliyejisifia hadharani huku adui akimkaribia anatimua mbio na kudai ameshinda kwa makelele mengi bila mpango. Hebu mkumbuke Kemikali Ali wa Iraq.Huku tunaita kutapatapa.
Rais hapaswi kutoa habari zisizochujwa, kwani yeye kama kiongozi wa watu kauli yake ni ya mwisho, siyo ya kupapasapapasa umbeya umbeya. Alipaswa kumwita Mkuu wa TRA na kumwambia orodha hii hapa TIMUA WATU HAWA! Kama uchunguzi haujakamilika Kiongozi kaa yeye hapaswi kuzungumzia habari za kijiweni kwa wananchi.
Kwanza kajulishwa na washikaji tuu, not official statement. Sasa utawala wa sheria ni kuongoza nchi kwa majungu tuu na kuvizia vizia ofisi za watu? Atavizia ofisi ngapi kwa mtindo huo? Basi hata kule mipakani kuna matatizo aende basi,Kasumulu, Nandonde, Kyaka, Rongai na Namanga kwa staili hiyo hiyo.
Nchi ina sheria na taatibu za kaz kuna mfumo wa ufuatiliaji utendaji na kutoa taarifa. Iweje leo President ni M&E Officer wa serikali?