Nawahabarisha mambo kadhaa...

Hongera sana mwanakijiji na wote ambao mmekuwa mkichangia mada mbalimbali. Huu ni mwanzo tu, lazima kieleweke.
 
Heshima mbele Mwanakijiji.
Tutakuunga mkono, pamoja na ugeni wetu hapa kijijini. Endelea kukamua.
 
Hi Mwanakijiji,

I am very new to the JF, but I am getting more and more excited.

Ninafuatilia kila siku habari hapa JF na kweli watanzania sasa tume-advance.

Napenda nikupongeze na kukushukuru kwa kazi nzito unayofanya, and of course support will come just a matter of time.

Can't wait to hearing the Mwalimu Nyerere 'hotuba' and the sunday session as well


Good Luck.
 
Kati ya mambo ambayo nilikuwa nafuatilia ni la msiba wa vijana wetu hawa. Naomba niweke habari ambazo zimetolewa leo bungeni:

‘Waliohusishwa kuwaua Watanzania wamehojiwa’
Mwandishi wetu
HabariLeo; Saturday,November 03, 2007 @00:06

SERIKALI imesema kuwa watuhumiwa mbalimbali waliohusishwa na kuuawa kwa Watanzania, Walter Mazula na Vonetha Nkya nchini Marekani mwaka jana, wameshahojiwa kuhusiana na mauaji hayo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Seif Ally Iddi alisema kuwa licha ya watuhumiwa kadhaa kuhojiwa bado hakuna mtu aliyekwishakamatwa au kufikishwa mahakamani kwa kuhusika na mauaji hayo.

“Uchunguzi bado unaendelea…Idara ya Upelelezi wa kesi za mauaji ya Detroit, imeeleza ugumu wa kuelezea kwa kina ni hatua gani haswa waliyofikia kwa sasa kwani hali hiyo inaweza kuvuruga uchunguzi wao,” alisema.

Hata hivyo alisema Idara hiyo ya Upelelezi imeahidi kutoa taarifa ya jumla ambayo itagusia hatua iliyokwishafikiwa katika uchunguzi wao.

Hadi sasa serikali kupitia ubalozi wake wa Washington DC imekuwa ikiendelea kuwasiliana na maofisa wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Mauaji huko Detroit kwa ajili ya kupata maendeleo ya uchunguzi wa vifo hivyo.

Septemba 22 mwaka jana Mazula na Nkya waliuawa na watu wasiofahamika wakiwa huko Detroit, Michigan nchini Marekani.

Balozi Seif Ally Iddi alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Mfenesini, Mossy Suleiman Mussa (CCM), aliyetaka kufahamu kwa namna gani serikali imefuatilia suala hilo.
 
Wapendwa wana JF na Wasikilizaji wa KLH News,

Napenda kutumia nafasi hii kuwapa taarifa za mambo mbalimbali ambayo nimekuwa nikiyafanya na ambayo yana maslahi na wadau wengi hapa. Mambo haya ni yale ambayo aidha yamejadiliwa humu au nimewahi kuwapasha habari zake.

a. Suala la vijana Ukraine:

Suala la wanafunzi waliokwama Ukraine limefikia hatima yake, ingawa ni hatima ambayo mimi binafsi na wazazi wengi wa vijana hawakuitarajia. Tarehe 15 Septemba kundi la mwisho la wanafunzi waliokuwa Ukraine liliwasili nyumbani baada ya kuingia mkopo wa tiketi na deni lao "kushughulikiwa" na serikali. Kati ya wanafunzi wote 29 wachache walikwisha acha masomo, wengine walijirudisha wenyewe baada ya serikali kugoma kabisa na kundi hilo la mwisho ambalo hatimaye lilipatiwa tiketi na kuondoka Ukraine.

Ni mmoja tu ambaye hakuweza kuondoka kutokana na uzito wa ushiriki wake katika suala hili zima na hisia kuwa kwa vyovyote vile kurudi kwake Tanzania ingekuwa ni kushindwa kwa jitihada zote za kuhakikisha anaendelea na masomo. Huyo mwanafunzi mmoja kwa msaada wa wadau wa hapa JF tumeweza kuhakikisha amehama toka Chuo Kikuu alichokuwapo na kwenda chuo kingine ambapo familia yake wameahidi kujitahidi kumwendeleza na masomo kama tungewapa tafu kwa mwaka huu.

Tulifanya hivyo na ninashukuru wale ambao tuliwasiliana chemba na ambao waliitikia wito wangu.

Nashukuru kwa namna pekee serikali kwa ushirikiano walioonesha hasa baada ya kuamua kufanya mazungumzo ya chini kwa chini ambayo yaliwezesha vijana hawa kurudi nyumbani na zaidi ya yote kupewa nafasi nyingine ya kuendelea na masomo. Ingawa bado tuna issue ya wanafunzi wachache ambao tunaendelea kushughulikia ni matumaini yangu kuwa serikali hatimaye itaamua kuwasamehe deni la tiketi ambalo walitakiwa kulipia ndani ya miezi sita.

Mke wa Bob
Kwa wale wanaokumbuka mapema mwaka huu nilijitahidi kumuunganisha binti wa Kizambia ambaye alikuwa ameolewa na Mtanzania na waka wanaishi Angola. Mapema mwaka huu kijana huyo Bob alifariki dunia akitanguliwa na mtoto wake wa miaka kama mitano hivi.

Alipofariki mkewe alikuwa haijui familia ya marehemu na walikuwa wamepanga kwenda Handeni baadaye mwaka huu. Hivyo kijana huyo alizikwa Angola pasipo taarifa kwa wazazi wake au ndugu yeyote Tanzania. Ndipo jambo hilo likanifikia na kwa kutumia contactz zangu tukaweza kupeleka habari za msiba nyumbani kwa Marehemu na nikaweza kuwaunganisha mke wa marehemu na wazazi kwa njia ya simu na hatimaye kuwezesha mpango wa binti huyo kwenda kuwatembelea huko Handeni katikati ya mwaka huu.

Kwa hili namshukuru sana Mbunge wa Handeni Dr. Abdalah Kigoda kwa ushirikiano wote alionipa, na milele moyo wangu umejaa shukrani.

Ujumbe kwa Watanzania
Mapema mwaka huu pia kutokana na mjadala wa "Kuanguka kwa CCM, Unabii Utatimia" lilitolewa wazo la kuandika ujumbe ambao ungeweza kuelekezwa kwa Watanzania wote na ambao utakuwa na nguvu zaidi kuliko Makala ile ya awali. Ujumbe huo umekamilika na uko kwenye uhariri na utatolewa kabla tu ya kuanza kwa mkutano mkuu wa CCM.

Tovuti ya KLH News
Kama mnakumbuka katika mada ya "KLH Kufungwa" nilielezea ugumu unaonipata katika kufanikisha majukumu mbalimbali niliyojitwika ya kuwaletea maoni na habari na katika kutimiza dhana ya "hoja hujibiwa kwa hoja" na ya kuwa kwenye KLH News hapendwi mtu, hapendelewi mtu na haogopwi mtu.

Mwitiko wa wadau hapa umenitia moyo sana, wale ambao walitoa ahadi wachache wameshazitimiza na daima nawashukuru na wengine ambao ahadi zao bado ziko njiani ila kutokana na sababu mbalimbali wameshindwa kufanya hivyo hadi hivi sasa. Kwa wao natanguliza shukrani na pamoja nao navuta subira. Naomba watakaoweza kutimiza ahadi hizo wawasiliane nami kabla ya Novemba 10, 2007 kabla hatujafanya beta testing.

Nimeshapata wataalamu wa mambo haya ya kompyuta ambao kuanzia jana (tarehe 8 Oktoba) wameanza rasmi kufanyia kazi tovuti hiyo ambayo itakapokuwa tayari (matarajio ni wiki ya kwanza ya Novemba) itakuwa ni tovuti bora kabisa ya habari na maoni ya mambo mbalimbali kuliko tovuti nyingine yoyote ya Watanzania.

Lengo ni kuinua ubora wa tovuti za habari na kuziweka kwenye kiwango cha kimataifa. Matunda ya awali nimeanza kuyaona na ndugu zangu, I am impressed (and I don't get impressed easily).

Ninawashukuru
Nawashukuru wale wote ambao hadi hivi sasa wamewezesha kunipa taarifa, mawazo, maoni, ukosoaji na kusahihisha kila nilipopotoka. Natumaini tutaendelea hivyo tunavyoelekea mwisho wa mwaka. Muda ni mfupi lakini safari ni ndefu. Peke yangu siwezi na sitoweza licha ya kujitahidi sana, lakini kwa msaada wenu mambo mengi yanakuwa mepesi kufanyika.

Mniunge mkono na mimi nawaahidi sitawaangusha katika kila nifanyalo. Siwaahidi kutokosea, nawaahidi kuwa nikikosoea sitajificha au kuficha makosa yangu! Na nawaahidi siwezi kuanguka bila kusimama tena! Kwani kusimama nitasimama!

Hotuba ya Nyerere Mei Mosi

Katika kukumbuka miaka nane tangu Baba wa Taifa atutoke, Kuanzia kesho Jumatano (Oktoba 10) nitaanza kuwaletea sehemu ya hotuba ya Rais Nyerere aliyoitoa kwenye sherehe za Mei Mosi 1995 ambayo imebakia kama alama ya Nyakati. Kwa wale mlioangalia kipindi cha Jenerali on Monday mtakumbuka kuwa hata Prof. Beregu alinukuu toka kwenye hotuba hiyo.

NI hotuba ambayo kwa hakika ilionesha ni upeo na umahiri wa Mwalimu katika kujenga hoja. Kwa kadiri ninavyoisikiliza ndivyo kwa namna fulani naamini kuwa hotuba hii inaanza kunijenga kifikra kama zilivyofanya barua ya MLK na hotuba ya Mandela kizimbani. Natumaini mtachukua muda kusikiliza.

Na katika sehemu ya kumbukumbu hiyo natarajia kuwa na onesho maalum siku ya Jumapili kupitia bongoradio.com na natumaini kuwa na ugeni mkubwa kwenye show hiyo tunapoangalia nyuma na kumkumbuka Mwalimu. Nitawapa muda na jina la mgeni/Wageni pindi mambo yakitengemaa..

Ndugu yenu na Mtanzania mwenzenu,

M. M. M.
🙏🙏🙏
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom