Nawaachia malenga...

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,328
23,879
Habari zenu wandugu,
Ni mkasa ulomtokea kaka yangu. Japo nimeuweka in poem form, I hope haujapoteza maana. I hope kuna jambo tutalojifunza..Its areal life story, he is 34yrs now na bado hajaoa. Nimekuwa nikimsumbua kwa maswali ila juzi kaamua kunipasulia ukweli...Ingekua wewe, ungeendelea kupenda kweli!???

Machungu na simanzi, tele vimejaza moyo
nishajifunga kitanzi, sitaki kutiwa moyo
silitaki tena penzi, limenipondea moyo
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.

Penzi silitaki tena, moyo limenipondea
nilimpenda Irena, ngoma nilimchezea
hakuhitaji kunena, vyote nilimletea
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.

Minne nayo miaka, meno akanichekea
kajua mwisho wa mwaka, ndoa tutajifungia
kawajua zangu kaka, wazazi na dada pia
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.

Siku moja nimelala, simu nikaipokea
anajiita Matumla, tena akanifokea
mkewe niache mla, ndumba angenitumia
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.

Sa mi ningejuaje, Irena ameolewa
tumesoma wote nje, -kumbe- nyumbani anangojewa
linipoza wananjenje, na nyimbo nikatungiwa
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.

Miezi tisa kapita, na moyo nimeufunga
nikamuona Anita, upole ndo ulonifunga
kasahau yalopita, safari tukaifunga
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.

Mpole, mzuri sura, mcheshi nakuambia
kasoma Makutopora, mjeshi alotimia
n'kaapa h'watonipora, moyoni keshaingia
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.

Siku kuzaliwa kwake, keki nikamletea
kamlisha wangu mke, kisha kanitapikia
kamkimbiza Temeke, -ati- aleji memzidia
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.

Hongera nikapokea, ati ya miezi sita
kashindwa hata kulia, moyo kwenda ukasita
tulingoja hadi ndoa, vipi mama hukuniita
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.

Mengi mekutana nayo, Ana, Linda na Jesicca,
wamenichezea moyo, sitaki tena ushika
kitanzi nimeufunga, kupenda mpende nyie
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.

mh pole kaka
njoo kwangu ntakupenda

dahh pole mshkaji...bt jchek unakosea wap..uenda unakosea somewhre bila kujijua ..ata km unaprovide vyooooooooote bt kuna vtu tunaviitaji...ebu jchek fresh..uenda unakosea sehemu....

najua ni wewe si kaka yako wala nani.....:A S-baby:
 
Duh hv inakuwaje mke wa mtu unadanganya hujaolewa? Unakuwa na mategemeo gani hapo mbeleni? Kama unamtamani si useme tu ndio lakini nimeolewa! Ah masikini pole kaka kwa maumivu!

Rose napenda ulivyojitolea kumfariji shemeji!
 
Pole.Ni bahati mbaya tu umejikuta unapata wasichana wasio waaminifu.Ila wema na waamimifu bado wapo
 
mh pole kaka
njoo kwangu ntakupenda

dahh pole mshkaji...bt jchek unakosea wap..uenda unakosea somewhre bila kujijua ..ata km unaprovide vyooooooooote bt kuna vtu tunaviitaji...ebu jchek fresh..uenda unakosea sehemu....

najua ni wewe si kaka yako wala nani.....:A S-baby:

Dada Rose..Nitamshawishi aingie hapa akutafute..maana si mimi.
I am <25yrs...not yet married na nikisikia habari kama hizi ndo namuunga mkono mwanaFA kusema Bado nipo nipo sana!!!
Nilikuwa namtania kwamba sina pesa ya kumletea mbuzi..(sisi wachaga, kama mdogo atatangulia kuoa kabla ya kaka yake, basi itabidi umpelekee mbuzi)...ndipo akanipa stori yake.
Tumekuwa tukimtania sana kwamba siku moja tutamfungia ndani na mdada na iwe ndoa ivo...!!!
But after this..reallly...unamshauri mtu aoe kweli!???

Secondly, sidhani kama ana shida sna..labda umuone ndo umthaminishe...labda unaweza muonesha wat he doesn't see with his naked eyes!!!
 
Duh hv inakuwaje mke wa mtu unadanganya hujaolewa? Unakuwa na mategemeo gani hapo mbeleni? Kama unamtamani si useme tu ndio lakini nimeolewa! Ah masikini pole kaka kwa maumivu!

Rose napenda ulivyojitolea kumfariji shemeji!

Imagine huyu dada huwa namwonaga mara kwa mara..juzi ndo nimejua ukweli. Sote tulimfahamu, aliporudi bongo afta samtym tukasikia ana mme..ambacho hatukujua ni alikuwa keshaolewa longtym, katudanganya ati kaka yetu alikuwa anampotezea muda, damn!!!!!!
walisema wanaume ni wabaya..but i dont know what to say of her.
 
Mpe pole mwepesi wa kupenda ..vizuri.
Lakini pia anatakiwa afanye uchunguzi kidogo si kila atembeae ni mwema...
 
Sasa we unataka umwambieje?!“Yeahhh kweli bro usioe.“ Alafu siku ya siku we unakutana na mtu atakaekufanya uitamani hiyo ndoa....ukaingia na ukawa na furaha.Huoni kwamba utakua mchoyo??We mpe pole hayo mengine yaachie MUDA yajiweke sawa yenyewe....huwezi jua atakutana na nani next na huyo nani atakuaje....labda wote hao hawakua size yake alikua analazimisha.
 
Dada Rose..Nitamshawishi aingie hapa akutafute..maana si mimi.
I am <25yrs...not yet married na nikisikia habari kama hizi ndo namuunga mkono mwanaFA kusema Bado nipo nipo sana!!!
Nilikuwa namtania kwamba sina pesa ya kumletea mbuzi..(sisi wachaga, kama mdogo atatangulia kuoa kabla ya kaka yake, basi itabidi umpelekee mbuzi)...ndipo akanipa stori yake.
Tumekuwa tukimtania sana kwamba siku moja tutamfungia ndani na mdada na iwe ndoa ivo...!!!
But after this..reallly...unamshauri mtu aoe kweli!???

Secondly, sidhani kama ana shida sna..labda umuone ndo umthaminishe...labda unaweza muonesha wat he doesn't see with his naked eyes!!!

dah
aongee na wakubwa /wenye busara then awaelezee jins anavyoishi na wasichana wake ...
watatambua tatizo lake...
 
dah
aongee na wakubwa /wenye busara then awaelezee jins anavyoishi na wasichana wake ...
watatambua tatizo lake...

ok..wakubwa wanaogopa kumwuliza asijekurupuka kuingia kwenye ndoa...kisa walim-pressure sana!
Kuna wakati mama alimuuliza sana, mpaka yeye mwenyewe mama akajishtukia (only that she didnt know the truth!)..so, now wanaogopa kumuliza sana asije ona wanamlazimisha...!
wewe huwezi kumsaidia!??
 
kimawazo?naweza.
 
pouer sis...kama vipi ebu comment kaka afanyeje sasa?!
Well he should just take it easy asijistress na swala la kwamba hatokaa aoe au kupata mtu atakaempenda kweli na kua mwaminifu kwake.Nashangaa kwamba alikutana na binti nje alafu kabla hata hawajarudi nyumbani na kupata kujua background yake kidogo akaanza kufikiria maswala ya ndoa (kama sijaelewa tofauti). Hiyo inaonyesha anavyopenda haraka na asivyochelewa kukimbilia ndoani...kitu ambacho sio kibaya kama angekua amekutana na wasichana wakweli na waaminifu.Afungue moyo wake na ajiruhusu kupenda akitokea mtu atakaeushawishi moyo wake ufanye hivyo....ila sasa hivi ajitahidi sana kupata intel ya binti kwa kupitia binti mwenyewe na pia watu wengine wanaomfahamu.Maana kuna watu hata hua hawaulizi past ya mtu ilikuaje...wanadhani sio muhimu ila ni vizuri kila mtu akijua kwamba TODAY MAKES TOMORROW....na hata kama ya kale yalishaachwa bado ni muhimu kujua ni mtu wa aina gani unadeal nae.Kama mahusiano yake ya nyuma na kama aliwahi kuolewa ajue kwanini dada aliachika ili ajue wapi inabidi awe mwangalifu nae...au kama yeye ndie alieichoka ndoa pia ajue kwanini ili asifanye makosa kama ya mwenzake aliepita.All in all aache kusoma hatooa wala kupenda tena...hivyo viapo vitamfanya hata akikutana na mtu ambae ni genuine na akatokea kumpenda kweli ampite.
 
Pole yake aisee. Kweli ya leo sio ya jana, mwacheni atulie ipo siku tu atamuona wakumpenda. Ila mapenzi haya jamani mapenzi.......mweeeh!! Cjui kwa nini hayatabiriki!
 
Imagine huyu dada huwa namwonaga mara kwa mara..juzi ndo nimejua ukweli. Sote tulimfahamu, aliporudi bongo afta samtym tukasikia ana mme..ambacho hatukujua ni alikuwa keshaolewa longtym, katudanganya ati kaka yetu alikuwa anampotezea muda, damn!!!!!!walisema wanaume ni wabaya..but i dont know what to say of her.
Masikini hii ni sawa na wale wanaume wanaorubuni bila kusema kama wameoa au la! Pole sana Mentor ingawa limemkuta kaka yako naamini nawe pia limeitikisa imani yako juu ya mapenzi na ndoa pia. Maana kama mke wa ndoa anawezakudanganya hajaolewa wewe utapata wapi moyo kuwa mkeo wewe hatofanya hivyo?Jamani hv wanajamii hakuna researches zinazoweza kufanyika kwenye taasis hii angalau kuangalia trends za cheating, historical development, perceptions e.t.c pengine tunawezadevelop some indicators au causes za mvurugano huu!
 
Well he should just take it easy asijistress na swala la kwamba hatokaa aoe au kupata mtu atakaempenda kweli na kua mwaminifu kwake.Nashangaa kwamba alikutana na binti nje alafu kabla hata hawajarudi nyumbani na kupata kujua background yake kidogo akaanza kufikiria maswala ya ndoa (kama sijaelewa tofauti). Hiyo inaonyesha anavyopenda haraka na asivyochelewa kukimbilia ndoani...kitu ambacho sio kibaya kama angekua amekutana na wasichana wakweli na waaminifu.Afungue moyo wake na ajiruhusu kupenda akitokea mtu atakaeushawishi moyo wake ufanye hivyo....ila sasa hivi ajitahidi sana kupata intel ya binti kwa kupitia binti mwenyewe na pia watu wengine wanaomfahamu.Maana kuna watu hata hua hawaulizi past ya mtu ilikuaje...wanadhani sio muhimu ila ni vizuri kila mtu akijua kwamba TODAY MAKES TOMORROW....na hata kama ya kale yalishaachwa bado ni muhimu kujua ni mtu wa aina gani unadeal nae.Kama mahusiano yake ya nyuma na kama aliwahi kuolewa ajue kwanini dada aliachika ili ajue wapi inabidi awe mwangalifu nae...au kama yeye ndie alieichoka ndoa pia ajue kwanini ili asifanye makosa kama ya mwenzake aliepita.All in all aache kusoma hatooa wala kupenda tena...hivyo viapo vitamfanya hata akikutana na mtu ambae ni genuine na akatokea kumpenda kweli ampite.

Duh..well said! sitaki kumtetea sana ila he knew the lady for like 3 years...mpaka sisi wadogo zake tukamfahamu huyo dada, sijui kama alifanya haraka!?? si tulikujashtukia tu binti ana mume.
Well, langu somo nimelipata from your discussion....kuufungua moyo tena ndilo jambo ambalo nimemuusia, ila mi mdogo i hope alinisikia.
Yeye kabaki kuhudhuria vikao vya harusi tu..namwonea huruma but kama wadada wenyewe ndo hivyo!???
Haya huyo wa kwanza alikurupuka, huyu aliyepata mimba while they were in a relationship? kweli kaka alifanya haraka?? ama ndo his fate kuumizwa na wadada?
 
Back
Top Bottom