Nauza na kufuga Mapaka karibuni...

We acha tu Mkuu...Kuna siku nilialikwa kwa rafiki kwa ajili ya msosi. Sikujua kama nyumba ile kuna mapaka. Basi chakula kilipowekwa mezani mama mwenye nyumba akapotea kama dakika tano hivi chakula kiko mezani waziiiii basi mapaka manne yakarukia pale mezani na kuanza kudokoa dokoa chakula kile. Mie mkanda mzima nauona live. Nikaamua mara moja kwamba sigusi kile chakula. Sasa akili inanizunguka kutafuta uongo wa kutokula. Basi nikagundua uongo wa kuwaambia wenyeji ili nikwepe kile chakula maana yale mapaka manne yalichezea kile chakula na nilikuwa sijui chakula kipi kilichochezewa.

Basi nilipokaribisshwa rasmi nikaomba samahani jamani mie nilisahau kabisa kuhusu huu mwaliko hivyo nimekula kabla ya kuja hapa na vinono ninavyovipna juu ya meza najuta kwanini nilisahau. Yaani sina nafasi hata ya tonge mbili :):) Ila nitakunywa kinywaji na samahani nyingi sana kwa wenyeji wangu....Yaani mie na mapaka!!! ptuuuuuuuuu...:puke:
Hawakugundua kabisa sababu ya kuukwepa msosi ule.

Yaani walivyo wahalibifu...ntafuga mbwa lakini sio paka
 
Back
Top Bottom