Nauza kiwanja Mbezi kwa msuguri

Mutensa

JF-Expert Member
Feb 20, 2009
421
90
Wapendwa,
Nauza kiwanja. Kipo Mbezi (loius) kwa Msuguri kilometa 2.5 hivi kutoka main road. Kina slop na ni kizuri sana, maana utapata upepo mwanana ukijenga pale. Kama nusu kilometer kutoka hapo St. Thomas high school, nusu kilometer ipo St. Anne Marie School, na km 1 ipo Gift nursery and promary school. hii ina maana wanao watapata shule nzuri bila adha ya usafiri. Pia maji yapo, mradi wa wachina umefika huko ndo wako busy wanachimba mabomba. umeme upo karibu utahitaji nguzo moja au usihitaji kabisa (itategemea Tanesco baada ya kupima). Ukubwa 30x50. Barabara ya gari kubwa inafika pale pale site. Kina msingi japo umejengwa siku nyingi. Wasiliana nami kwenye mutensa@live.co.uk. hakuna haja ya dalali maana kiwanja hiki ni cha kwangu.
 
Mkuu tumekuelewa ungeweka na bei ya kuanzia kama sio ya mwisho.
 
6.5m wakuu maongezi yapo, waungwana hawawezi kukosa kuelewana. Kwa detailed negotiations tuwasiliane kwa email.
 
Nimevutiwa sana na wasifu wa kiwanja chako. Ingekuwa vema kama ungetutajia kadirio la bei yake!
 
Ile barabara ya kwenda Pugu mnadani si inapita mitaa hiyohiyo mzee,au wewe uko mbali kidogo.Barabara hii kwa macho haionekani lakini ndio njia ambayo zamani ilikuwa inatumika kupitishia ng`ombe toka pugu kwenda kiwandani kawe. Nisaidie hapo kidogo,mimi mwenyewe nataka.
 
6.5m wakuu maongezi yapo, waungwana hawawezi kukosa kuelewana. Kwa detailed negotiations tuwasiliane kwa email.

Kama maelezo yako ya awali ni sahihi kabisa.......bei siyo mbaya kivile kwa maeneo hayo mkuu!

Wakuu kazi kwenu......30*50m....is big plot anyway!
 
Ile barabara ya kwenda Pugu mnadani si inapita mitaa hiyohiyo mzee,au wewe uko mbali kidogo.Barabara hii kwa macho haionekani lakini ndio njia ambayo zamani ilikuwa inatumika kupitishia ng`ombe toka pugu kwenda kiwandani kawe. Nisaidie hapo kidogo,mimi mwenyewe nataka.

Mkuu hii barabara haipiti mitaa hiyo. Sehemu yenyewe unaingilia kituo cha mbezi kwa msuguri kwa mbele unakunja kulia kuelekea shule ya St. Anne Marie.
 
Mkuu Mutensa na wewe unaishi kule?Nataka j2 niende nikapacheki ili nifike bei.
 
30X50m? au 30miguu x 50miguu?..maana kwa uelewa wangu wa viwanja hasa maeneo uliyoyataja huwa hawapimi mita wanatumia miguu na mbaya zaidi huwa ni miguu ya muuzaji ambaye anatembea taratibu hatua ndogondogo ili shamba lake atoe viwanja 50 apate pesa nyingi...

please cofirm kama ni kipimo cha mita ili nianze kukushusha bei maana najuwa watu kibao watazichomolea hizo slopes za huko na huo udongo mfinyanzi wengu tunaufahamu kwa kupasua misingi ya nyumba...kama ni miguu wala sihitaji kuongea zaidi nakuwa nimeishajitoa katika list ya wateja wako watarajiwa
 
Mkuu Mutensa na wewe unaishi kule?Nataka j2 niende nikapacheki ili nifike bei.
mkuu siko mbali na mitaa hiyo. ukitaka kuona kiwanja tuwasiliane. Kwa maelezo zaidi tuma mail kaka ili tupeane na namba za simu, etc...
 
Wakuu kiwanja hiki kipo bado. Nimeona nitume tena ili muone tangazo. Ni-PM tuongee bei nzuri tu, original seller yuko pale pale hivyo hakina longo longo. 30mx50m. also you can email: mutensa@live.co.uk
Price 5,000,000 kama kwa negotiation, itapungua kidogo. Usiogope tutaelewana, i just need money.
 
Last edited:
Wapendwa,
Nauza kiwanja. Kipo Mbezi (loius) kwa Msuguri kilometa 2.5 hivi kutoka main road. Kina slop na ni kizuri sana, maana utapata upepo mwanana ukijenga pale. Kama nusu kilometer kutoka hapo St. Thomas high school, nusu kilometer ipo St. Anne Marie School, na km 1 ipo Gift nursery and promary school. hii ina maana wanao watapata shule nzuri bila adha ya usafiri. Pia maji yapo, mradi wa wachina umefika huko ndo wako busy wanachimba mabomba. umeme upo karibu utahitaji nguzo moja au usihitaji kabisa (itategemea Tanesco baada ya kupima). Ukubwa 30x50. Barabara ya gari kubwa inafika pale pale site. Kina msingi japo umejengwa siku nyingi. Wasiliana nami kwenye mutensa@live.co.uk. hakuna haja ya dalali maana kiwanja hiki ni cha kwangu.

Mkubwa nieleweshe kidogo hapo 30x50 sijaelewa ukubwa wake vizuri je imefika eka moja??Mimi nina kiwanja changu hiyo hiyo barabara kule karibu yanapoishia yale magari ya usafari I mean pale karibu na shule sasa sijui wewe!!
 
yaani JIRANI unataka kumuamisha mwenzako???duhhhhhhhhhhh
 
Mkubwa nieleweshe kidogo hapo 30x50 sijaelewa ukubwa wake vizuri je imefika eka moja??Mimi nina kiwanja changu hiyo hiyo barabara kule karibu yanapoishia yale magari ya usafari I mean pale karibu na shule sasa sijui wewe!!

...Nadhani ni zaidi kidogo ya NUSU eka kama tutakubaliana na vipimo vya wanaouza mashamba maeneo hayo kuwa Ekari moja ni maguu 70x70. Nisahihisheni.
 
Haya mahesabu ya maumbo yalikuwa yananipa taabu kweli. Kwa sababu kama 70 x 70 ni hekari 1, sijui 35 x 70 zitakuwa hekari ngapi, hasa ukitilia maanani kuwa 30 x 50 ni zaidi kidogo ya nusu heka!
 
....teh teh. Ngoja tungoje wajuzi wa hayo mambo waje hapa watujuvye!:)
 
Back
Top Bottom