Nauza harrier milioni 20 - t234 - bgq

Wewe unajua magari au unasimuliwa? Hakuna Harrier ya 900cc - 1300cc duniani, labda uwe umetengeza wewe. Cc ni equivalent na body, sasa kwa akili yako body ya Harrier inaweza kutembezwa na engine ya cc 1300?

Suzuki Swift au Corrola 111 itakuwaje? Kifupi na kwa uhakika Harrier inaanzia CC 2000- 2005 nyingi zina engine ya D4 VVTi.

Mwambie jamaa aweke picha ya engine tuone au akupe specification zake kama huamini.

Na wewe usigeuke chura kabla hujamaliza kusoma unaclick reply.

Hiyo niliyozungumzia cc ni Terios siyo Harrier.

Kijana nimeanza kuendesha kabla ya wewe kuzaliwa leo nisijue hata cc za engine?
 
Mkuu Bitimkongwe,

Inategemea matumizi yako let say unatoka nyumbani hadi ofisini lami tupu 2 - 5 km per day unaweza kukaa hata miaka minne bila kununua wish boan/Shock up.Mimi nakaa Arusha week end nakwenda Tanga shambani 250 - 300 km wakati narejea naweka na mzigo kati ya 100 - 250 kgs ukitumia Harrier ndani ya mwezi mmoja tu unaiweka juu ya mawe.Naizungumzia Harrier kwa maana ya maisha ya kiTanzania ya kuangaika lakini kama una mtazamo wa Bilicana... nunua mwenzako natumia Defender P/U mashine inapiga mzigo wa kufa mtu barabara mbaya mvua milima nakatiza utadhani mamba ndani ya maji.

Nameijua Harrier kupitia rafiki yangu anayefanyakazi UNICTR ni kweli inakimbia ,inatulia sana barabarani kama unataka kununua gari kwa kuangalia sifa hizo sawa lakini lazima utie akili disadvantages zake kwanza.Mwisho hiyo bei ni kubwa mno.

Sasa wewe kwa mahitaji yako ndiyo hasa unahitaji landrover maana yule ni kenge shida kwake ndiyo raha. Ukitumia Harrier, au mfano range rover kwa shughuli kama hizo utakuwa unazionea.

Mimi nnayo Harrier na nazungumza from experience kwa vile nimeendesha gari aina tafauti kwa miaka kadhaa. Nilipoinunua niliidharau lakini kwa kweli hivi sasa nimebadili mawazo.
 
tusiwakatishe tamaa jamani wenye ndoto za kumili harrier naamini kabla mtu hajanunua gari anaangalia vitu muhimu kwanza na urahisi wa kulimiliki na kulihudumia

Warning aliyotoa jamaa hapo juu kuhusu Harrier na zile Lexus zinazofanana na Harrier ipo hapo pekundu. Umiliki si ishu kubwa, ishu ni kwenye kulihudumia. Unajua wengine mkiwaza kuhudumia gari mnawaza mafuta na kubadili oili tu, wazeni na bei za vipuri na upatikanaji wake. Ni rahisi sana kumiliki Chevloret, Hummer, Citroen na Skoda kwa Tanzania, lakini je likiharibika vipuri vyake vinapatikana? Au ndio mwanzo wa kuegesha na kulitelekeza kwa fundi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom