Naunga mkono posha ziongezwe HASWA HAPA!

LATTICE BOND

JF-Expert Member
May 30, 2011
219
48
Kwa maelezo ya wabunge wanaotetea posho ni kwamba zinawasaidia kutoa misaada kwa raia wao wanaowazonga kila siku kuomba misaada mbali mbali! nami nasema hivi wafuatao nao waunganishwa kwenye mfumo wa posho za wabunge:-
1. Madaktari - wanakutana na wagonjwa ambao hawana hata nauli za kurudi makwao hivyo kulazimika kutoa sehemu ya mishahara yao kuwasaidia
2. Askari magereza - Wafungwa wanapomaliza vifungo vyao wakti fulani wanakuwa hawana hata nauli ya kurudi makwao hivyo askari magereza hao hulazimika kutoa fedha zao ili kuwapa nauli
3. Walimu - wanafunzi maskini wakati mwingine wanaenda shuleni bila hata daftari wala kalamu hivyo mwalimu hulazimika kutoa fedha yake ili yule mwanafunzi anunue daftari
Hayo ni baadhii ya makundi yanayohitaji kuongezewa posho. Swali langu kwa wabunge hasa wanaotembelea hii forum ni hili:-
"JE, WABUNGE WETU MKO TAYARI KUTETEA MAKUNDI HAYA?"
 
Kwa polisi ni muhimu kwani ili wafanyekazi nilazima wakae vikao vya kuwakabili waalifu na mambo ya polisi jamii
 
Back
Top Bottom