Naulizia Duka lenye flat screens na furniture za kisasa Dar not fake stuff

Jamani huku Bara flat screen ya inch 32 SINGSUNG inafikia 670,000/= hadi 720 ,000/= kwa Hitachi
Naambiwa TLC inaweza fikia 550,000/ hadi 600,000/= kwa bei ya hiyohiyo 32'
tusaidieni ni maduka gani? maana mm naanziaga Kariakoo Msimbazi, majuzi kati wamenibandika kanyaboya niokoeni nisije ibiwa hela

Bara wapi tukikutajia maduka ya Mwanza, Musoma au Bukoba kama upo Singida utasafiri kwenda kununua huko
 
Jamani huku Bara flat screen ya inch 32 SINGSUNG inafikia 670,000/= hadi 720 ,000/= kwa Hitachi
Naambiwa TLC inaweza fikia 550,000/ hadi 600,000/= kwa bei ya hiyohiyo 32'
tusaidieni ni maduka gani? maana mm naanziaga Kariakoo Msimbazi, majuzi kati wamenibandika kanyaboya niokoeni nisije ibiwa hela

karibia 60% ya maduka ya kariakoo ni bidhaa fake zilizobandikwa lebel za bidhaa zilizo katika soko duniani, hakikisha una mtaalamu kama una wasiwasi na bidhaa unayohitaji ila usiombe ushauri kwa muuzaji atakurubuni hasa vijana wenzetu hawa wa kitanzania wakigundua mtu hajui ndio wanakuchanganya kwa maneno ili uamini kuwa bidhaa wanazouza ni halisi.
 
rmashauri hiyo Orcadeco iko barabara ya mandela. Jengo moja na ilipo ofisi ya Maersk. Wana vitu vya ndani kiwemo sofaz, makabati, dinning tables&chairs na interior decor nyingi sana..
Ukweli niliona sofaz nzuri sina uhakika kama nilitupia macho leather maana mie nilienda kwa dhumuni la kununua kabati la nguo, nilipata kwa laki 5..! Nakushauri utembelee, hata jumamosi wanafungua!!

BJ, hili kabati ulilochukua ni mambao yetu haya ya mninga ama mpodo sijui? wasiwasi wangu kwa haya maduka ya kisasa mara nyingi ni malighafi wanayotumia kuundia vitu. Nilipokuwa kwenye ajira nilikuwa nashangaa fanicha za ofisini zilizokuwa zinanunuliwa kwa bei mbaya na wazee wa ten% wa ofisini kwetu kutoka maduka haya haya ya kisasa, zilikuwa hazidumu! lakini ilikuwa miaka 5/6 nyuma labda mambo yamebadilika.
 
Mkuu kama unataka genuine products kwa TV nenda pale Samora kuna agent wa Sony, Game pale Mlimani City usiende, kwani wana bei kubwa sana na ubora ni compromised. Kwa upande wa furniture nzuri fika pale LifeMate furniture barabara ya Nyerere karibu na Quality Centre au Monalisa opposite na Shoprite ya Kamata.

Nafikiri unamzungumzia yule bi mkubwa wa BISH International ama kitu kama hicho. Anajitahidi. nimenunua hapo mara nyingi vifaa vya electronic na vinadumu ingawaje pia ni yale yale ya 'Made in China ama Malaysia' nk.
Hii mara nyingi imenifanya nijiulize; Hivi hapa Dar/TZ hakuna maduka ambayo yanauza vifaa genuine kutoka Nchi vinakotengenezwa kwa maana ya tv, music system, dvd player nk kutoka Japan, simu za Nokia kutoka Finland nk?

nauliza wakuu, hivi ukinunua kitu cha electronic jeshini mfano hizo flat screen TV wanakupa na kadi ya warranty ile au inakuaje?
 
rmashauri hiyo Orcadeco iko barabara ya mandela. Jengo moja na ilipo ofisi ya Maersk. Wana vitu vya ndani kiwemo sofaz, makabati, dinning tables&chairs na interior decor nyingi sana..
Ukweli niliona sofaz nzuri sina uhakika kama nilitupia macho leather maana mie nilienda kwa dhumuni la kununua kabati la nguo, nilipata kwa laki 5..! Nakushauri utembelee, hata jumamosi wanafungua!!

Asante dada Belinda, nitawatembelea nikaone walivyonavyo.
 
Jamani huku Bara flat screen ya inch 32 SINGSUNG inafikia 670,000/= hadi 720 ,000/= kwa Hitachi
Naambiwa TLC inaweza fikia 550,000/ hadi 600,000/= kwa bei ya hiyohiyo 32'
tusaidieni ni maduka gani? maana mm naanziaga Kariakoo Msimbazi, majuzi kati wamenibandika kanyaboya niokoeni nisije ibiwa hela
Pale mlimani kuna Game,Samsung Store,LG Storena Hitachi store.Nilipitia maduka yote hayo na pamoja na kuwa watu tunakariri majina ya brand kama vile Samsung n.k niliona Samsung bei zao ni kubwa ,nilienda pale Hitachi wana TLC na Benq, kwa hakika nilipendezewa na Benq V42600 picha zake ni babu kubwa kuliko Samsung LCD,na bei hapo ni Tsh 1,500,000 wakati pale Samsung LCD ya 32 ni 1,700,000 na kwangu mimi ilibidi nichukue Benq
 
rmashauri hiyo Orcadeco iko barabara ya mandela. Jengo moja na ilipo ofisi ya Maersk. Wana vitu vya ndani kiwemo sofaz, makabati, dinning tables&chairs na interior decor nyingi sana..
Ukweli niliona sofaz nzuri sina uhakika kama nilitupia macho leather maana mie nilienda kwa dhumuni la kununua kabati la nguo, nilipata kwa laki 5..! Nakushauri utembelee, hata jumamosi wanafungua!!
Una roho nzur sana,hongera kwa hilo.JF tunajivunia kuwa hiv sio mtu anaomba msaada anapondwa kama nini.
 
Kwa wenye uzoefu na ununuzi wa flat screens na furnitures Dar naomba mnipe uzoefu wenu wa duka ambalo lina fare price but quality products nilizozitaja. Natanguliza shukrani.

It depends hiyo 'Fair price' ni ipi. Nyerere road ina maduka kadhaa ya furniture kama walivyosema wenzangu hapo juu. Kuna Orca Deco, lipo kabla hujafika Quality Plaza. Opposite yake kuna duka lingine la furniture. Pale Tazara kuna Funrniture Center, nao bidhaa zao ni nzuri sana. Nilinunua pale sofa nzuri kwa bei ya 800,000, sio leather lakini, 6 seaters. Zimetulia. Kuhusu TV, ni vema kwenda kwa wakala kwa sababu wanatoa garantee. Sony, Panasonic na Hitachi wana maduka clock tower mjini, makutano ya Uhuru na Nkrumah.
 
Back
Top Bottom