Nauliza wakuu wenzangu je jina lako lipo sehemu gani katika mwili wako?

mimi liko akilini.nikiitwa naitika..
Jina lako haliwezi kuwa Akilini ukitwa unaitikia kivipi? kama kweli jina lako lipo akilini?Jina lako lipo kwenye masikio yako mawili unapoitwa ukaitikia hapo ndipo penye makao makuu ya jina lako napo ni masikioni pako uko pamoja na mimi mkuu?
 
Kwa viziwi je?
Hapa umetuchakachua! Jina lako haliwezi kuwa masikioni..
Anyway, lakini kalikuwa kamchezo kazuri! Watu wamejikanyaga sana.
Kwa Viziwi hawana majina mkuu Rejao. nimeshajibu kuwa jina lako lipo kwenye masikio yako mawili hilo ndilo jibu sahaihi
 
hahahaaha Kwa sababu umenijibu hivyo mimi sasa nalijibu hilo swali nililokuwa nawaulizeni . Ni hivi jina lako au jina langu lipo kwenye sehemu ya MaSikioni mwilini mwako. Hilo ndilo jibu Sahihi Kwa mfano wewe ukiwa upo barabarani

mimi nikakuita kwa jina lako kwa mfano nikakuita jina lako ( klorokwini) kitu cha kwanza wewe utasikia kwa masikio yako mawili hiyo sauti aliyokuita ni nani? utageuka na kuniona mimi na kuitikia wito wangu. Mfano wa pili tukiwa tunaishi nyumba moja mimi na wewe, wewe ukawa jikoni mimi

nikawa chumbani nikakuita Mkuu kwa sauti ya juu ( klorokwini) wewe kitu cha kwanza utasikia kwa masikio yako mawili na kunijibu Naam Mzizimkavu unaniita nije? kwa hiyo jina lako lipo masikioni mwako hilo ndilo jibu sahihi asanteni samahanini kwa kukusumbueni sana.

I am not sure kama nimeridhika Mzizi.... Dah! Alafu mbaya zaidi wala sielewi kwanini sijaridhika.....
 
I am not sure kama nimeridhika Mzizi.... Dah! Alafu mbaya zaidi wala sielewi kwanini sijaridhika.....
mkuu bi AshaDiii bado tu hujaridhika? kwamfano mimi ni mume wako wewe upo jikoni unapika nikakuita kwa mfano tumezaa mtoto anaitwa omari mimi nikakuita kwa sauti ya juu kidogo mama omari wewe kitu cha kwanza utasikia kwenye masikio yako na kujuwa baba omari ananita na lazima utaitika Bee Baba omari unasemaje? mimi nikakuambia mletee mgeni chai utasikia kwa masikio yako ndio utaleta chai ili umpe mgeni wangu sio hivyo ? kwa hiyo jina lako lipo kwenye tundu za masikio yako mawili upo na mimi mkuu AshaDii?
 
aaaiisee!! Huo mfano naona umekaa sawa mpaka nimeelewa.....lol... Mzizi bana!

BTW kama kweli utakua na mgeni sitaitika "Bee Baba Omari Unasemaje" Nitanyanyuka na kukufuata na kusema "Bee mme wangu, kuna kitu unahitaji??"
 
:lol: naona sasa umeridhika hapo? nimetoa swali lingine angalia nimeweka Thread mpya
 
Back
Top Bottom