Nauliza tu

Hii inaonyesha kabisa wahusika wapo hapo hapo bank! Mimi nakushauri toa hiyo 25000 ili umfahamu mbaya then udai fidia. Kwa kuwa mbaya atakuwa ni muhusika wa bank hiyo hiyo
 
Hivi huduma za kuangalia camera Bank ni za kulipia?kuna ndugu yangu kaibiwa 1.2 M alikuwa anaandika baada ya kumaliza kujaza amount and all, that bahasha ya pesa ilikuwa pembeni sasa achukue ile bahasha ili aweze kuhesabu hela bahasha ikawaishachukuliwa pale pale bank,akatoa ripot na kuomba kama anaweza kucheki kwenye camera kaambiwa alipie sh elfu 25!(imetokea leo asb)Hii ni sawa kweli?labda cjui jamani.

Aende polisi na kuwasha moto kuanzia huko...
 
Yani kakamera ni kadogo aje!???????????????
huo ni wizi full..
 
najua mabenki yanatuibia sana na serikali inapaswa kuangalia upya sera, sheria na taratibu za mabenki ili kumlinda na kumtetea mteja wa benki. lakini kuna mtu katahadharisha kuwa huenda mhusika hakuwa na pesa na hiyo ni namna ya utetezi wake. lakini kama alikuwa na pesa na kaibiwa kweli, kwa hatua aliyokuwa amefikia, kwa mujibu nwa taratibu/regulations zinazoendesha benking hall, hahesabiwi kama mteja wa benki kwa vile hakuwa amefikia hatua ya ku-deposit wala hakuwa amemfikia karani wa benki na ndiyo maana ametozwa pesa. ,
 
Mhhhh P,

Mpe pole huyo dada...Hiyo ni Bongo Darisalam at work. Kwani ingekuwa imeibiwa pesa ya bank camera pia ingeelezwa kuwa inazunguka? Kama ni hivyo hata bank zenyewe haziko salama!
 
tatizo letu watanzania ni kutotumia vyombo vya sheria ingawa na vyenyewe ni corrupt..peleka hao crdb mahakami watampata mtu huyo mwizi..huo ni uzembe wa hali juu hawezekani camera isione tukio kama hilo ...ni deal hizo...au mwambie huyo ndugu yako atoe kwenye magazeti kuwa ameibiwa ndani ya benki na benki inasema haijarekodi tukio wakati ina camera...uone kama hao crdb hajamtafuta kumlipa kuondoa hiyo aibu kwa customer wake..... hizi dharau zetu za kuona 1.2 sio kitu eti utapata nyingine ndio inayopelekea kuwanufaisha watu wachache na wanyonge kuendelea kuibiwa kizembe..embu tafuta young lawyer apate kesi yakutokea...
 
Linapokuja suala la ushahidi wa Camera CRDB ni Benki mbovu sana! Nadhani watu wa IT wanashirikiana na wezi katika Benki ile. Hii si mara kwanza kusikia ujinga wao. Watu wengi sana wanaibiwa kwa Card za ATM na wakitaka kuona nani kachukua pesa inakuwa taabu sijui kwa nini? Nadhani Benki imejaa watu wanaoshirikiana na wezi..
 
Hayo mabenki ni ya mafisadi kwa hiyo watakusumbua na ka ni wenyewe wamechukua ndo basi tena vumilia tu omba katiba mpya ije
 
Huyo ni mteja wao,wamsaidie zikipatikana wakate vijisenti hivo vya camera. Na kama ikithibitika kuwa mteja wao kaeleza uongo, wamshitaki kwa kutaka kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu. Pole yake.
 
Hivi huduma za kuangalia camera Bank ni za kulipia?kuna ndugu yangu kaibiwa 1.2 M alikuwa anaandika baada ya kumaliza kujaza amount and all, that bahasha ya pesa ilikuwa pembeni sasa achukue ile bahasha ili aweze kuhesabu hela bahasha ikawaishachukuliwa pale pale bank,akatoa ripot na kuomba kama anaweza kucheki kwenye camera kaambiwa alipie sh elfu 25!(imetokea leo asb)Hii ni sawa kweli?labda cjui jamani.

Hata kwenye bus unaambiwa abiria chunga mzigo wako.

Ndugu yako mzembe
 
Mabank teller nao wana wizi sana. Muwe makini kusoma zile receipt kabla hamjasign.
Sometimes ukienda na eg laki udeposit anadondosha chini elf 10 halafu anakwambia umeandika laki wakati ni elf 90.
Bro wangu yashamkuta hayo.
Pole sana pearl.
 
I KNEW IT!!! IF NOT CRDB then NBC!!

Kuna uchafu unaoendela kwenye hizo benki hausemeki!! hasa January hii!
Hii January ina wizi sana kwa sababu watu wanatafuta ada za watoto , Desemba sikukuu walitumia pesa sana hivi sasa wamechacha na ada ya shule inatakiwa. Hii Benki kama Kimei asipokuwa makini kulinda wateja watu wataachana nayo kabisa! Haiwezekani ushahidi wa picha mteja auziwe , hii haikubaliki kabisa lazima wanashirikikiana na wezi.
 
Hivi huduma za kuangalia camera Bank ni za kulipia?kuna ndugu yangu kaibiwa 1.2 M alikuwa anaandika baada ya kumaliza kujaza amount and all, that bahasha ya pesa ilikuwa pembeni sasa achukue ile bahasha ili aweze kuhesabu hela bahasha ikawaishachukuliwa pale pale bank,akatoa ripot na kuomba kama anaweza kucheki kwenye camera kaambiwa alipie sh elfu 25!(imetokea leo asb)Hii ni sawa kweli?labda cjui jamani.

Poleni sana. Kwa kuibiwa 1.2m ningekubali haraka sana kulipia hiyo sh 25,000 ili kujaribu kumfahamu huyo mwizi na labda kuweza kuzipata tena hizo pesa.
 
Back
Top Bottom